Wednesday, June 28, 2017

KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO.

Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari .

Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) ,Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MSIKITI WA RIADHA MJINI MOSHI.

Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa akiwasili katika msikiti wa Riadha mjini Moshi kwa ajili ya Swala ya Eid el Fitri iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa aikishiriki Swala ya Idd el Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakishitiki Swala Idd.
Swala ya Idd ikifanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa,akiwa na Sheakh Mkuu wa Tanzania ,Mufti Abubakary Zubery ,Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu ,Said Mwema.
Mshindi wa kuhifadhi Quran tukufu ,Ibrahim Mitigo akionesha namna ambavyo alivyohifadhi Quran wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika katika msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki Swala ya Idd mjini Moshi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,akizungumza wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika kitaifa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Mufti wa Tanzania na Sheakh Mkuu,Abubakary Bin Zubery akitoa nasaha zake wakati wa Swala ya Idd iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki katika Swala ya Idd El Fitry iliyofanyika mskiti wa Riadha mjini Moshi

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya mauaji yaliyotokea Kibiti,Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha wanafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.
Waziri Mkuu wa Tanzania ,Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika baraza la Idd lililofanyika kitaifa katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro lkitanguliwa na Swala ya Idd El Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha.
“Kinachofanyika sasa nikuhakikisha kwanza tunawapata waharifu halisi ilikuepuka kuingiza watu wasio husika, kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji haya yanafanywa labda na waislamu hapana .”alisema Mh Majaliwa .
Alisemakaz kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja na kujua nani hasa anshiriki katika mauaji hayo huku akiwashukuru watanzania ambao tayari wameanza kutoa ushirikiano kwa kuanza kueleza nani wanahusika katika tukio hilo.
“Kazi yetu ni kuwapeleleza pale ambapo tunauthibitisho wa ushiriki wao na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kazi hiyo inaendelea vizuri.”alisema Majaliwa.
Mapema katika taarifa ya Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyosomwa na kaimu katibu Mkuu,Sheakh Salim Amir Abeid alisema Bakwata imeshtushwa na matukio ya mauaji ya kutisha ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani.
Alisema kutokana na matukio hayo Baraza kuu linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo aliyoyataja kutokuwa na hata chembe ya kibinadamu .
“Kumekuwepo na matukio ya kutisha ya mauaji ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani,matukio ambayo yametushtua sana na kuisikitisha mioyo yetu,baraza kuu la waislamu la Tanzania kwanza kabisa linatoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika matukio hayo ya kinyama yasio na chembe ya kibinadamu hata kidogo.”alisema Abeid
Alisema Bakwata inasikitishwa na vitendo vyenye viashiria vya kutaka kuichafua dhima nzuri ya Tanzania kuwa ni kisiwa cha amani na utulivu hasa pale matukio hayo yanapo husishwa na na Dini ya Kiislamu.
“Uislamu ni dini ya amani upendo kuvumilia na nakuishi pamoja na watu wa imani tofauti na kwamba yeyote afanyae matendo yoyote na kinyama kama hayo katu haiwakilishi uislamu na baraza linawataka waislamu kushikamana.”alisema Abeid.

Mwisho.



WAISLAMU WATAKIWA KUENDELEZA UCHA MUNGU

Na Swahilivilla Washington Waislamu wametakiwa kuendeleza Ucha Mungu na mema waliyokuwa wakiyafanya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Yussuf Mecca, kutoka Columbus, Ohio
Wito huo ulitolewa jana na Sheikh Yussuf Mecca alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Iddi zilizoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania wa Jiji la Washington na Vitongoji vyake ijulikanayo kwa jina la TAMCO.
"Kwa vile mwezi wa Ramadhani umekwisha isiwe yale yote mazuri tuliyokuwa tunayafanya ikawa ndiyo basi, na tusubiri Ramadhani nyengine" alisema Sheikh Yussuf.
Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kujitahidi kumcha Mungu wakati wowote na kujitahidi katika kutenda mambo mema na ibada ili kujiandaa na safari ya Akhera ambayo inanaweza kumfikia mtu wakati wowote.
" Hakuna hata mmoja ambaye anajua ni siku gani atafumba jicho na atakufa", alisisitiza Mgeni huyo rasmi kwenye shere hizo, huku akitilia nguvu hoja yake kwa Aya ya Qur'an isemayo: "كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ" (Kila nafsi itaonja mauti/kifo), akigogoteza kuwa hakuna mtu yoyote anayejua atakufa lini au mahali gani.
Aliongeza kusema kuwa kurejea kwenye maasi baada ya juhudi kubwa za ucha Mungu na ibada katika mwezi wa Ramdhani ni sawa na kuiharibu kazi ya kiufundi liyofumwa kwa juhudi na ustadi mkubwa.
Mwenyekiti wa TAMCO Bwana Ali Muhammed
Sherehe za Iddi za Waislamu wa Tanzania katika Mji huo Mkuu wa Marekani, ni utamaduni ulioanza tangu mwaka 1998, ambapo Waislamu waliona haja ya kuwa na mjumuiko wa pamoja katika Siku Kuu, ikizingitwa kuwa Marekani si nchi ya Kiislamu na kwa hivyo hakuna sherehe rasmi za Iddi, kama alivyoelezea Mwenyekiti wa TAMCO Bwana Ali Muhammed:
"Wazee na vijana waliokuwepo hapa katika miaka hiyo waliona kuna haja ya kuanzisha Umoja ambao utawasaidia katika mambo yao ya Kidini, siyo tu kwenye sherehe za Iddi, bali pia katika maswala mengine ya sherehe na misiba. Na baada ya chombo hicho kuanzishwa ndipo ukaanza utaratibu wa kuandaa sherhe kama hizi za Iddi".

