Monday, July 31, 2017

MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.

Na fredy Mgunda, Mafinga


Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.


Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.

"Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80" alisema Makoga

Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.

Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.

Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga Zacharia Vang'ota wa kata changarawe,Chesco lyuvale wa Kata ya kinyanambo walimtaka Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuzisimamia ipasavyo sheria ambazo zimetungwa na halmashauri pamoja na serikali ya jamhuli ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Dr John pombe Magufuli ili kukuza mapato katika halmashauri hiyo.

"Ukiangalia hapa Mafinga tunavyanzo vingi vya mapato lakini watalaamu wetu hawavifanyii kazi ndio maana sisi madiwani tumeamua kuanzia sasa vyanzo vyote tulivyovibainisha leo kwenye baraza vifanyiwe kazi haraka sana ili kukuza mapato ya halmashauri yetu"walisema madiwani

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Mafinga Mjini walisema kuwa Mji huo una changamoto nyingi hivyo serikali ya mji inatakiwa kuanza kuzitumia hizo sheria Mpya haraka ili hata wananchi wayatambue maeneo yanayopaswa kulipa kodi na kuewezesha halmashauri kukuza mapato na kutatua changamoto za Mji wa Mafinga.

"Angalieni nyie waandishi Mafinga maji ni tatizo kubwa,Barbara bado hazijatengenezwa hasa huku mitaani kwetu,Mji bado mchafu kila mtu anatupa takataka anavyotaka kwa kuwa hakuna mtu wa kumkamata ila ukiangalia sheria Mpya zipo lakini hazifanyiwi kazi na Mafinga maeneo ya maegesho ya magari hayalipiwi wakati miji mingine ni moja vya mapato hivyo viongozi wanapaswa kuanza kuzitumia sheria Mpya" walisema wananchi

MAADHIMISHO YA NANENANE 2017 KITAIFA KUFANYIKA LINDI KUANZIA KESHO

Na Mathias Canal, Lindi
   
Maonesho ya Kilimo (NaneNane) yanataraji kuanza kesho Agosti 1, 2017 kote nchini kwa ngazi mbalimbali za kanda huku Maonesho hayo Kitaifa yakifanyika Mkoani Lindi huku Maandalizi na maonesho ya  Ki-Kanda yanaratibiwa na uongozi wa  mikoa husika.


Maandalizi ya Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane yatafanyika kwa siku 8 ambapo Kitaifa yatafika ukomo jioni ya Agosti 8, 2017 katika Viwanja vya Ngongo na Maeneo mengine yatakapoadhimishwa kikanda  katika  viwanja vya maonesho ni John Mwakangale –Mbeya; Mwalimu J.K. Nyerere –Morogoro; Themi – Arusha; Nzuguni -  Dodoma; Nyahongolo – Mwanza; na Fatuma Mwassa - Tabora. 


Maonesho ya mifugo sanjari na Maonesho ya Kilimo hutoa changamoto ya kuleta mapinduzi katika Ufugaji, Uvuvi, na Kilimo na kutoa ajira hususani kwa vijana kuwaongezea zaidi kipato na kuondoa umasikini. 


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ndg Mathew Mtigumwe wakati akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com  kueleza muktadha wa Maonesho hayo ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi na kubebwa na kauli mbiu mahususi kwa mwaka huu 2017 isemayo "Zalisha kwa Tija Mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati" 



Mtigumwe ameuambia Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com kuwa Wizara, taasisi/Makampuni ya umma na binafsi, Mabenki na wadau wote wa kilimo na mifugo wataendelea kuwasaidia wakulima na wafugaji hapa nchini ili kuongeza uzalishaji kuwezesha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyokusudiwa kuanzishwa. 

Malengo ya maonesho hayo ni utoaji elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi lakini pia wadau kujionea na kujifunza huduma zitolewazo na serikali, mashirika ya umma na binafsi. 

