Wednesday, November 18, 2015

asilimia 17 tu ndiyo kaya zenye vyoo bora mkoani iringa.

JUMLA ya kaya 201,120 ambayo ni sawa na asilimia 89 mkoani Iringa zina vyoo na kati ya Kaya hizo asilimia 17 tu ndiyo zenye vyoo bora.
Kauli hiyo imetolewa jana na katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Wamoja  Ayubu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo  ya kuhamamisisha  wanahabari juu ya usafi wa mazingira.
Ayubu amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwa kuwajengea uwezo wanahabari kujua mambo muhimu yanayohusiana usafi wa mazingira na matumizi ya choo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini.
Amesema kuwa hali ya unawaji mikono kwa sabuni ni sawa na asilimia tisa  huku hali ya matumizi ya choo na unawaji wa mikono kwa sabuni bado vikiwa bado vipo chini.
Naye ofisa afya wa mkoa wa Iringa Khadija  Haroun amesema mafunzo hayo yanaenda sambamba na wiki ya usafi wa mazingira hapa nchini.
Haroun amesema kuwa watu takriban milioni 1.8 wanakufa kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya kuhara.
Amesema kuwa watoto chini ya miaka mitano  760,000 hufa kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara kila mwaka.
Pia amesema kuwa tanzania watu 30,000 hufa kila mwaka kutokana na magonjwa ya kuhara.
Amesema kuwa asilimia 60 hadi 80 ya wagonjwa wote wa nje wana magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji na mazingira machafu.
 Naye Ofisa habari wa mkoa wa Iringa Dennis  Gondwe amewataka wanahabari mkoani hapa  kutoa elimu kwa jamii kuhusu mafunzo waliyoyapata katika mafunzo hayo ambapo alisema kwa kupitia waandishi wa habari jamii itapata elimu itakayowasaidia kuweza kuepukana na ugonjwa wa kuhara pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More