Saturday, June 24, 2017

ZAIDI YA VIJANA 400 WAPATA ELIMU YA UJASILISIAMALI KUTOKA KWA MBUNGE RITTA KABATI

 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akitoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana zaidi ya 400 wa kanisa la kikatoriki parokia ya Ismani Mkoani Iringa
 Baadhi ya vijana walishiriki katika mafunzo ya kupewa elimu ya ujasiliamali katika kanisa la parokia ya Ismani

Na Fredy Mgunda, Iringa

Zaidi ya vijana mia nne (400) wa kikatoriki kutoka katika parokia kumi zinaizunguka Manispaa ya Iringa wamepata elimu ya ujasiliamali kutoka kwa mbunge wa viti maalum Mkoani kupitia chama cha mapinduzi (CCM).

Mafunzo hayo yametolewa katika Kanisa la kikatoriki parokia ya Ismani linaloongozwa paroko Leonard Maliva.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo mbunge wa viti maalumu Ritta Kabati alisema kuwa ujasiliamalia ni kitendo mtu yeyeto yule kutumia fursa ipasavyo pamoja na kuwa na nidhamu ya kuzitumia vizuri fursa unazipata.

"Leo hii tupo hapa Ismani kuna changamoto nyingi sana ambazo hazijapatiwa ufumbuzi hivyo inatakiwa kuzibarisha changamoto hizo kuwa mtaji wako kwa kubuni kitu ambacho kitakuletea faida hapo ndio utaanza kuitwa mjasiliamali"alisema Kabati

Kabati aliwataka vijana kuacha kutumiwa na wanasiasa kwa sababu wanasiasa wengi wapo kwa ajili ya maslai yao na sio kumtetea kijana hivyo vijana wanapaswa kutumia akili sana anapofanya kazi na wanasiasa.

"Ukitawa utafuna bigijii mwanzoni huwa inakuwa na utamu ila mwishoni utamu unaisha ndio hata sisi wanasiasa ndio tunavyowatumia vijana kwa maslai yetu" alisema Kabati

Aidha Kabati aliwaambia washiriki wa elimu hiyo ya ujasiliamali kukubali hasara wanapoanza ujasiliamali wao kwa kuwa vitu vingi vianakuwa vigeni kwao hivyo lazima uwe mvumilivu katika hali ngumu na hali ya faida.

Kabati aliwataka vijana kuacha kutumia vibaya pesa wanazipata kwenye biashara kwa kuwa ukifanya hiyo utakuwa unapunguza mtaji na hatimaye wanajikuta wamefilisika .

"Leo umepata faida kubwa lakini faida yote unaipeleka kula starehe ambayo haina faida kwa na kujikuta kila siku unataka kushindana na matajili wenye uwezo wako hivyo pesa inataka nidhamu ya hali juu kwa sababu hata nyie ni mashaidi huko majumabini kwenu kuna watu walikuwa na matajili lakini wamefilisika kutokana kutumia pesa bila nidhamu "alisema Kabati

Salvatory Komba,Lameck Lugala,Bariki Matonya,Francisco Mhehe na Odeth Kikoti ni baadhi ya washiriki waliohudhuria elimu hiyo ya mjasiliamali na kuwapongeza viongozi kuwa kuwakutanisha vijana na kuwapa elimu yenye faida kubwa kwenye maisha.

"Leo hii tumenufaika na elimu hii kutoka kwa mbunge na viongozi wengine ambao wametufundisha vitu vingi tuwaombe vijana wenzetu kufanya kazi kwa kujituma na kuitumia katika kujiletea maendeleo binafsi na ya nchi" walisema baadhi ya washiriki

Washiriki hao wasilisema kuwa ukifuatilia kwa makini mafunzo ya ujasiliamali yanafaida kubwa kwenye maisha yetu.

Kwa upande wake paroko Leonard Maliva wa parokia ya Ismani alimushukuru mbunge huyo kwa elimu aliyoitoa na kuwaomba vijana kuieshimu na kuitumia vizuri kwa ajili ya kuongeza maarifa vichwani mwao.

