Thursday, June 28, 2018

MBUNGE WA KILOSA MBARAKA BA WAZIRI AWACHIMBIA KISIMA WANANCHI WA KIJIJI CHA RUDEWA NA KUTOA MSAADA WA MAMABTI NA SIMENTI

Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri ametoa msaada wa ujenzi wa kisima kikubwa cha mita 100 ambacho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya vijiji viwili katika kijiji cha Rudewa kilichopo kata ya Rudewa wilayani Kilosa  ambapo ujenzi wake umeanza mara moja, kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kuwa tatizo sambamba na ahadi ya  ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya huduma ikiwemo ya wajawazito pamoja na watoto huku tayari akiwakilisha  bati 120 waajili ya ujenzi wa kituo cha afya simenti 200 kwaajili yakujenga vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Rudewa katika wilaya ya Kilosa.
Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akimpa mkono diwani wa kata ya Rudewa Subiri Joseph wakati akikabidhi mradi waujenzi wa kisima cha mita 100 kwaajili ya kutatua kero ya maji katika kijiji hicho kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Kilosa Aziza Juma   kushoto Hassan Mkopi Mwenyekiti wa Halmahauri wilaya ya Kilosa pamoja na viongozi mbalimali wa CCM na serikali.
Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akikabidhi diwani wa kata ya Rudewa Subiri Joseph moja ya mfuko wa simenti kama mfano  kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya shule katika kijiji cha Rudewa Kata ya Rudewa Walayani Kilosa ambapo alitoa msaada wa simenti 200 kwaajili ya shughuli hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Rudewa Hamad Maboga akipokea bati kutoka kwa diwani wa kata hiyo Subiri Joseph wakati wakikabidhiwa msaada wa vifaa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji hicho.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akihutubia wakazi wa vijiji na kata ya Rudewa wakati wa mkutano na wananchi hao alipokua akisikiliza kero na kutoa utatuzi wa kero hizo ikiwemo katika sekta ya Afya, Elimu na Maji.
Wakazi wa Kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wakiwa makini kumsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo Mbraraka  Ba Waziri wakati alipokua akifanya mkutano na wananchi hao akiskiliza kero na kutoa utatuzi kwa baadhi ya kero hizo
 Diwani wa kata ya Kimamba  Pendo Mpoto akihutubia wananchi wa kata ya Rudewa wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri alipoku akiongea na wananchi kuhusu matatizo mbalimbali ya nayo wakabili sambamba na kutoa msaada wa vifaa kwaajili ya utatuzi wa kero za Maji Elimu na Afya.

Sunday, June 24, 2018

BAVICHA WAWEKA MIKAKATI ZANZIBAR KUKISAIDIA CHAMA.

Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa leo katika ukumbi wa ofisi za Kanda ya Unguja kwa pamoja wameweka mikakati ya kukusaidia chama na Baraza katika visiwa vya Zanzibar.

Kikao hicho wakuu viongozi wa BAVICHA Taifa wakiongozwa na M/kiti wa BAVICHA Taifa Mh Patrick Sosopi ,Mh Zeudi Mvano Makamu M/kiti Zanzibar na Mh Edward SIMBEYE Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa kilihudhuriwa viongozi wote wa mikoa wilaya na majimbo yote ya Kanda ya Unguja.

Katika Kikao hicho M/kiti amesisitizi ujenzi wa Baraza kwa kasi kubwa sana ili kuendana na ratiba na Kalenda ya chama tuliyojiwekea.

Amesisitiza vijana kuendelea kujitoa kukipigania chama pamoja na mazingira magumu ya kisiasa yanayoendelea katika nchi yetu.

Pamoja na vikao hivyo vya ujenzi wa Baraza vinavyoendelea M/kiti kwa kushirikiana viongozi wa chama kutoka maeneo mbalimbali pamoja na Makamu M/kiti na Mwenezi kesho wataendelea na uzinduzi wa matawi na misingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Mpendae na Jimbo la Mto Pepo.

Edward SIMBEYE
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa.

Edward SIMBEYE

Thursday, June 21, 2018

Chumi aitaka TRA kupanua wigo wa elimu kwa mlipa kodi

Na Fredy Mgunda

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameitaka Mamlaka ya Mapato nchini kukutana mara kwa mara na wafanyabiashara ili pamoja kutoa elimu ya mlipa kodi, isikilize kero zao.

