Thursday, June 30, 2016

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.

MKOA WA IRINGA WAKAMILISHA MADAWATI YA MAGUFULI

 SERIKALI    ya    mkoa wa  Iringa  imetekeleza  agizo la  Rais  Dr  John Magufuli  kwa kukabidhi  jumla ya madawati 21,304 kwa   shule  za  msingi na   sekondari katika Halmashauri  zote  tano  za  mkoa   huo .

Wednesday, June 29, 2016

UKAWA Watishia Kumpeleka Rais Magufuli Katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)


Wabunge wa Ukawa wamemtaka Rais John Magufuli kutoa tamko juu ya uvunjifu wa haki za binadamu Zanzibar na kwamba wana mpango wa kumpeleka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakidai yanayotokea visiwani humo yana baraka zake. 

Wabunge Wataka CUF Ifutiwe Usajili

MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Munira Mustafa Khatib, ameitaka serikali kukifutia usajili Chama cha Wananchi (CUF), kwa madai kuwa kimekuwa kikishiriki katika matukio ya kupigwa na kuharibu mali za wananchi visiwani Pemba.

Sheria ya Manunuzi Yaanza Kung’ata....Posho Zafyekwa, Vikao Vyapunguza Kutoka 12 Hadi 4

MAREKEBISHO ya Sheria mpya ya Manunuzi, yamewasilishwa bungeni yakitamka kufyeka posho za watendaji, wanaosimamia mchakato wa zabuni na kuondoa vikao vya bodi kutoka 12 kwa mwaka hadi vinne, ikisisitiza kuziba mianya ya rushwa na kuongeza uwazi.

Gesi ya Helium ya Futi za ujazo B ilioni 54 Yagundulika Tanzania

GESI ya helium ya takribani futi za ujazo bilioni 54 inayoelezwa kuwa adimu duniani, imegundulika nchini Tanzania na kuiweka nchi kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye madini mengi na muhimu.

CCM Yawalima Barua Wabunge Wake.

Kamati Kuu ya CCM imeagiza Kamati ya Wabunge wa chama hicho kuwapa barua za kujieleza wabunge wao wasiohudhuria, wanaochelewa na wanaondoka kabla ya vikao vya Bunge kuahirishwa. 

Kujitoa EU: Uingereza Yawatoa hofu Watanzania

Siku chache baada ya Uingereza kuamua kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), Balozi wa nchi hiyo nchini amesema wataendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania ili kuhakikisha uwekezaji haupungui.

Taarifa ya Lugumi Yapigwa Kalenda Tena Bungeni

Ripoti ya sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi Enteprises na Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa Bunge, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.

SABABU ZA KUNDI LA MUZIKI LA PAYUS & MECRAS KUTOKA JIJINI MWANZA KUBADILI JINA.

Wakali wa wimbo wa Chausiku, Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza, ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Muziki la Payus & Pacras, wamebadili jina la kundi lao na sasa wanaitwa WAPANCRAS.

RC MAKONDA ATEMBELEA BANDA LA UN KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Makonda alifika katika banda hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa UN kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa nchini.

Tuesday, June 28, 2016

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Aandaa Ibada ya Shukrani

BUNGE limepitisha kwa kauli moja Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba 2 ya mwaka 2016 ambayo pamoja na mambo mengine, imeongeza adhabu kwa watu wanaowapa mimba au kuoa ama kuolewa na mwanafunzi, sasa watafungwa jela miaka 30.

Hukumu kesi ya Mauaji ya Mwangosi Inayomkabili Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Itatolewa Julai 21

Hukumu ya kesi ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10, Daudi Mwangosi itatolewa Julai 21 baada ya Mahakama Kuu kusikiliza majumuisho na maoni ya Baraza la Wazee. Kesi hiyo inamkabili askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Iringa, Prisifius Simon.

KITUO CHA HUDUMA NA MTOTO EAGT LUMALA MPYA CHA JIJINI MWANZA CHAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO WENYE UHITAJI.

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG

Monday, June 27, 2016

Afariki Dunia Baada ya Kunywa GONGO Kupita Kiasi


MKAZI wa Mondo katika Kijiji cha Kitumba wilayani Magu, Wilson Magola (45), amekufa baada ya kunywa pombe haramu ya gongo.

CHADEMA Watafakari Hatua za Kuchukua Baada ya Rais Magufuli Kutaka Siasa Zifanywe 2020

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani kimesema kinatafakari hatua gani ya kuchukua baada ya Rais John Magufuli kutaka siasa za nguvu zifanywe wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao, kauli inayotafsiriwa kuwa ni kupiga marufuku shughuli za kisiasa. 

Dk. Mbassa wa Chadema afariki dunia akiwa usingizini

ALIYEKUWA Mbunge wa   Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Anthony Mbassa alifariki dunia jana usiku  akiwa usingizini nyumbani kwake.

Waziri Mkuu alia na mauaji dhidi ya raia

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amekemea matukio ya mauji yanayoendelea nchini na kusema kuwa hakuna dini inayofundisha vitendo hivyo viovu.