Maliva alisema kuwa kila mwaka wamekuwa wakitoa elimu ya maisha kwa zaidi ya vijana elfu moja kwa lengo la kuisaidia serikali kupata vijana wenye elimu ya dunia pamoja na elimu ya dini hivyo ukiwa na vijana wanaojituma kufanya kazi huku wakiwa na nidhamu basi nchi itapata maendeleo kwa kazi.

Friday, June 23, 2017

AKINAMAMA WALIMA NYANYA KINYEREZI DAR WAJIFUNZA KILIMO CHA UYOGA

Mafunzo kwa vitendo. Akinamama wa Kinyerezi Green Voices wakiweka udongo kwenye mifuko kama maandalizi ya kilimo cha uyoga.

FANYA YAFUATAYO KUNOGESHA SIKUKUU YA EID-AL-FITR

Na Jumia Travel Tanzania

Ni siku chache zimebakia kabla ya waumini wa dini ya kiislamu nchini na duniani kote kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Zipo namna tofauti za kusherehekea sikukuu hii kulingana na sehemu watu walipo.

Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuifanya sikukuu hii kuwa ya tofauti na kipekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka.   
 
Fanya maandalizi pamoja na familia. Katika kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia sikukuu basi ni vema ukawashirikisha kwenye maandalizi yake. Kama baba au mama wa familia na una watoto au ndugu unaishi nao litakuwa ni jambo zuri kama mtafanya hata kikao kidogo na kujadili. Kwa mfano, shughuli zote zitakazofanyika kipindi cha sikukuu, chakula kitakachopikwa, vinywaji, zawadi, wapi kwa kusherehekea, wageni gani wa kuwaalika, kupamba nyumba nakadhalika. Hii itasaidia siku hiyo ikifika kila mtu anafurahia na sio kufanya mambo ambayo yatakufurahisha wewe tu kuwaacha baadhi ya wengine kunung’unika.

Sherehekea pamoja na familia na majirani. Mara nyingi sikukuu hupendeza pale zinaposherehekewa kwa pamoja na ndugu na jamaa. Haijalishi familia uliyonayo ina ukubwa gani, kujumuika kwa pamoja kunaleta furaha na muunganiko zaidi miongoni mwa watu. Pia, hata kama una familia ndogo ni vema ukawashirikisha majirani zako. Unaweza ukapika chakula cha kutosha na ukaamua kuwaalika au kuwagawia lengo ni kuifanya iwe na shamrashamra zaidi.
 
Sherekea pamoja na watu wenye mahitaji maalum. Sio kila mtu huwa anapata fursa au kuwa na uwezo wa kusherehekea sikukuu. Na kwa sababu sikukuu ya Eid al-Fitr husherehekewa kwa siku mbili mpaka tatu (kwa sehemu zingine), unaweza ukapanga kwamba sikukuu ya moja au mbili ukasherehekea na familia yako na nyingine ukajumuika pamoja na watu wenye mahitaji maalumu kama vile watoto wa mitaani, watoto wa mitaani, wagonjwa mahospitalini, wazee, wafungwa na wengineo.

Wasimulie watoto kuhusu maisha ya Mtume na namna waislamu wa wakati walivyokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eid-al-Fitr. Sio siku zote watoto wakishamaliza kupata chakula cha pamoja na familia wakaenda kutembea. Unaweza kuitumia siku hiyo kwa muda mchache tu ukawakusanya watoto na kuwasomea hadithi za Mtume Mohammad na namna waislamu wa kipindi hiko walikuwa wanasherehekea vipi sikukuu hii.  Hii itawafanya si tu kufurahia kwa kuwaongezea maarifa lakini pia kuelewa ni nini maana zaidi ya siku hii.
 
Safiri pamoja na familia. Unaweza ukaamua kusherehekea sikukuu hii kwa kusafiri mahali tofauti na nyumbani. Mnaweza kutumia gari binafsi kama usafiri, mkawa mnapumzika kwenye vituo kadhaa kwa ajili ya chakula na kuswali mpaka mkafika mahali muendapo.

Toa zawadi kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kipindi cha Ramadhan mbali tu na kuwa ni kipindi cha kufanya toba na kumuomba Mwenyezi Mungu kukupunguzia dhambi zako lakini pia kutoa zawadi kunaweza kuwa ni njia mojawapo ya kukuongezea thawabu. Kutoa zawadi ni jambo jema kumfanyia mtu hususani unapolifanya kwa moyo mkunjufu. Basi kama utakuwa na uwezo unaweza kununua zawadi kadhaa na kuwapatia ndugu na majirani zako.

Badili muonekano wa nyumba yako. Itapendeza kama siku ya sikukuu mtaisherehekea kwenye nyumba yenye muonekano tofauti. Unaweza kufanya hivi kwa kushirikiana na familia yako ili kupata mwonekano utakaovutia. Mambo yanayoweza kubadili mwonekano wa zamani ni kama vile kupaka rangi mpya, kubadili samani za ndani, kununua mapambo, kufanya usafi au hata mpangilio wa vitu ndani ya nyumba.

