Tuesday, November 24, 2015

MVUTANO WA MEYA WA MANISPAA YA IRINGA WAZIDI KUIVURUGA CHADEMA

mwenyekiti wa chadema iringa mjini frank nyalusi.
wakatika ndio mwenyekiti wa chadema iringa mjini frank nyalusi.
 
NA RAYMOND MINJA IRINGA
Mvutano wa  nani atakaye kwa mrithi kiti cha aliyekuwa meya wa manispaa ya Iringa Amani Mamwindi (ccm) ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo chadema umeendelea kufukuta baada ya kusogeza mbele uchaguzi wa atakaye kuwa meya wa manispaa ya Iringa
uliokuwa ufanyike leo baada ya kupokea maagizo kutoka ofisa ya chama hicho kanda ya nyanda za juu kusini  mpaka hapo watakapo pangiwa tarehe nyingine ya kufanya uchaguzi

 Chama hicho kilikuwa kinaimgia katika historia ya kutoa meya wa kuiongoza halimashauri hiyo kumekuwa na mvutano wa chini kwa chini
ndani ya chama wa nani atakeyechukua kiti hicho huku wanachama na wananchi wakitao vigezo vya kuwa na  meya mwenye elimu nzuri ili aweze kuiongoza vema halimashauri hiyo

Hii ni  kwa mara ya kwanza chama hicho mkoani hapa kupata  viti 14 vya udiwani  hivyo kuwa na uwezo wa kuunda halimashauiri na  leo  ndio walikuwa wakiingia kwenye mchakato wa kura za maoni za nani atakayekalia kiti cha Meya na Naibu Meya ambaye ataongoza halmashauri ya manispaa ya Iringa kwa kipindi cha mwaka 2015/2020.


 Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Iringa ambaye pia ni diwani mteule wa chadema kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi alisema kuwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike leo umesitishwa na ofisi za kanda huku akishidwa
kueleza sababu za kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo

Nyalusi alisema kuwa tayari walikuwa katika maandalizi ya kumtafuta meya atakayerithi kiti cha meya ambapo hapo awali kilikuwa kikishikiliwa na  diwani wa Mlandege  Amani Mamwindi ambaye ameshinda udiwani katika kata yake lakini atashindwa kuwania nafasi hiyo
kutokana na chama chake kuwa na idani ndogo ya viti walivyoshinda (4)

Nyalusi alisema kuwa uchaguzi huo umeahirishwa mpaka hapo utakapotagazwa tena huku akisema mpaka  sasa wameshajitokeza madiwani sita ambao watatu wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Meya na wengine watatu kwenye kinyang’anyiro cha Unaibu Meya.

Nyalusi aliwataja madiwani ambao wemejitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi hizo huku wakisubiria maamuzi ya chama hicho.

Waliojitokeza kuwania nafasi ya Meya ni Diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyalus,diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata na Diwani wa kata ya Isakalilo Alex Kimbe.

Waliojitokeza kuusaka unaibu Meya ni diwani wa kata ya Gangilonga Dadi Igogo,Diwani wa kata ya Kwakilosa Joseph Lyata na diwani wa kata ya mkimbizi Evaristo Mtitu.

Mchakato wa uchukuaji wa fomu ulianza  Novemba 21 Mwaka huu na wanatarajia kurudisha fomu hizo leo Novemba 24 na kuingia kwenye kura za maoni huku gharama ya fomu zikiwa   Tsh.50,000 kwa kila moja.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa wakiwamo madiwani wenyewe wamekuwa na mchecheto wa kumjua nani atakaye kuwa mrithi wa Meya aliyemaliza muda wake na pia ni diwani mteule wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Mlandege Aman Mwamwindi.

Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara wa mjini Iringa Abdulikarim Abubakari  alisema  kuwa madiwani hao wanapaswa kumchagua meya atakayekuwa na tija na halimashauri mwenye uwezo wa kupitia mikataba mibovu inayoingiwa na halimkashauiri na kuachana na kasumba ya kuchagua kiongozi kwa mazoeya au ya uchama

Alisema kuwa chama hicho kinapaswa kufanya kazi kwa weledi na maarifa kwani endapo watachezea nafasi waliyopewa wasitegemee kuchaguliwa katika kipindi kijacho kwani watu watakuwa wanachagua kiongozi kwa kile kitu alicho kifanya katika jamii na wala awatachagua mtu kwa umaarufu wake au ushabiki wa kichama

Alisema kuwa nchi hii inahitaji viongozi shupavu kama Raisi Magufuli kwani amekuwa akifanya kazi kwa vitendo na wala si kwa mazoeya na wale viongozi wazembe na walafi wameshanza kuona ofisi zao chungu kwa kuwa
walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya hivyo kila mmoja anapaswa kusimama vema katika nafasi yake ili kuipata Tanzania mpya

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More