Chumi alisema hayo leo tarehe 21 Juni, 2018  wakati akichangia mjadala  wa bajeti kuu ya serikali.

Mbunge huyo alisema kuwa ilifika wakati ilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa mbao mpaka pale kilio chake kiliposikika na Serikali kuamua kumtuma Kamishna wa Kodi za ndani kwenda kukutana na wafanyabiashara wa Mafinga.

 tunachotaka serikali ikusanye chake lakini bila kuumiza wafanyabiashara, alisisitiza Mbunge huyo.

Akizungumzia fedha za miradi viporo, Chumi aliitaka serikali kutoa fedha hizo mapema kwa kuwa bado siku tisa tu ili mwaka wa fedha kufikia mwisho.

Na hizo mtakazotoa kwa awamu zionekane katika kitabu cha matumizi, kinyume chake pamoja na kuwa naiamini serikali, tunaweza kupigwa changa la macho

Akizungumzia changamoto za mapato, Chumi alisema kuwa Taifa linapoteza mabilioni ya fedha kutokana na kukosa usimamizi wa kufahamu kiwango cha mafuta kinachoingia hapa nchini.

hii flow meter ameshaenda Mhe Rais, ameenda Waziri Mkuu tena mara mbili, lakini ujanja ujanja umeendelea, na Taifa linapoteza fedha

Kuhusu michezo ya kubahatisha, Mbunge huyo alisisitiza kuwa ili kuleta uwiano ni afadhali mazingira yakawa rafiki ili kuvutia wachezaji wengi na hivyo kuongeza mapato ambayo alishauri sehemu ya mapato hayo itengwe kuendeleza michezo.

Chumi alisisitiza kuwa, kwa kuwa vyanzo vingi vimechukuliwa na Serikali kuu, asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani inayotengwa kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu haitoshelezi hivyo Serikali ione uwezekano wa kutoa 10% kama ruzuku.

Akigusia msamaha wa kutoka 25% hadi 15% ya karatasi za kuzalishia madaftari, Chumi alisema kuwa HS Codes zilizotajwa ni kwa ajili ya karatasi ngumu zinazotumika kwa ajili ya kutengenezea maganda ya nje ambayo katika daftari ni 3% tu ya gharama.

kama nia ni hiyo basi kaangalieni upya hizi HS Codes zenu, vinginevyo hatustahili kupiga makofi kwa jambo hili

Saturday, June 16, 2018

DK. MNDOLWA AMALIZA ZIARA YAKE KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA MKOA WA SINGIDA

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akipata maelezo kuhusu eneo lenye madini la Jumuiya hiyo lililopo katika Kijiji cha Bigigi, alipokagua eneo hilo akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Singida, jana. Anayempa maelezo ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Mjini Ali Balo (Wapili kushoto) na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Sosthenes Masola. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar Haidar Haji abdallah. Dk. Mndolwa ameagiza uongozi wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Singida kuharakisha kulitafutia leseni na kuliwekea vigingi vya mipaka eneo hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, jana. 
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akishiriki kucheza ngoma, iliyokuwa ikitumbuizwa wakati akipokewa kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Singida alipofika kwenye ofisi hiyo kuwanza ziara ya kikazi mkoani humo jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu akimtuza msanii wa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Dk. Edmund Mndolwa katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida jana.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa na Makamu Mwenyekiti wake upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah wakisaini vitabu vya wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, jana.
 Katibu wa CCM mkoa wa Singida Jimson Mhagama akisoma taarifa ya Chama ya mkoa.
 Kamishna Msaidizi wa Madini kanda ya Kati Sosthenes Masola (wapili kulia), akiwa na baadhi ya viongozi na maofisa wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Singida
 Baadhi ya maafisa kutoka Makao Makuu ya Jumuiya ya Wazazi Tanzania wakifuatilia wakati Dk. Mndolwa alipongia katika Ofisi ya CCm mkoa wa Singida kusaini vitabu vya wageni.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Singida Mashigani Kija akisoma taarifa ya jumuiya hiyo mbele ya Dk. Mndolwa
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akipata maelezo kuhusu eneo lenye madini la Jumuiya hiyo lililopo katika Kijiji cha Bigigi, alipokagua eneo hilo akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Singida, jana. Anayempa maelezo ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Mjini Ali Balo.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Friday, June 15, 2018