Valia mavazi nadhifu. Tumezoea kwamba linapokuja suala la kuvaa nguo mpya siku za sikukuu huwa ni watoto pekee wanaopenda kufanya hivyo. Kwenye familia nyingi imekuwa ni kawaida wazazi kuweka kipaumbele kwa kuwanunulia watoto nguo mpya. Kutokana na desturi hiyo kuzoeleka miongoni mwa watu wengi, imewafanya watu wazima kupuuzia kuvaa nguo mpya kipindi cha sikukuu. Hiyo ni dhana na mawazo ya watu tu na wala isikufanye ujisikie vibaya kuvaa nguo mpya siku ya sikukuu. Unastahili kuutendea vema mwili wako kwa kuuvika na mavazi mapya na nadhifu siku hiyo, kama una uwezo lakini.   

Dhumuni la kukupatia dondoo hizi ni kuifanya sikukuu hiyo iwe na upekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka. Jaribu kufanya baadhi ya mambo hayo na utagundua utofauti mkubwa. Sio lazima ufanye yote yaliyoorodheshwa kwenye makala haya, machache tu yanatosha. Tofauti na hapo, Jumia Travel ingependa kukutakia maandalizi na mapumziko mema ya sikukuu ya Eid al-Fitr!

SBL YAZINDUA MRADI WA MAJI KWA WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani wakati wa uzinduzi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68  uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Hawa Ladha. 

Thursday, June 22, 2017

ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILLE WA KKKT DAYOSISI YA IRINGA KUANZA KAZI RASMI TAREHE 25 / 6 / 2017

Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Nayman chavala akizungumza na wanahabari

Na Fredy Mgunda, Iringa

KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John pombe Magufuli kwa utendaji kazi.

Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo

wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya kuwekwa wasifu kwa askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga.

Alisema kuwa sherehe za kumpa madaraka ya kuanza kufanya kazi kama askofu wa kanisa la KKT Jimbo la Iringa mchungaji Gavile na msaidizi wake Saga itafanyika jumapili ya june 25 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Gangilonga .

Kuwa ibada hiyo itaongozwa na askofu mkuu wa KKKT Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na kuwa kabla ya idaba kutakuwa na maandamano ya wachungaji na washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi Gangilonga.
" Tunaomba wananchi wote na washarika kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria pia tunategemea kuwa na viongozi mbali mbali wa serikali na wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Tanzania"

Chavala alisema maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya tukio hilo kubwa ambalo lilikuwa likisubiliwa kwa shauku kubwa .

Askofu Gavile amechukua nafasi ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Dkt Mdegella ambaye alistaafu kwa heshima kubwa na kuacha heshima ya aina yake ndani ya KKKT .

Wakati huo huo Katibu huyo amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuwatumikia watanzania kwa uadilifu mkubwa na kuwa kazi kubwa kwa watanzania ni kuendelea kumpa ushirikiano .

Kwani alisema kuwa hatua ya kuwabana wasio waadilifu pamoja na kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu (MAKINIKIA) ni hatua ya kupongezwa kwani suala hilo lilikuwa likiwanufaisha wachache huku Taifa likibaki patupu .

" Sisi kama kanisa tumekuwa tukimuombea kila wakati tena kwa kumtaja kwa jina na hatutachoka kuendelea kumuombea maana kazi anayoifanya ni ngumu ambayo silaha kubwa ni maombi "

