Friday, May 27, 2016

Juma Nkamia Adai Wapinzani Wanasura Mbaya Kiasi Kwamba Wanataka Kutapika na Wengine Meno Yao Yameoza!

Kanuni inayozuia lugha ya kuudhi bungeni ni kiinimacho kwani mbunge wa upinzani akitoa lugha inayokera, mbunge wa CCM ataomba mwongozo kwa Spika na mara akijibiwa atasimama mbunge wa CCM na kutumia lugha hiyo hiyo iliyoombewa mwongozo.

Chumba Cha Dereva Tax Chazua Kizaa Zaa Mtaa Wa Mbezi Mtoni Gold Star, Jijini Dar Baada ya Kukutwa Kimejaa Makopo ya MIKOJO na KINYESI


Na Ripota wa Sufianimafoto ,Dar UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.

Lowassa Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Japani Hapa Nchini

May 27 2016, aliyekuwa mgombea Urais mwaka jana kwa tiketi ya Chadema na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini, Masahau Yoshida.

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG

Wednesday, May 25, 2016

MWIGULU CUP MBIONI KUANZA KUTIMUA VUMBI JIMBO LA IRAMBA

Mbunge  wa  jimbo la Iramba  Bw  Mwigulu Nchemba akikabidhi  vifa vya  michezo kwa  vijana  jimboni kwake  kwa  ajili ya  kuanza kwa kombe la Mwigulu jimboni humo

Wamiliki wa silaha watakiwa kuhakiki silaha zao kabla ya Juni 30

Jeshi la Polisi nchini limetoa wito kwa wamiliki wa silahi  kujitokeza na kuhakiki silaha zao katika Wilaya wanazoishi kabla ya kumalizika kwa zoezi hilo mnamo Juni 30 mwaka huu.

Milioni 392 Zajenga Barabara HEWA Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amebaini matumizi ya Sh392 milioni zilizoandikwa kwenye taarifa ya manispaa hiyo kuwa zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Sinza - Igesa ambao haukufanyika.

Lowassa azungumzia tuhuma za kukwapua ardhi ya wananchi, Lukuvi aahidi kumnyang’anya

Baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza Bungeni kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alijimilikisha ardhi iliyotolewa kwa wananchi wilayani Monduli mkoani Arusha na kuahidi kuirejesha, Mwanasiasa huyo amejibu tuhuma hizo.

MBUNGE WA MAFINGA MJINI ATOA MSAADA WA AMBULANCE JIMBONI KWAKE

MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi akizindua
gari la kubeba wagonjwa (ambulance) 
 na fredy mgunda,iringa
MBUNGE wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwa kushirikiana na asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Monday, May 23, 2016

Chadema Wamtaka Rais Magufuli Amfuate Lowassa Ili Amshauri Kuhusu Sukari

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais John Magufuli kuweka siasa kando na kuomba ushauri kwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ili kutatua tatizo la kuadimika kwa sukari.

Watumishi HEWA Waziponza Benki.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuweka mishahara ya watumishi hewa, kurejesha fedha hizo serikalini ; au kubainisha waliokuwa wakitumia akaunti hizo, kuchukua fedha.

Hatutamuadhibu Kitwanga Mara Mbili

CCM imesema kitendo cha Rais John Magufuli kumvua uwaziri Charles Kitwanga kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, kimedhihirisha kuwa bado kuna baadhi ya watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma, lakini hakitachukua hatua kwa kuwa ameshaadhibiwa.

Friday, May 20, 2016

Kessy Amvaa John Mnyika

Jina la aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vilivyounda Ukawa, jana liliingia tena katika Bunge la Kumi na Moja na kuzua mvutano.

Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.

Serikali Yajibu Hoja za Kivuko cha MV Dar es Salaam na Uuzwaji wa Nyumba Zake

Serikali imejibu hoja za upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali na kutetea ununuzi wa kivuko cha MV Dar es Salaam ambacho kilitakiwa kufanya safari zake kati ya Dar na Bagamoyo.

UTT-PID YAIWEZESHA MANISPAA YA LINDI KUVUNA BILIONI 2 KATIKA MRADI WA VIWANJA

IMG_6645
Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Bi. Elpina Mlaki akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi wakati wa mkutano huo ambao jumla ya Bilioni 2, za mradi wa viwanja kwa Manispaa ya Lindi ziliweza kupatikana katika mradi wa upimaji viwanja.