BITEKO AELEKEZA TUME YA MADINI KUPELEKA TIMU YA WAKAGUZI WA MADINI WILAYANI ULANGA

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wananchi wa kijiji cha Ipanko juu ya changamoto ambazo wanakabiliwa nazo na kuunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote na aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika seckta ya madini. 
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Naibu waziri wa madini mheshimiwa Doto Bitoke alifanya ziara ya kutatua mgogoro baina ya wawekezaji na wananchi kwenye sekta ya madini

NA FREDY MGUNDA,MOROGORO.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa ataunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote nchini ikiwa ni pamoja na utambuzi wa aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika sekta ya madini.

Akizungumza wakati wa ziara ya siku mbili Mkoani Morogoro Mh Biteko alisema kuwa madini yote yaliyopo katika ardhi ya Tanzania ni mali ya watanzania hivyo yanapaswa kuwanufaisha watanzania kwanza ndipo watu wengine wafuate.

“Naombeni watanzania wote mjue kuwa madini haya ni mali ya watanzania wote hivyo tunapaswa kuyalinda na kutoa taarifa sahihi kwa serikali kama kuna mtu anaiibia serikali kwa namna moja au nyingine ili serikali iweze kuchukua hatua za kisheria dhidi yake, Na mimi nawaambieni watanzania tuache uoga tuseme ukweli kama Rais wetu Mhe Dkt John Pombe Magufuli anavyosisitiza utendaji wa uwazi na uwajibikaji katika serikali” Alikaririwa Mhe Biteko

Biteko amepiga marufuku wawekezaji kutumia fedha zao kuwanyanyasa wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo kuna migodi kwa ajili ya kuwaibia watanzania ambao bado wana kipato cha chini katika maeneo yanapopatikana madini.

“Najua hawa wawekezaji wanapesa nyingi sana hivyo isiwe sababu ya kuwarubuni baadhi ya wananchi na kuwatesa wananchi wengi hususani waliopo kwenye maeneo ya madini na leo nataka niwaambie ukweli wawekezaji wote nchini najua ambavyo mnatumia pesa zenu kuwanyanyasa wananchi, sasa ndio mwisho wenu maana serikali ya awamu ya tano inataka haki kwa kila mwananchi” Alisisitiza Biteko

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Bitoke alifanya ziara ya kikazi katika kijiji cha Ipanko kilichopo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kugundua kuwa kuna wawekezaji wanaidanganya serikali na wananchi kwa kutoweka wazi kiasi gani ambacho wanakipata kwenye migodi iliyopo katika kijiji hicho.

“Jamani wana Ipanko nchi hii tumeibiwa sana sasa ifike mwisho tusema hapana haiwezekani tena kwenye serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli tuendelee kuibiwa madini yetu na kuwanufaisha watanzania ambao wapo nje ya nchi yetu, Rais kashasema na sisi wasaidizi wake tunaungana naye kwamba iwe mwisho kuchezewa kwa rasilimali zetu”

“Chonde chonde nyie viongozi wetu wa ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa tunaomba msituangushe kwa kupokea rushwa kutoka kwa wawekezaji na kuisaliti nchi yako kuendelea kuibia kirahisi namna hii” alisema Biteko

Biteko alieleza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inawapenda sana kuwa na wawekezaji wengi wenye tija ambao sio wababaisha na ambao wamekuja nchi kuiba rasilimali za watanzania.

Aidha, Biteko alisema kuwa haiwekani muwekezaji akawekeza Bilioni 42 halafu akachangia madawati na mifuko ya saruji katika jamii kama ndio mchango wake, haiwezekani wanapaswa kuchangia kulingana na kiasi ambacho wamewekaza kwa faida na manufaa ya wananchi.