Tuesday, June 20, 2017

UNESCO YATOA TAHADHARI ONGEZEKO LA JANGWA

Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu. Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo - hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa. Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya 'wakimbizi wa mazingira' sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. Na hili hii inategemewa kundelea kuongezeka. Kufikia 2030, Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa imeonya kuwa, kufikia mwaka 2030 watu wapatao milioni 135 wako katika hatari ya kuhama makazi yao kwa sababu ya kuenea kwa jangwa, na watu milioni 60 wanatarajiwa kuhama kutoka Kusini mwa jangwa la Sahara kuelekea Afrika ya Kaskazini na Ulaya. Utabiri huu unaonyesha kuwa sehemu zilizo kame na zile zilizo kame zaidi huathirika zaidi na kuenea kwa jangwa na kuhama kwa watu. Watu wanaokaa vijijini amabao hutegemea ufugaji wa wanyama, kilimo na maliasili watakuwa katika hatari zaidi ya kuwa wahanga wa athari hizo, ambazo hujumuisha umaskini, kudorora kwa elimu, ukosefu wa uwekezaji, umbali kutoka huduma muhimu, na kutengwa. Ni lazima tukabiliane na hali hii na hii inamaanisha kufanya kazi katika ngazi mbili: Kwanza, ni lazima tusimamie ardhi kwa usahihi,hii ni muhimu katika kuzuia kuenea kwa jangwa na katika kulinda kiwango chake cha uzalishaji. Hifadhi ya Bayongahewa ya Las Bardenas Reales ya UNESCO iliyoko nchini Hispania inaonyesha kwamba usimamizi wa ardhi kame unaotumia taarifa sahihi, kwa kuzingatia kupishana kati ya matumizi ya malisho, ukulima na vipindi ya bila ya kuilima ardhi hupelekea si tu kusitisha kuwepo hali ya kuenea kwa jangwa lakini pia huleta uwezekano wa kurejesha ardhi kama ilivyokua awali. Hii ndio sababu Programu ya Kimataifa ya UNESCO ya Nishati-Maji imejikita katika kujenga uwezo na kutoa mwongozo wa sera na zana za kushughulikia ukame, kuenea kw jangwa na changamoto zinazotikana na hayo, hasa kuhusiana na usimamizi wa rasilimali maji, kwa njia ya Mtandao wa Kimataifa unaohusika na Maji na Maendeleo ya Taarifa ya Ardhi Kame (G- WADI). Pili, inatupasa kuimarisha ustahimilivu wa watu walio katika mazingira hatarishi kwa kuwawezesha kuwa na njia mbadala za kujipatia kipato ili tuweze kuuharibu mduara wa kuenea kwa jangwa na madhara yake ya kijamii na kiuchumi ambayo mara nyingi husababisha watu kuyahama makazi yao. Katika kutafuta na kuendeleza elimu na kujenga uwezo katika sayansi, teknolojia na uhandisi, kwa wasichana na wavulana katika nchi zilizo katika hatari zaidi, Programu ya Sayansi ya Msingi ya Kimataifa ya UNESCO inafanya kazi ya kujenga fursa mpya za ajira kwa vijana, kupunguza utegemezi wa rasilimali zinazotegema hali ya hewa, ili kuwapatia watu maisha yenye ustahimivu katika makazi yao. Katika siku hii, ni lazima tutambue kuwa hali ya kuenea kwa jangwa ni jambo la kimataifa ambalo linalomtishia kila mtu na ni lazima lishughulikiwe kwa pamoja ili kujenga mustakabali endelevu na imara kwa wote. Ujumbe kutoka kwa Bi. Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Kuenea kwa Jangwa na Ukame Duniani, 17 Juni 2017

"NEXT EINSTEIN" YAZINDUA WIKI YA SAYANSI AFRIKA TANZANIA

Mtaalamu wa masomo ya Sayansi, Fadhil Leonard akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi namna ya kutengeneza gari linalojiendesha bila ya kuwa na dereva wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sayansi Afrika Tanzania iliyofanyika  katika viwanja vya Shule ya Al-Murtaza Upanga jijini Dar es Salaam leo. 

VIDEO: BUNGE LA WATOTO LAVUTIA WENGI MKOANI MWANZA

Jana juni 16,2017 mataifa mbalimbali barani Afrika yaliungana pamoja kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkoani Mwanza, maadhimisho hayo yalifanyika uwanja wa Furahisha kwa kujumuisha matukio mbalimbali ya watoto. Wengi walivutiwa na kipengere cha bunge la Watoto mkoani Mwanza kwenye maadhimisho hayo yaliyokuwa na kaulimbiu ya "Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto.
Tazama video

ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM


Na Jumia Travel Tanzania

Umaarufu wa Dar es Salaam kwenye shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza.
 
Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi eneo la Oyster Bay, Jumia Travel ingependa kukufahamisha kwamba unaweza kujifunza na kufurahia mambo mengi pindi utakapotembelea maeneo yafuatayo.

Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni. Makumbusho haya awali yalifunguliwa mwaka 1940 kama kumbukumbu ya Mfalme George wa tano ambapo kihistoria huwarudisha watanzania nyuma walipotokea. Makumbusho haya huonyesha mabaki muhimu ya binadamu wa kale yaliyogunduliwa na Dkt. Leakey aliyoyachimbua kwenye bonde la Olduvai. Wageni wanaweza kujifunza urithi wa kitamaduni kutoka kwa makabila mbalimbali Tanzania pamoja na athari za biashara ya utumwa kipindi cha utawala wa kikoloni. Baadhi ya vitu vingine vinavyopatikana katika makumbusho haya yaliyopo mtaa wa Shaaban Roberts ni zana za jadi, desturi, mapambo na vyombo vya muziki.  
 
Kijiji cha Makumbusho. Takribani maili 6 kutokea katikati ya jiji, kuna kiji cha makumbusho ambacho kimehifadhi tamaduni za makabila zaidi ya 120 yanayopatikana Tanzania. Wageni wanaweza kuzunguka kwenye vibanda kadhaa vya nyasi vinavyopatikana pale kwenye ukbwa wa takribani hekari 15 na kujionea ufundi wa kijadi katika kuchora, ufumaji na uchongaji. Kijiji hiki kinachopatikana eneo la Kijitonyama, barabara ya Bagamoyo pia huwa na ngoma na michezo ya jadi pamoja shughuli nyingize za kitamaduni.

Sanamu la Askari. Likiwa limetengenezwa kwa shaba sanamu hili ya Askari huonyesha askari akiwa amevalia vazi rasmi lililotumika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia huku ncha ya mbele ya bunduki (kama kisu) ikiwa imeelekezwa karibu na bandari iliyopo jirani. Sanamu hili huonyesha kama kumbukumbu ya majeshi ya waafrika walioshiriki kupigana kwenye vita ya Kwanza ya Dunia na linapatikana mtaa wa Azikiwe na Samora.
 