Teknolojia/Bidhaa zitakazooneshwa ni pamoja na zana za Kilimo, Mbegu bora za mazao mbalimbali, Uzalishaji wa mazao katika mazingira yaliyodhibitiwa ambapo piaTaasisi za kitafiti ambazo zitaonyesha teknolojia mbalimbali za kuongeza tija zenye ukinzani dhidi ya magonjwa mbalimbali, Utengenezaji wa chanjo dhidi ya magonjwa ya mifugo, Uboreshaji wa viasilu ili kupata mifugo na mazao ya kilimo yanayostahimili hali ya hewa kutokana na maeneo walipo wananchi wanaohitaji kujihusisha na ufugaji na kilimo na udhibiti wa magonjwa. 

Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta. 

Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yohusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binafsi, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yalifunguliwa tarehe 03 Agosti 2016 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe.


Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka. Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo.

Miaka ya 1990 sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.Ambapo Lengo la serikali likawa kuitumia Saba Saba kama siku ya maonyesho ya biashara ya kimataifa, ambapo wafanyabiashara wengi walijitokeza ama hujitokeza kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha na siyo kuwafundisha Watanzania mbinu za kuzalisha biadhaa hizo.

Picha zaidi zinaonyesha maandalizi ya Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi

UNAITUMIAJE TEKNOLOJIA KURAHISISHA SHUGHULI ZAKO ZA KILA SIKU?

Na Jumia Travel Tanzania

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia binadamu waliyonayo kwa sasa si jambo la kushangaza kumuwezesha mtu akafanya shughuli zako zote akiwa yupo sehemu moja ndanin ya muda mfupi.

Kwa mfano, kwa kutumia simu yako ya mkononi unaweza kutatua changamoto kadhaa hapo nyumbani kwako kama vile kufanya miamala ya fedha kutoka benki na kisha kutoa kwa mawakala huduma za fedha, kulipia umeme, kulipia maji, kulipia king’amuzi, kuagiza chakula, kuagiza usafiri, kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali.

Lakini swali ni kwamba, je ni watanzania wangapi wanaiona fursa hiyo iliyoletwa na teknolojia kama suluhu za changamoto tofauti zinazowazunguka?

MAMA NAMAINGO ‘AWAFUNDA’ AKINAMAMA WA GREEN VOICES KILIMOBIASHARA NA UJASIRIAMALI

Mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahim
Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka Hispania, Alicia Cedaba, akiwapa majukumu washiriki wa warsha hiyo.

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim, amewataka akinamama wanatekeleza mradi wa Green Voices Tanzania kuwa wabunifu na kutokata tamaa katika shughuli wanazozifanya.

MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI

Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA. Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo. Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu. Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo. Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo.[/caption] Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, ambao ni wafadhili wakubwa wa mtandao huo Bw. Christophe Legay kwa niaba ya Mkuu wa ofisi Bi. Zulmira Rodrigues amepongeza hatua iliyofikiwa na Radio wanachama ya kuunda mtandao mpya. Alieleza kuwa UNESCO itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na shirika hilo jipya la TADIO ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma sahihi za kihabari zitakazosaidia kuboresha maisha yao na kuchochea maendeleo ya upashanaji wa habari nchini. Bw. Christophe amehimiza kwamba vyombo vya jamii vinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha sauti za watu wanaowahudumia hasa wanaoishi vijijini. [caption id="attachment_2588" align="aligncenter" width="640"] Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe mara baada ya uchaguzi. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya TADIO, Maimuna Msangi na Katibu Mtendaji wa TADIO, Marco Mipawa.[/caption] Aliwaasa kushughulika na masuala ya kibinadamu na si watu binafsi. Wakati huo huo Mtandao huo unaoundwa na jumla ya Radio 32 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar, umefanya uchaguzi mkuu na kuwapata viongozi watakaosimamia shughuli zake kwa miaka mitatu ijayo. Uchaguzi huo ulitanguliwa na tukio la kujiuzuru kwa viongozi wa mpito waliochaguliwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya kutangazwa rasmi kuvunjika kwa muungano wa awali wa radio jamii wa COMNETA. [caption id="attachment_2589" align="aligncenter" width="640"] Katibu Mtendaji mpya wa TADIO, Marco Mipawa (kulia) akizungumza jambo mara baada ya uchaguzi kufanyika. Kutoka kushoto ni Balozi Mstaafu Mh. Christopher Liundi, Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay, Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize na Mjumbe wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi.[/caption] Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo ambae pia ni mlezi wa ushirika huo, Balozi mstaafu Mheshimiwa Christopher Liundi, alimtangaza Bw. Prosper Kwigize aliyekuwa mgombea pekee kuwa Mwenyekiti mpya baada ya kupata kura za ndiyo 26 kati ya kura 30 zilizopigwa na wajumbe waliohudhuria. Balozi Liundi, pia alimtangaza Bw. Marco Mipawa kuwa Katibu Mtendaji baada ya kupata kura 28 za ndiyo, Aidha Mipawa pia alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo. Viongozi wengine waliochaguliwa ni pamoja na Mweka Hezina, Shaaban Ali Makame aliepata kura 24 za ndiyo. Pia mkutano huo uliwachagua wajumbe sita wa Bodi ya shirika hilo la TADIO ambao ni Maimuna Msangi kutoka Pangani FM, Gladys Mapeka kutoka Radio Kilosa, Ali Mbarouk Omar kutoka kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari wa Pemba (PPC), Ali Khamis kutoka Adhana FM Zanzibar, John Baptist kutoka Dodoma FM na Anthony Masai kutoka Triple A FM. [caption id="attachment_2590" align="aligncenter" width="640"] Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi (kulia) akimpongeza akimpongeza Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize. Akizungumza baada ya kutangaza matokea hayo, Balozi Liundi aliitaka safu ya uongozi mpya kuongoza kwa kufuata katiba na malengo ya shirika hilo kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya wananchi kwa kupitia kazi zinazofanywa na radio za kijamii. Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa TADIO Bw. Prosper Kwigize amewashukuru wajumbe kwa kuchagua safu mpya ya uongozi na kuahidi kujenga ushirikiano mpya ambao utawezesha kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa kwa mtandao huo wa ushirikiano wa vyombo vya habari vya kijamii. Bw. Kwigize ametoa wito kwa wadau wengine hususani Radio za kitaifa, magazeti, waandishi wa habari za mitandaoni (bloggers) Muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT, TAMWA, MISA, Baraza la Habari Tanzania, Runinga na Vilabu vya waandishi wa habari mikoani kushirikiana na shirika la TADIO ili kutoa huduma stahiki kwa jamii. Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi akimpa pongezi Katibu wa TADIO Bw. Marco Mipawa (shati la kitenge) mara baada ya matokeo kutangazwa. Amehimiza pia serikali na taasisi zake kutoa ushirikiano kwa TADIO ili misimamo, dira na malengo yanayoibuliwa na serikali yawafikie wananchi kwa haraka kupitia muungano huo wa Radio za mikoani. Amesisitiza kuwa, mtandao huo wa TADIO una ofisi na studio ya kisasa ndani ya Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT makao makuu Kinondoni Dar es Salaam ambako kazi ya ofisi na studio hiyo ni kuratibu shughuli za mtandao pamoja na kuandaa vipindi ambavyo vitakuwa vikisambazwa kwa radio wanachama. Aliitaka safu ya uongozi mpya kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kujenga umoja na mshikamano pamoja na kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuyafikia malengo ya ushirika huo. Mtandao wa TADIO unafadhiliwa na UNESCO chini ya mradi wa SIDA/SDC. Msimamizi wa uchaguzi huo mwanasheria Harold Sungusia (mwenye tai) akimpongeza Mwenyekiti mteule wa TADIO, Prosper Kwigize. Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi na Msimamizi wa uchaguzi huo Mwanasheria Harold Sungusia.

