Sunday, November 8, 2015

LUKUVI ATAKA WANANCHI KUPUUZA UZUSHI WA MITANDAONI

Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa hasa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyemaliza muda wake Ndg William Lukuvi kumpeleka mfanyabiashara maarufu nchini Ndg Tanil Somaiya kwa Rais John Pombe Magufuli ili kumtambulisha kwake mfanyabiashara huyo.

Taarifa hiyo sio ya kweli, ni uzushi wa kutunga ambao unalenga kumchafua Mheshimiwa Lukuvi na kuharibu haiba yake mbele ya jamii.

Tangu baada ya kutangazwa, kuapishwa na kuanza kazi rasmi kwa Rais Magufuli, Mhe Lukuvi hajawahi kwenda nyumbani kwake ama ofisini kwa lengo la kumtambulisha mfanyabiashara wala mtu yeyote.

"Mimi ni kiongozi wa muda mrefu mwenye uzoefu na ninayezingatia nidhamu ya uongozi na utawala bora, siwezi kufanya jambo hilo ambalo ni kinyume na kanuni, taratibu na sheria za kiutendaji" amesema Mheshimiwa Lukuvi.

Mhe Lukuvi amesikitishwa sana na taarifa hiyo ambayo imeendelea kusambaa mitandaoni na amewataka watanzania kuipuuza taarifa hiyo lakini pia amechukua hatua stahiki zinazohusu makosa ya kimtandao kwa wanaohusika.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More