Boma la Kale. Likiwa limejengwa mnamo mwaka 1866 mpaka 1867 na Majid Bin Said, Sultani wa Zanzibar, Boma hili la kale ni jengo lenye umri zaidi ambalo linapatikana kwa sasa jijini Dar es Salaam. Jengo hili lilitumika kuwakarabisha wageni wa Sultani ambaye alikuwa na kasri lake pembeni yake. Vitu vya kuvutia kwenye jengo hili lililopo mtaa wa barabara ya Sokoine ni namna lilivyojengwa kwa ndani vikiwemo mlango wa mbao kutokea Zanzibar na kuta zilizojengwa kutokana na matumbawe.

Kanisa la Mtakatifu Joseph. Jengo hili la Kanisa la Kiroma lilijengwa na wamisionari wa Kijerumani mnamo mwaka 1897 mpaka 1902, kwa kiasi kikubwa ni kivutio kinachoweza kuonekana eneo la karibu na bandarini. Jengo hili kwa ndani limejengwa kwa ufundi na ubunifu wa hali ya juu na kutumia stadi halisi kabiza za kijerumani. Jengo hili ndio Makao Makuu ya kanisa hilo na liinapatikana katika barabara ya Sokoine.   

Kanisa la KKKT Azania Front. Wajerumani walilijenga kanisa la KKKT Azania Front mnamo mwaka 1898. Namna jengo hili lilivyojengwa hususani paa lake kunalifanya kuwa ni nembo ya kivutio jijini Dar es Salaam. Kuna kipindi kanisa hili ndilo lilikuwa kituo kikuu cha shughuli za kimisionari mnamo karne ya 19, kwa sasa ndio makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Ikulu. Ikiwa imejengwa kwenye miaka ya 1890, jengo la Ikulu ndilo lilikuwa ni makazi ya mwanzo kabisa ya Gavana wa Ujerumani. Mnamo mwaka 1922, Waingereza walifanya maboresho ya jengo hilo maeneo mbalimbali kufuatia kuliharibu katika kipindi cha vita ya Kwanza ya Dunia. Ingawa raia wa kawaida hawawezi kuingia ndani lakini bado linabaki kuwa kivutio kikubwa mtu akipita karibu nalo. Jengo hili linapatikana mtaa wa Luthuli barabara ya kuelekea Kivukoni.   
 
Kisiwa cha Mbudya. Kisiwa hiki kinapatikana umbali wa dakika kumi kwa mwendo wa boti kutokea Kunduchi kikiwa ni hifadhi ya majinii jijini Dar es Salaam. Ukiwa kisiwani hapa utasahau kabisa pilikapilika za katikati mwa jiji hili kwa kufurahia fukwe safi, michezo ya kwenye maji na kuogelea. Kisiwani haoa kuna vibanda vya kukodisha karibu na ufukwe huku vyakula vya baharini pamoja vinywaji vikipatikana pia. Sehemu hii ni maarufu sana kwa watu wanaopenda kutalii kwa siku moja wakitokea katikati ya jiji.

Kisiwa cha Bongoyo. Takribani maili 4 Kaskazini mwa jiji la Dar es Salaam eneo la Msasani kinapatikana kisiwa cha Bongoyo. Kwa wale wanaopenda kusafiri kwa siku moja na kurudi hii sehemu pekee na ya kuvutia ambayo unaweza kufurahia mambo mengi. Kisiwa kina fukwe safi, michezo ya kwenye maji, pamoja na kujionea aina kadhaa za samaki wa baharini. Nyuma ya kisiwa hiki kuna mibuyu mikubwa ambayo huleta hewa safi kwenye fukwe za kisiwa hiko huku vyakula vya baharini na vinywaji hupatikana kwa ajili ya wanaotembelea. Bongoyo kwa sasa inawezekana kuwa ni miongoni mwa visiwa vinne vinavyotembelewa zaidi kwenye hifadhi za maji jijini Dar es Salaam.
 
Dar es Salaam ina mambo mengi ya kujifunza ingawa mengi yamezingwa na shughuli za kibiashara zilizotapakaa kila kona. Jumia Travel inaamini kuwa inawezekana unaishi na vivutio vya kitalii karibu nawe lakini ulikuwa haufahamu. Hivyo basi kabla ya kufikiria kwenda mbali kutalii vivutio vingine anza na vilivyomo jijini hapa kwani vipo karibu nawe na haikugharimu sana kuvitembelea.