Benki ya Watu iwa Zanzibar PBZ Yaibuka Kidedea Katika Mwajiri Bora Katika Ushirikishwaji na Chama cha Wafanyakazi ZAFICOW.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZAFICAW Bi. Rihii Haji Ali, akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh cha Mwajiri Bora Katika Ushirikiano na ZAFICOW kwa mwaka 2017. wakati wa hafla ya Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi ZAFICAW Bi. Rihii Haji Ali, akimkabidhi Cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh cha Mwajiri Bora Katika Ushirikiano na ZAFICOW, wakati wa hafla ya Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
 Viongozi wa PBZ na wa ZAFICOW wakiimbi wimbo wa ushirikiano wa Wafanyakazi wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti zilizofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar. 
Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar wakiimbi wimbo wa Wafanyakazi wa Mshikamano wakati wa mkutano wao na Mwenyekiti wa ZAFICOW wakati wa hafla ya bonaza la Michezo lililowashirikisha Wafanyakazi wa PBZ, 
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Rihii Haji Ali akitzungumza wakati wa mkutano huo na wafanyakazi wa PBZ kujuwa wajibu wao katika kazi na kuwataka kujiunga na Chama hicho kwa faida yao na maslahi kwa muajiri wao.Pia alikabidhi Kadi kwa Wanachama wapya ya PBZ 10 waliojiunga na kuwakabidhi Kadi za Uwanachama. 
Watendaji wa PBZ wakifuatilia mkutano huo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar Bi Rihii Haji Ali alipokuwa akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa Tamasha la Bonaza la Wafanyakazi wa PBZ lililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Wafanyakazi wa PBZ wakifuatilia mkutano huo na Uongozi wa PBZ na ZAFICOW uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Ndg. Suleiman Abdi, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Ndg. Bakari Hussein, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Fatima Ali Denge, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir Khafidh akimkabidhi Kadi ya Mwanachama mpya wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZAFICOW Bi. Mkunga Mohammed Saleh, baada ya kujiunga na Chama hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mkurugenzi Mtendajio wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ngd Juma Ameir Khafidh akimkabidhi zawada ya fedha shilingi miliono moja kwa kuibuka Mfanyakazi Bora wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa mwaka 2017  Ndg. Juma Ameir Makame (kulia) akishuhudia Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOW) Bi. Rihii Haji Ali hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mfanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg.Haji Masoud, akikisoma Cheti cha Mwajiri Bora Katika Ushirikishwaji katika Chama  cha Wafanyakazi cha ZAFICOW, wakati wa kukabidhi na Uongozi wa ZAFICOW.  
Afisa Muandamizi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Ndg. Anasi Rashid akizungumza na kutowa maelekezo wakati wa Mkutano huo wa Wafanyakazi na Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi Zanzibar Wafanyakazi Zanzibar (ZAFICOW)  
Mkurugenzi Rasilimali Watu PBZ Ndg. Mohammed Omar (kulia) akimkabidhi zawadi maalum iliyotolewa na Wafanyakazi wa PBZ kwa Boss wao wakati wa Mkutano huo na Wafanyakazi wa PBZ Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Juma Ameir Khafidh akitowa nasaha zake kwa Wafanyakazi wakati wa mkutano huo ulioambatana na michezo mbalimbali iliowashirikishwa Wafanyakazi kujumuika pamoja na kubadilishana mawazo Bonaza hilo limefanyika katika ufukwe wa Hoteli ya Visiter Inn Jambani.Mkoa wa Kusini Unguja.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg. Juma Ameir Khafidh akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na Wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Visiter Inn Jambiani Zanzibar.


Wafanyakazi wa PBZ wakipata viburudisho ya maji ya madafu baada ya mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Visiter Inn Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.

