Wednesday, November 18, 2015

Trafiki 78 watimulia kwa utovu wa nidhamu

Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo

ASKARI 78 wa usalama barabarani Mkoa wa Mwanza, wameondolewa katika nafasi zao na kupangiwa kazi nyingine katika vitengo mbalimbali kutokana na utovu wa nidhamu. .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo, akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema mabadiliko hayo yamefanywa baada ya askari hao kujulikana hawafuati maadili na sheria za jeshi hilo.

Mkumbo alisema kuwa askari waliondolewa nafasi hizo na kupangiwa vitendo vingine ni 78, huku akisema kwamba wilaya ambayo haijafanyiwa mabadiliko ni Ukerewe kati ya saba za mkoa huo.

“Tumefanya mabadiliko haya ni ya kawaida tu, tumefanya hivyo ili kuleta utendaji wenye tija, baada ya kubaini kuna mapungufu kwa askari hao na tusingeendelea kuwa nao kwa kuwa ni watovu wa nidhamu.

“Wilaya ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Nyamagana askari 19, Ilemela 23, Sengerema 15, Magu 15, Misungwi na Kwimba mmoja (1), wilaya ambayo haijaguswa ni Ukerewe,” alisema Mkumbo.

Hata hivyo Mkumbo alisema kuwa kabla ya kufanyika kwa mabadiliko hayo, walianza kutoa mafunzo kwa askari waliochukua nafasi hizo, kabla hawajaingia barabarani.

Mkumbo alisema kuwa kabla ya mabadiliko hayo mkoa wa Mwanza ulikuwa na trafiki 249, na kwamba walioondolewa katika nafasi hizo ni askari wa kawaida na vyeo mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More