Friday, June 16, 2017

Save the Children yaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Dar

Shirika la Save the Children nchini limeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kukutana na Watoto mbalimbali wa shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo Walimu na Maafisa wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii walishiriki na kuchangia mijadala iliyoibuliwa na watoto wenyewe kuhusu malengo ya usawa na haki ya jinsia ifukapo mwaka 2030.
 Katika tukio hilo baadhi ya shughuli walizofanya watoto ni pamoja na kuibua mijadala ya Haki na Wajibu wa Mtoto, Unyanyasaji na changamoto za kurepoti kesi za unyanyasaji. Watoto walipata majibu jinsi ya kuripoti kesi za ukatili na unyanyasaji katika kituo cha dawati la jinsia kwenye kituo cha Polisi karibu nao. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Halili Katani wakati wa kufungua mjadala wa Siku ya Mtoto wa Afrika, alieleza kuwa, Watoto wana haki na wajibu wa kusaidiwa pamoja na kulindwa kama wajibu wa Serikali na Jamii yote. Alitoa wito na rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa, haki za watoto zinatimizwa na kulindwa na kuwafikia watoto zikiwemo za elimu, ulinzi na malezi bora. Aidha, aliwataka watoto hao wakawe mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa wenzao kwa kuwapa elimu waliopata katika siku ya Mtoto wa Afrika. Bi Halili aliwataka watoto Manispaa ya Kinondoni na maeneo mengine kuhakikisha wanaripoti matendo ya kikatili pindi watakapofanyiwa huko mitaani ama na walezi wao kwa kutoa taarifa kwa watu wanaowaamini ikiwemo Walimu, Maafisa wa Ustawi wa jamii na madawati ya Jinsia katika ngazi mbalimbali ikiwemo kwenye Kata, Vituo vya Polisi na sehemu zingine. Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Haki kwa vijana na watoto, Bi. Ellen Otaru amesema kuwa, watoto wenyewe wamebaini kutokuwa na usawa katika malezi yao huku wakilalamika kuwa wamekosa upendo kutoka kwa wazazi / walezi kutokana na aina ya maisha ya baadhi ya familia. “Shughuli hii ni maalum kwa watoto wa Manispaa ya Kinondoni ambapo watoto wenyewe pamoja na walimu wao wameweza kuelezea hali halisi wanayopambana nayo huko majumbani na mashuleni hivyo changamoto hizo zimepokelewa na walimu wenyewe pamoja na maafisa Maendeleo ya Jamii hatua zaidi ya utekelezaji zimewekwa bayana hapa.” Alieleza Bi. Ellen. Aidha, amewasihi wazazi kuwa na desturi ya kufuatilia watoto wao hasa mienendo ya maisha na makuzi yao kwani watoto wamekuwa na maisha mabaya katika makuzi yao. Shughuli zingine kwenye tukio hilo ni pamoja na watoto hao kuonyesha igizo maalum, mijadala ya wazi ya wao kwa wao pamoja na kuamsha mijadala ya kujifunza kutoka kwa maafisa wengine waliokwemo . Kwa mwaka huu Siku ya Mtoto wa Afrika Kitaifa inatarajia kufanyika hapo kesho Juni 16.2017, Mkoani Dodoma huku ikiwa na kauli mbiu “Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto”. Katika maadhimisho hayo, Jumla ya shule 10 za Manispaa hiyo ya Kinondoni ziliweza kushiriki huku baadhi ya shule hizo ni pamoja na : Mbezi Ndumbwi, Salasala, Mikocheni A, Ushindi, Mikocheni B Sekondari, Nakasangwe, Changanyikeni, Makongo Juu na nyinginezo. Mwisho. CODES: Save the Children yaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika Dar Shirika la Save the Children nchini limeadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa kukutana na Watoto mbalimbali wa shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo Walimu na Maafisa wa Ustawi na Maendeleo ya Jamii walishiriki na kuchangia mijadala iliyoibuliwa na watoto wenyewe kuhusu malengo ya usawa na haki ya jinsia ifukapo mwaka 2030. Katika tukio hilo baadhi ya shughuli walizofanya watoto ni pamoja na kuibua mijadala ya Haki na Wajibu wa Mtoto, Unyanyasaji na changamoto za kurepoti kesi za unyanyasaji. Watoto walipata majibu jinsi ya kuripoti kesi za ukatili na unyanyasaji katika kituo cha dawati la jinsia kwenye kituo cha Polisi karibu nao. