Tuesday, November 3, 2015

FRED SWAGG AACHIA ‘NIMEWAKA’ MTANDAONI

IMG-20151102-WA0031
Na Modewjiblog, team
Mwanamuziki anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki Bongo, Fredrick Kalala ama jina la usanii akijulikana zaidi, Fred Swagg ameachia wimbo mpya mtandaoni ‘NIMEWAKA’ au ‘Nimelewa’.
Akizungumza na Modewjiblog kwa njia ya simu kutoka jijini Mwanza, Fred Swagg mkali wa vibao vya Maandishi alichowashirikisha Younf Killer na Kad Go. Ameeleza kuwa katika wimbo wake huo mpya wa Nimewaka, upo katika mahadhi ya rap, ni maalum kwa watu wa rika zote hasa sehemu za starehe ikiwemo Club.
“Wimbo huu mpya wa Nimewaka ni wa ku-Party’ ndani yake kuna komediani ikielezea watu wanavyotumia pesa na kulewa pombe za aina mbalimbali.. hivyo fans wakae mkao wa kula kuanzia sasa itakuwa mtandaoni ikiwemo mkito.com “ ameleza Fred Swagg.
Fred Swagg anabainisha video ya wimbo huo zinatarajia kuanza muda wowote kuanzia mwezi ujao huku kwa sasa akiendelea na promo za nyimbo zake zingine zinazofanya vyema kwenye vituo vya radio mbalimbali za ndani na nje wimbo wa ‘Kikomo’ aliomshirikisha Msanii, Da Prince na wimbo wa Maandishi aliowashirikisha Young Killer na Kad-Go.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More