“Mimi binafsi hainiingi akilini kuona muwekezaji amewekeza pesa nyingi kama hizo halafu kwenye shughuli za kimendeleo amechangia kiasi kidogo namna hiyo kwangu nasema haiwezekani na nchi hii kwa sasa sio yakuchezewa tena” alisema Biteko

Lakini pia Naibu waziri huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe Goodluck Mlinga kwa kuwapigania wananchi wake kwa kuzifikisha kero mahali husika na kutafutiwa ufumbuzi.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Pangarasi Kanyali, Cyprian Kanyali, Micky Sengo, Doedatus Moholeli, Hilda Linoma na Fredrick Kazimoto  walimpongeza Naibu Waziri wa Madini Mhe Biteko kwa kufika kijiji hapo na kusiliza kero zao kwani wana amini zitatafutiwa ufumbuzi kwa kufuata sheria na katiba ya nchi.

“Toka sisi tuzaliwe hatujawahi kutembelewa na waziri na kusikiliza kero zetu kama ambavyo wewe umefika kijijini kwetu leo hii tunajisikia wenye amani na furaha kwa kuwa tunajua kero zetu tunazifikisha moja kwa moja kwa kwa Rais wetu kupitia wewe waziri” Walisema wananchi hao

Awali Mbunge wa Jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga alisema kuwa lengo la waziri kufika katika kijiji hapo ni kujionea kero wanazokumbana nazo wananchi kupitia wawekezaji wa sekta ya madini na kuzitafutia ufumbuzi.

“Huku ni mbali sana Mheshimiwa Naibu Waziri lakini kuna madini mengi ambayo ndio utajiri wa nchi hii hivyo tunapaswa kuwa makini na hawa wawekezaji maana wamekuwa wakiibia sana serikali yetu” Alisema Mlinga

Saturday, June 9, 2018

KAMPUNI YA ASAS YADHAMINI LIGI YA MKOA WA IRINGA KWA MIAKA MITATU KWA KIASI CHA TSH MILIONI MIA MOJA

 Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Iringa (IRFA) Cyprian  Kuyava akiwa na viongozi wengine wa chama hicho pamoja na mdhamini wa ligi ndugu Feisal Abri Asas ambapo waimeingia mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini ligi ya mkoa wa Iringa kwa shilingi milioni mia (100,000,000/=) ambapo ligi hiyo itakuwa inaitwa  ASAS IRFA SUPER LEAGUE.  

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

KAMPUNI ya Asas limited ya mkoani Iringa imeinga mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini ligi ya mkoa wa Iringa kwa shilingi milioni mia moja(100,000,000/=) ambapo ligi hiyo itakuwa inaitwa  ASAS IRFA SUPER LEAGUE.

Akizungumza na waadishi wa habari katika ofisi za IRFA mwenyekiti wa chama hicho Cyprian Kuyava alisema kuwa udhamini waliipata kutoka kampuni ya Asas limitedutasiadia kuongeza chachu ya ushindani kwa vilabu vyote mkoani Iringa ambayo vitakuwa vinashiriki.

“Tumekuwa tukiendesha ligi hii bila kuwa na mdhamini wa kudumu ila sasa tumepata mdhamini ambaye atakuwa masaada mkubwa kwa kuongeza nguvu katika vilabu kuandaa timu ambazo zitakuwa bora na zenye ushindani” alisema Kuyava

Kuyava alisema kuwa udhamini huo utakuwa wa miaka mitatu ambao utagusa katika maeneo mbalimbali kama vile zawadi ya mshindi wa kwanza,mshindi wa pili,mshindi wa tatu,kutoa jezi seti mbili kwa vilabu vyote ambavyo vitakuwa vinashiriki,kutoa zawadi kwa mwamuzi bora,kipa bora,mfungaji bora,mchezaji bora,choka bora pamoja na zawadi wa waandishi wa habari ambao watafanya vizuri kazi.