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Halili Katani wakati wa kufungua mjadala wa Siku ya Mtoto wa Afrika, alieleza kuwa, Watoto wana haki na wajibu wa kusaidiwa pamoja na kulindwa kama wajibu wa Serikali na Jamii yote. Alitoa wito na rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha kuwa, haki za watoto zinatimizwa na kulindwa na kuwafikia watoto zikiwemo za elimu, ulinzi na malezi bora. Aidha, aliwataka watoto hao wakawe mabalozi wazuri wa kutoa elimu kwa wenzao kwa kuwapa elimu waliopata katika siku ya Mtoto wa Afrika. Bi Halili aliwataka watoto Manispaa ya Kinondoni na maeneo mengine kuhakikisha wanaripoti matendo ya kikatili pindi watakapofanyiwa huko mitaani ama na walezi wao kwa kutoa taarifa kwa watu wanaowaamini ikiwemo Walimu, Maafisa wa Ustawi wa jamii na madawati ya Jinsia katika ngazi mbalimbali ikiwemo kwenye Kata, Vituo vya Polisi na sehemu zingine. Naye Meneja wa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Haki kwa vijana na watoto, Bi. Ellen Otaru amesema kuwa, watoto wenyewe wamebaini kutokuwa na usawa katika malezi yao huku wakilalamika kuwa wamekosa upendo kutoka kwa wazazi / walezi kutokana na aina ya maisha ya baadhi ya familia. “Shughuli hii ni maalum kwa watoto wa Manispaa ya Kinondoni ambapo watoto wenyewe pamoja na walimu wao wameweza kuelezea hali halisi wanayopambana nayo huko majumbani na mashuleni hivyo changamoto hizo zimepokelewa na walimu wenyewe pamoja na maafisa Maendeleo ya Jamii hatua zaidi ya utekelezaji zimewekwa bayana hapa.” Alieleza Bi. Ellen. Aidha, amewasihi wazazi kuwa na desturi ya kufuatilia watoto wao hasa mienendo ya maisha na makuzi yao kwani watoto wamekuwa na maisha mabaya katika makuzi yao. Shughuli zingine kwenye tukio hilo ni pamoja na watoto hao kuonyesha igizo maalum, mijadala ya wazi ya wao kwa wao pamoja na kuamsha mijadala ya kujifunza kutoka kwa maafisa wengine waliokwemo . Kwa mwaka huu Siku ya Mtoto wa Afrika Kitaifa inatarajia kufanyika hapo kesho Juni 16.2017, Mkoani Dodoma huku ikiwa na kauli mbiu “Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto”. Katika maadhimisho hayo, Jumla ya shule 10 za Manispaa hiyo ya Kinondoni ziliweza kushiriki huku baadhi ya shule hizo ni pamoja na : Mbezi Ndumbwi, Salasala, Mikocheni A, Ushindi, Mikocheni B Sekondari, Nakasangwe, Changanyikeni, Makongo Juu na nyinginezo. Tazama hapa tukio hilo:
Meneja wa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Haki kwa vijana na watoto, Bi. Ellen Otaru akitoa elimu katika tukio hilo la siku ya Mtoto wa Afrika 2017, ambapo maadhimisho hayo yamefanyika mapema leo Juni 15, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mratibu wa Ulinzi kwa Watoto wa Save The Children, Bi. Haika Harrison.
Baadhi ya watoto waliokuwa kwenye shughuli hiyo ya siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Manispaa ya Kinondoni leo Juni 15.2017.
Mratibu wa Ulinzi kwa Watoto wa Save The Children, Bi. Haika Harrison akiwaimbisha watoto nyimbo mbalimbali
Watoto hao wakitoa burudani
Afisa wa Save the Children kutoka Sweden- Award Manager, SCS, Bwana. Olle Kvist akizungumza na watoto hao wakati wa tukio hilo
Afisa wa Save the Children kutoka Sweden- Award Manager, SCS, Bwana. Olle Kvist akizungumza na watoto hao wakati wa tukio hilo
Afisa mipango wa Save the Children, Mzee John Komba 'JK' Kijana akizungumza jambo katika tukio hilo
Baadhi ya walimu wakifuatilia tukio hilo
Baadhi ya watoto wakitoa maelezo namna ya michoro yao katika mradi maalum wa watoto katika baadhi ya shule unaoendeshwa na Save the Children
Meneja wa miradi ya Watoto wa Save the Children, Bwana. Anthony Binamungu akiwatambulisha meza kuu wakati wa ufunguzi rasmi wa tukio hilo
Meza kuu
Afisa wa Save the Children kutoka Sweden- Award Manager, SCS, Bwana. Olle Kvist akizungumza na watoto hao wakati wa tukio hilo
Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Halili Katani ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, akizungumza katika tukio hilo
Mkaguzi wa ubora wa miradi wa Save the Children, Bi. Amy Scchmidity akizungumza katika tukio hilo
Bi. Agnes Mbussa afisa ustawi wa Jamii akizungumza katika tukio
Afisa wa maendeleo ya jamii Bi. Editha Mbowe akizungumza katika tukio hilo
mijadala ikiendelea
Baadhi ya walimu wakichangia mada katika tukio hilo
Baadhi ya walimu wakiwa katika majadiliano
matukio yakiendelea
Baadhi ya shule ziliweza kupata zawadi kwa uwasilishaji bora wa mada zao
Zawadi zikitolewa kwa shule zilizoweza kuwasilisha mada bora
Watoto walipata kusali ili kuweza kuendesha mambo yao katika suala la imani
Watoto walipata fursa ya chakula safi katika shughuli hiyo
Meneja wa Mradi wa Elimu ya Afya ya Uzazi na Haki kwa vijana na watoto, Bi. Ellen Otaru akiendesha mijadala na watoto hao katika tukio hilo la siku ya Mtoto wa Afrika 2017, ambapo maadhimisho hayo yameweza kuzikutanisha shule 10 za Manispaa ya Kinondoni.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More