MSANII ELIZAYO HB KUTOKA JIJINI MWANZA AWAPA USHAURI WASANII CHIPUKIZI NCHINI.

Elizayo HB ni Msanii wa Kizazi kipya ambae anatoka Jijini mwanza. Anao ushauri kwa wasanii chipukizi nchini.

MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA MKOLANI SEKONDARI JIJINI MWANZA YAFANA

Jana Alhamisi, Mei 19,2016 ilikuwa ni siku yenye furaha kubwa kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza ambapo walikuwa wakisherehekea Mahafali yao ya Kuhitimu kidato cha sita.

Thursday, May 19, 2016

Zitto Kabwe, Halima Mdee na John Heche Wawekwa Kitimoto

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) na wenzake wawili, jana wamehojiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika kwa kufanya fujo bungeni kuhusu suala la Bunge kutorushwa ‘live’.

Magari Ya Washawasha Kugeuzwa ya Zimamoto

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema Serikali iko katika mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi magari ya polisi ya kuzuia ghasia kwa kurusha maji ya kuwasha maarufu washawasha yaweze kutumika kuzima moto.

Mbunge wa CCM Anusurika Kupigwa na Wabunge wa UKAWA

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Msongozi juzi jioni alinusurika kipigo kutoka kwa wabunge wanawake wa UKAWA baada ya kuwaeleza kuwa upande huo una wabunge wawili tu wenye michango ya maana ambao ni Upendo Peneza (Viti Maalumu Chadema) na Magdalena Sakaya (Kaliua - CUF).

Edward Lowassa na Fredrick Sumaye Watajwa Katika Sakata la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali.

Uuzwaji wa nyumba za serikali umegeuka mwiba huku wabunge wakiendelea kuhoji hatua zilizochukuliwa kutokana na kadhia hiyo

CHADEMA Yajipanga Kumng'oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uzito wa Rais John Magufuli kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na kutajwa kuhusika na Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kulitapeli Jeshi la Polisi, utasababisha waanze harakati za kumng’oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wednesday, May 18, 2016

Mtoto wa Chacha Wangwe Abadili Msimamo Mahakamani


Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari na Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amebadili msimamo mahakamani katika kesi ya kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii, kuwa Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake.

Mganga mbaroni akidaiwa kugoma kumhudumia mjamzito


Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga wilayani Serengeti kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua pacha na kusababisha kifo cha mtoto mmoja.

Upinzani Wamtega Rais Magufuli

Kambi ya Upinzani imelizidi maarifa  Bunge na kurejesha sakata la kuuzwa nyumba za Serikali ambalo juzi lilisababisha kiti cha Spika kuagiza yaondolewe maneno yanayomtaja Rais katika hotuba ya maoni mbadala. 

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili

Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

TRA Yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 Kufikia Lengo Lao

Na Ally Daud- Maelezo.
Mamlaka  ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.

"MAZIWA YA UNGA SI SALAMA KIAFYA"-BODI YA MAZIWA TANZANIA

DSC_3770
Afisa masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Michael Mkalati (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano huo juu ya hali ya maziwa hapa nchini uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Wengine ni watendaji wa bodi hiyo. 

Monday, May 16, 2016

WAFANYABISHARA ZAIDI 2500 WAKWAMA KUFANYA BIASHARA ZAO BAADA YA HOTELI KUFUGWA KWA MUDA


kushoto ni meneja wa hoteli ya star com iliyoko kilolo mkoani iringa wakiwana na wafanyakazi wa hoteli hiyo wakizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani baada ya hoteli hiyo kusitisha huduma zake kwa muda

Tuesday, May 10, 2016

Waziri Nchemba Awapasha Wafugaji na Wakulima

WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, amewataka wakulima na wafugaji kuacha kutumia uhai wa mtu kama fidia ya mifugo au mashamba yaliyoharibiwa kwa kuuana katika mapigano ya wenyewe kwa mwenyewe.

Rais Magufuli Awagomea Wabunge Nyongeza Ya Mikopo Ya Magari

Katika kile kinachoonekana amedhamiria kuendelea kubana matumizi ya serikali, Rais John Magufuli amekataa ombi la kuongeza fedha za ununuzi wa magari kwa wabunge pamoja na fedha za mfuko wa bunge.

Waziri Ataka Wakurugenzi NHC Washindanishwe

NAIBU  Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angeline Mabula, ametaka wakurugenzi  wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mikoa yote washindanishwe   kujua utendaji kazi wao.