Sunday, July 30, 2017

MCHAPALO WA MIAKA 50 YA BENKI YA NBC WAFANA JIJINI MWANZA

Na George Binagi-GB Pazzo Jana Julai 28,2017 usiku wa kuamkia leo jumamosi, mchapalo (sherehe) wa kusherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa benki inayolitumikia Taifa la Wachapakazi, NBC umefana Jijini Mwanza ambapo benki hiyo imekutana na wadau wake wakiwemo wafanyabiashara. Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NBC, Theobald Sabi alisema maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Mwanza ikizingatiwa kwamba Jiji hilo ni la pili kwa ukubwa nchini na kwamba inao wateja wa muda mrefu wanaohudumiwa kwenye matawi yake matatu hivyo ni jambo jema kujumuika nao pamoja. "Hakika NBC ina historia ndefu katika kujenga uchumi wa nchini yetu, ni jambo lisilopingika kwamba NBC ni mama wa benki za kibiashara hapa Tanzania". Alidokeza Sabi huku akiwashukuru wafanyakazi wa benki hiyo waliojawa uzalendo, umakini na ubunifu katika kazi. Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein alisema moja ya hatua za benki hiyo ni kuwa kitovu cha malipo yote nchini (National Payment System) mfumo ambao hadi sasa unategemewa nchini. Alidokeza kwamba miaka ya 70 mbali ya kutoa huduma nchini nzima, vile vile benki hiyo ilikuwa ikitoa huduma kwa njia ya mawakala, ikawa mwanzishi wa mobile banking pamoja na huduma za bima. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Merry Tesha aliipongeza benki ya NBC kutokana na mapinduzi yake kwenye sekta ya kifedha nchini na kuiomba kuwekeza moja kwa moja ama kwa ubia katika utekelezaji wa azima ya serikali ya ujenzi wa viwanda nchini ikiwemo kutoa mikopo kwa wawekezaji wa ndani. [caption id="attachment_27640" align="alignnone" width="620"] Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Merry Tesha akizungumza kwenye mchapalo huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.[/caption] [caption id="attachment_27641" align="alignnone" width="620"] Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NBC nchini, Theobald Sabi, akizungumza kwenye mchapalo huo wa miaka 50 ya NBC[/caption] [caption id="attachment_27642" align="alignnone" width="620"] Mkurugenzi wa bodi ya benki ya NBC, Dr.Kassim Hussein, akizungumza kwenye mchapalo huo[/caption] [caption id="attachment_27643" align="alignnone" width="620"] Mmoja wa wateja wa benki ya NBC akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya wateja wengine kwenye mchapalo huo[/caption] [caption id="attachment_27644" align="alignnone" width="620"] Burudani kutoka kikundi cha ngoma asili, Mwanza Dance Group kikitumbuiza[/caption] [caption id="attachment_27645" align="alignnone" width="620"] Mgeni rasmi, viongozi wa NBC na wageni waalikwa wakifungua muziki kwenye mchapalo huo[/caption] [caption id="attachment_27646" align="alignnone" width="620"] Afisa Mahusiano Jiji la Mwanza, Elirehema Kaaya (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein (kulia) kwa utendaji kazi mzuri wa benki ya NBC nchini.[/caption] [caption id="attachment_27647" align="alignnone" width="620"] Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein (kulia), akipokea pongezi kutoka kwa Afisa Mahusiano Jiji la Mwanza, Elirehema Kaaya kuhusu miaka 50 ya benki ya NBC kulitumikia Taifa la Wachapakazi.[/caption] [caption id="attachment_27648" align="alignnone" width="620"] Mchapalo/ sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa benki ya NBC[/caption] [caption id="attachment_27649" align="alignnone" width="620"] Mgeni rasmi, viongozi wa NBC pamoja na wageni waalikwa kwenye picha ya pamoja[/caption] [caption id="attachment_27650" align="alignnone" width="620"] Selfie kufurahia miaka 50 ya benki ya NBC[/caption] [caption id="attachment_27651" align="alignnone" width="620"] Hakika Ukubwa Dawa, BMG tunatoa pongezi za dhati kwa benki ya NBC kwa kutimiza miaka 50 tangu kuanza kulitumikia Taifa la Wachapakazi Tanzania.[/caption]
Tazama HAPA uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki ya NBC Jijini Mwanza

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More