Aliyeondolewa Ukuu wa wilaya Lushoto ajitetea,adai hakubebwa.

Siku moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutangaza upya nafasi za wakuu wapya wa wilaya nchini, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Lushoto mwenye umri mdogo kuliko wenzake ambaye jina lake limeondolewa katika orodha hiyo Mariam Juma,amedai kuwa nafasi aliyokuwa ameipata sio kwamba alichaguliwa kwa upendeleo,na badala yake elimu ndio iliyosababisha kupata hadhi ya kumuwakilisha Rais wa awamu ya nne.

ZULMIRA ATAKA KAZI KWA PAMOJA KUHAMI MAENEO YA URITHI WA DUNIA

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na shirika lake kwa wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Friday, June 24, 2016

Risasi Zarindima Zanzibar Watu watatu Wajeruhiwa

Watu watatu wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kupelekwa hospitali ya Alrahma kwa matibabu.

Majeruhi hao ni Yussuf Ali Juma (23), Ali Shaame Ibrahim (18) na Salim Masoud Bakar (18), wakazi wa Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja.

Mtuhumiwa kesi ya Mwangosi akana Ungamo Lake Mahakamani

Mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoani hapa, Daudi Mwangosi, Pacificus Simoni ametoa ushahidi wake mbele ya mahakama na kuieleza kuwa alilazimishwa kusaini ungamo mbele ya mlinzi wa amani bila kujua nini kilichoandikwa.

DK. MENGI ACHANGIA MADAWATI 1,000, ATOA SOMO KWA WATU MATAJIRI

Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.

KAMPUNI YA TOMONI FARMS LIMITED YAFUNGUA DUKA NA MGAHAWA WA KISASA WA MAZAO YA KILIMO DAR

DSC_8003 


Mkurugenzi wa uendeshaji wa Kampuni ya Tomoni Farms Limited, Bwana Franklin Bagalla akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani wakati wa utambulisho wa tukio hilo mapema leo Juni 23.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Willybroad Alphonce.

Monday, June 20, 2016

MTUMISHI WA MUNGU MASANJA MKANDAMIZAJI ARINDIMA KATIKA MKUTANO WA OYES 2016 JIJINI MWANZA.

Mhubiri na Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji, akihudumu katika Mkutano Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 wenye lengo la kuwafungua watu wote kiroho na hivyo kuondokana na vifungo mbalimbali vinavyowakabiri, uliofanyika katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mkutano huo ulianza June 12,2016 na kufikia tamati jana June 19,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo. Wahubiri na waimbaji mbalimbali walihudumu katika mkutano huo akiwemo Mchungaji wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone ambae amewahi kufariki na kufufuka siku ya nne, Mwimbaji na Mhubiri Joseph Rwiza pamoja na Mwimbaji Chamwenyewe Jembe ambapo watu wengi walifunguliwa kiroho na kuokoka katika mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo

MKURUGENZI WA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA AKABIDHI MADAWATI KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akizungumza wakati wa kukabidhi madawati katika Manispaa hiyo.
Na BMG
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 2,600 kwa shule zote 74 za Msingi za umma zilizopo kwenye manispaa hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli la kutaka kila wilaya kumaliza tatizo la madawati ifikapo Juni 30 mwaka huu.

Kubenea Amshitaki Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson

Wakati Kamati ya Haki, Maadili na Madara ya Bunge imepokea mashtaka dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, mbunge mwingine wa upinzani ameamua kumshtaki kiongozi huyo kwenye Kamati ya Kanuni ya Bunge.

Nape Asema Lowassa ni Alama ya Ufisadi, ampa ushauri mgumu

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amenena tena kuhusu uamuzi wa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupewa nafasi ya kugombea urais.

Breaking News: Wabunge wa Upinzani Waziba Midomo yao Kwa Karatasi na Plasta na Kisha Kutoka Nje

Wabunge wa Vyama vya Upinzani vinavyounda Ukawa, leo wametoka tena Bungeni kama walivyoazimia kukacha vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, lakini wamekuwa na mtindo wa aina yake.

MIRADI 43 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH BILIONI 23 KUZINDULIA NA MWENGE MKOA IRINGA

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Bi Amina Masenza  (kushoto)  akikabidhiwa  mwenge  wa Uhuru  na  mkuu  wa  mkoa  wa  Njombe baada  kuwasili mkoa  wa  Iringa  ukitokea  mkoa  wa  Njombe zaidi ya  miradi 43  yenye  thamani  ya  zaidi  ya  Tsh bilioni 23 kuwekea mawe  ya  msingi na  kuzinduliwa

Friday, June 10, 2016

WATOTO WALIOZALIWA NA MAMBUKIZI YA VVU MATUMAINI DODOMA, WAITAKA JAMII KUWAKUMBUKA

Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiongozwa na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo katika manispaa ya Dodoma karibu na Hoteli ya Mtakatifu Gasper.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Thursday, June 9, 2016

KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER LATUPIWA VYOMBO NJE


Hili ni eneo la Kanisa Hilo

JANGILI WA MENO YA TEMBO ASHUGHULIKIWA KISAWASAWA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, imemhukumu, Johnface Lyang’oka, mkazi wa Magozi, Pawaga wilayani Iringa; kifungo cha miaka 15 jela au kulipa faini ya Sh Bilioni 1.65 baada ya kupatikana na makosa mawili yaliyomuhusisha na biashara ya meno ya Tembo 34.