Lowassa: Bado Nipo Nanyi Kuwaletea Maendeleo

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa amewahakikishia wananchi wa Monduli kuwa bado yupo nao katika kuwaletea maendeleo.

Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu.

Songas Yazima Mitambo Yao kwa Kuidai Tanesco Sh Blioni 194

Kampuni ya kufua umeme kwa njia ya gesi asilia, Songas Limited imezima mitambo yake, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kushindwa kulipa deni la Dola 90 milioni za Marekani sawa na Sh193.5 bilioni, jambo linalotishia ukosefu wa nishati hiyo muhimu nchini.

Makonda Awasimamisha Kazi Vigogo wawili wa Manispaa Kwa Tuhuma za Kushindwa kutoa Maelezo kuhusu Watumishi Hewa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasimamisha kazi wakuu wawili wa idara katika manispaa mbili kwa tuhuma za kushindwa kutoa maelezo kuhusu watumishi hewa katika idara zao, huku wakiendelea kuidhinisha mishahara yao kwa miaka mingi.

Wachungaji Wawili wa KKKT Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Mauaji

Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Vita Ya Sukari Yazidi Kupamba Moto

Suala la uhaba bandia wa sukari limeendelea kuitikisa nchi, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya kazi nzuri baada ya kuwatia nguvuni wafanyabiashara wengine, waliohodhi bidhaa hiyo kinyume cha sheria huku ikiwamo kukamata kilo 622,000 za mfanyabiashara Haruni Zakaria mkoani Morogoro.

Mbunge Apinga Wakunga Wanaume Kuruhusiwa Kuwahudumia Wanawake Wakati wa Kujifungua

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Riziki Mngwali amepinga mpango wa Serikali kuajiri wakunga wanaume katika baadhi ya zahanati kuhudumia wajawazito wakati wa kujifungua kuwa ni udhalilishaji dhidi ya wanawake.

Monday, May 9, 2016

Naibu Waziri Anthony Mavunde Apewa Maji Machafu na Wapiga Kura Wake Ili na Yeye Ayanywe

Wakazi wa Kijiji cha Nala na vitongoji vyake juzi walimpelekea maji machafu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde wakimtaka ayanywe kwa kuwa ndiyo wanayotumia.

Aswekwa Mahabusu Kwa Kusema Uongo Mbele ya Mkuu wa Mkoa

Mkazi wa Kijiji cha Natambiso, Kata ya Natta wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Christopher Nyamasagi ameswekwa mahabusu kwa tuhuma za kutoa taarifa ya uongo kuwa mjumbe mmoja mwanamke aliombwa rushwa ya ngono ili wapate mikopo ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Polisi Waua Majambazi Wawili Mkoani Mwanza.

Watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Mwanza baada ya kurushiana risasi na askari wakati wakiwa kwenye harakati za za kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Baraka Said.

Vigogo Chadema Kyela Wavuliwa Uongozi kwa Usaliti

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Saadati Mwambungu pamoja na wajumbe 19 wa kamati ya utendaji wa wilaya hiyo, wamevuliwa uongozi baada ya kutuhumiwa kukihujumu chama.

Saturday, May 7, 2016

Ahukumiwa Miaka Mitatu Kwa Kosa la Kumtukana Mtandaoni Mwanamke Aliyedai Anatembea na Mumewe

Mfanyabiashara Naila Aminel (24) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano baada ya kukiri kutumia mtandao wa kompyuta kutuma ujumbe wa lugha ya matusi.

Wakurugenzi Katavi Kikaangoni

Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Katavi, wameagizwa kurejesha Sh200 milioni wanazodaiwa kuwalipa watumishi hewa ndani ya siku 21.

Serikali Yabaini tani 4,579.2 za Sukari zilizokuwa zimefichwa

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) imebaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa  tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari Kilombero.

WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA WA WAAHIDI UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, akifafanua jambo wakati wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza yanayofanyika Jijini Mwanza.

Friday, May 6, 2016

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO MAALUMU KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kufikia tamati kesho Mei 07,2016.

Wabunge wa UKAWA Wamzomea Profesa Tibaijuka huku Wakimwita Mwizi.

Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka jana alikuwa mkali bungeni akisema yeye si mwizi na kuwabeza wanaomuita hivyo kuwa wataisoma namba.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More