“Kila timu itapata jezi seti mbili,mipira miwili kwa timu zote shiriki lakini bingwa atapata kombe na shilingi million mbili,jezi seti moja,mipira mitatu, na nafasi ya kushiriki ligi ya mikoa, Mshindi wa Pili shilingi  1mil, Mipira 2, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki,Mshindi wa Tatu - Tsh 500,000/=, Jezi Seti 1, Cheti cha Ushiriki” alisema Kuyava

Kuyava aliongeza kuwa kuanzia msibu ujao kutakuwa na zawadi kwa waadishi wa habari ambao watakuwa wameripoti vizuri mashindano hayo kama ifuatavyo Mwandishi bora blog  atapata shilingi 50,000, Mwandishi bora Tv atapata shilingi 50,000, Mwandishi bora Redio atapata shilingi 50,000 na Mwandishi bora gazeti atapata shilingi 50,000

Baada ya kilio cha muda mrefu hatimaye ligi ya mkoa wa Iringa imepata mdhamini na sasa itajulikana kama ASAS IRFA SUPER LEAGUE

Kwa upande wake mdhamini wa ligi hiyo kutoka kampini ya Asas limited Feisal abri asas alisema kuwa kilichomvutia kuwekeza katika ligi ya mkoa wa Iringa ni kupanda kwa hamasa ya michezo mkoani Iringa na kuwa na viongozi ambao wanaupenda mchezo wa mpira wa miguu.

“Mimi ni mdau wa mpira wa miguu na nimekuwa nikifaatilia kwa ukaribu mno ligi ya mkoa wa Iringa na kugundua kuwa kwa sasa hamasa ya mchezo huu imekuwa sana ndio maana nimeamua kudhamini ili kuongezea amasa ya vilabu kushiriki kwa wingi” alisema Feiasl


Friday, June 8, 2018

RITTA KABATI CHALLENGE CUP KUZINDULIWA JUMAPILI HII KATIKA UWANJA WA KRELUU

 Baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu kutoka Manispaa ya Iringa mjini,Iringa vijiji na kilolo walipofika kuhudhulia droo ya kupata timu pinzani
 Baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu wa kundi la Mufindi wakiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya mashindano ya RITTA KABATI CHALLENGE CUP

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

JUMLA ya timu sitini na mbili (62) za mkoani Iringa kushiriki mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup ambayo yatalindima katika viwanja mbalimbali vya mkoani hapa.

Aklizungumza na blog hii mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup Gerald Malekela alisema kuwa mwaka 2018 umeanza kwa mafikio makubwa kwa kupata timu nyingi tofauti na ilivyokuwa msimu wa mwaka 2017 ambapo mashindano yaiisha kwa mafanikio makubwa.

“Mwaka huu timu zimejitokeza nyingi sana tofauti na tulivyoanza mwaka wetu wa kwanza lakini tunamshukuru mwenyezi mungu kwa kuwa mwaka huu timu zimekua fomu nyingi na timu zote ni nzuri” alisema Malekela

Malekela alisema kuwa kamati ya mashindano hayo imejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa michezo yote inachezwa kwa kufuata sheria za mpira wa miguu na kufuatilia kwa  umakini mno kila hatua ya kila mechi ili kuakikisha kuwa wanazitatua changamoto ambazo zinakuwa zinajitokeza kwenye michuoano hiyo.

Aidha Malekela alisema kuwa mashindano hayo yatazinduliwa siku ya tarehe kumi mwezi wa sita katika uwanja wa chuo cha Kreluu wananchi na wapenzi wa soka mkoani iringa mnakaribishwa