Viongozi CHADEMA Akiwemo Freeman Mbowe wazuiwa kuingia ofisini Shinyanga

Viongozi na makada wa Chadema waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea jijini Mwanza jana wamejikuta wakishindwa kuingia kwenye ofisi za chama hicho mjini Shinyanga kutia saini kitabu cha wageni baada ya Jeshi la Polisi kuzuia shughuli yoyote ya chama hicho mjini humo.

Wasiotumia EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali

KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.

Mwanza, Kagera, Kigoma Zaongoza kwa Umasikini wa Kipato


PAMOJA na maendeleo yaliyotokana na kukua kwa pato la wastani la Mtanzania na kupungua kwa umasikini wa mahitaji ya msingi, serikali imeainisha mikoa mitano iliyokithiri kwa umasikini wa kipato.

Mchanganuo Mzima wa Bajeti ya Serikali 2016/ 2017 Iliyosomwa Jana Bungeni.

SERIKALI imewasilisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ya Sh trilioni 29.53, ambayo nguvu kubwa imewekwa katika kukusanya mapato kwa kulinda viwanda vya ndani na kubana matumizi ya serikali ili kuelekeza sehemu kubwa ya matumizi katika maeneo ya vipaumbele.

Wednesday, June 8, 2016

MSASA WA SDGS WAENDELEA UDOM, VITIVO VYAKAMILIKA


Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiendesha mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi wa vitivo mbalimbali na walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyomalizika jana chuoni hapo.(Picha na Modewjiblog)

Serikali kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.

Zitto Kabwe Aitwa Polisi Kwa Mahojiano

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016  aliitwa Polisi  na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  ACP Camilius Wambura.

Waziri Mkuu: Sukari Haitakuwa Tatizo Ramadhani

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja isizidi Sh 2,300. 

Bajeti ya Magufuli 2016/17 Hadharani Leo....Macho na Masikio Yote Yaelekezwa Dodoma

TANZANIA kama zilivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki, leo inawasilisha bungeni mjini Dodoma Bajeti ya Serikali ili Bunge liijadili na kuipitisha, ianze kutekelezwa katika mwaka mpya wa fedha 2016/17 unaoanza Julai mosi.

Wapinzani Walegeza Waahidi Kuwasilisha Vipande Muhimu vya Hotuba Kivuli ya Bajeti

Wakati hatua ya upinzani kumsusia Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ikiingia siku ya nane, Kambi ya upinzani imesema leo itawasilisha vipande muhimu vya hotuba kivuli ya bajeti ambavyo ni vya msingi.

LEAT YAWATAKA WANANCHI KUHIFADHI MAZINGIRA NA MALIASILI

Ni Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Asumpta Mshama akihutubia wananchi wakati wa sherehe za siku ya mazingira duniani, katika kijiji cha Lugodalutali, wilaya ya Mufindi

Tuesday, June 7, 2016

HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA KINARA KWA UJANGILI WA TEMBO NCHINI

Mwalimu wa Uchumi na Utalii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),  Profesa Wineaster Anderson (kulia), akitoa mada kuhusu uchumi na Utalii katika mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali mjini Morogoro leo.

Majambazi Yaliyotoroka Mapangoni Jijini Mwanza Yazua Hofu

Siku moja baada ya kutokea mapambano ya zaidi ya saa 16 baina ya Jeshi la Polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwenye mapango ya mlima ya Utemini, wananchi wa eneo hilo wameingiwa na hofu ya usalama wao baada ya baadhi yao kuona wahalifu wakitoroka wakati wa tukio hilo.

TRA Yakusanya Trilioni 1.032 Mwezi wa Tano

Ikiwa imewekewa lengo la kukusanya Sh12.054 kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Mei 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kufikia malengo kwa kukusanya Sh1.032 trilioni kwa kipindi cha mwezi uliopita, ikiwa ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo lililowekwa.

CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuwakabili CHADEMA Waliojipanga 'Kumharibia' Rais Magufuli kwa Wananchi

Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

IBADA YA UCHUMBA WA RICHARD JEREMIA NA HAPPY KULOLA YAFANA KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Richard Jeremia (Kulia) akimvisha pete ya Uchumba, Mchumba wake, Happness Daniel Kulola (Kushoto). Ibada ya kutangaza Uchumba huo ilifanyika jumapili iliyopita, June 05,2016 katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji Dr.Daniel Moses Kulola.
Sendoff inatarajiwa kufanyika June 29,2016 na Harusi Julai 03,2016.
Imeandaliwa na BMG

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More