JAMII ISHIRIKISHWE MABADILIKO TABIA NCHI KUWA NA KILIMO CHENYE TIJA

 Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku akitoa utambulisho wa wanenaji wa mdahalo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.
 Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba akizungumzia malengo ya warsha wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo Bi. Shakwaanande Natai akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa nchi kwenye mikutano ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi akizungumzia vionjo vinavyotarajiwa kufanywa kuhusu uhifadhi wa mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (wa pili kushoto) akifafanua kanuni za kufauta katika kuhifadhi mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Tafiti zilizoanishwa ESRF, Bi. Vivian Kazi (kulia), Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (wa tatu kulia), Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba (wan ne kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango (kushoto) akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale akifafanua jambo wakati majadiliano kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mshiriki akichangia mada wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (katikati) akibadilishana mawazo na Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (kushoto) wakati wakielekea kwenye eneo la kupiga picha ya pamoja kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
 Picha ya pamoja ya washiriki wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
JAMII inayojitambua ndiyo inayoweza kutumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha  kushindikana kwa mipango mingi ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira kunatokana na uelewa duni na mipangilio isiyozingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo husika.
Kauli hiyo imo katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ofisi za ESRF.
Katika mdahalo huo uliowezeshwa na Shirika la Kimataifa la Care kwa kushirikiana na taasisi ya FANRPAN na ESRF imeelezwa kuwa kuna changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo na ukuaji wake kutokana na n chi nyingi Kusini mwa Afrika kutegemea mvua.
Aidha ilielezwa kuwa changamoto nyingine ni umaskini uliokithiri, upungufu nmkubwa wa raslimali watu, maandalizi hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu dhaifu.
Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko alisema kwamba kumekuwa na kulegalega kwa matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira miongoni mwa wananchi na uwezeshaji kwa watendaji kiasi cha kuharibu muitikio unaonekana wakati wa mafunzo.
Chinoko alisema kwamba kutokana na hali hiyo walibuni kanuni ambazo wao wanaziita SUPER kanuni ambazo zikifuatwa vyema zinajibu matatizo yaliyopo sasa.
Alisema kwamba Super ni mfumo wa uchakataji wa taarifa na utekelezaji wake unaolenga kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao ndio washiriki wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uzalishaji wa chakula.
Alisema kwa kutumia kanuni hizo wananchi wanaweza kutambua mwendelezo wa rasilimali ardhi na misitu waliyonayo, wakawezesha kuitumia kwa faida kutokana na uadimu wake.
Aidha kanuni hizo zinahitaji mipango kuzingatia usawa wa kijinsia  ili kuteketeleza sera katika uchumi.
Alisema mfumo wa masoko unazungumzwa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo ili kuipaisha na kuifanya kuwa na tija zaidi.
Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la kuwasilisha taarifa huku watengeneza sera wakiwa pekee yao bila kushirikisha wananchi ambao ndio watendaji wenyewe.
Katika mdahalo huo mada zingine ziliwasilishwa na Bi. Shakwaanande Natai, Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo akishughulikia sera katika kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa nchini Tanzania.
Pia kulikuwa na mada iliyowasilishwa na Bw. Richard Muyungi kutoka ofisi ya Makamu wa Rais ambaye alizungumzia vionjo vilivyokusudiwa katika kuhakikisha wanazungumza kilimo kinachozingatia mabadiliko hali ya tabia nchi (INDCs) Tanzania.
Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network( FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba alisema kwamba matokeo ya ushauri  katika mdahalo huo utafikishwa katika kanda na baadae dunia kwa kuwa utekelezaji wa mashauri hayo ni wa lazima kuzingatia mahitaji ya ulinzi wa mazingira kwa kuzingatia kilimo kinachoangalia mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema kwamba watatumia maazimio na ushauri kutoka katika mdahalo huo katika majukwaa mengine muhimu duniani ambayo yanazungumzia makubaliano ya COP 19 na maazimio ya Lome.
Alisema mdahalo huo ni muhimu katika kubaini utayari wa Tanzania na changamoto zake katika kuendesha kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi na kuhakikisha usalama wa chakula na lishe.
Alisema pamoja na kuwepo kwa sera nzuri za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kumekuwepo na hasara kubwa katika kilimo kinachofikia dola za Marekani milioni 200 duniani.
Alisema hasara hiyo ni tishio kwa maisha na kusema kwamba ni vyema wataalamu  naa wananchi wakazungumzia changamoto zilizopo kwa bara la Afrika ambalo linaweza kulisha dunia nzima kama mipango itachambuliwa ipasavyo kwa kushirikisha wananchi na wagani.
Alisema kilimo lazima kifanywe kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya tabia nchi ili kiwe na tija na kukabiliana na mafuriko, ukame, wadudu na magonjwa yanayotokana na mabadiliko hayo.
Bi. Shakwaanande Natai alisema kwamba Tanzania ipo tayari kufanya  kilimo cha kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na kuwapo kwa sera na sheria zinazohimiza kilimo chenye tija.
Alisema mipango ya kilimo ya sasa inazingatia mabadiliko hayo pamoja na kutengeneza mfumo wa masoko ili kusaidia watu maskini kabisa wakulima kuwa na uwezo unaotakiwa katika kujisaidia kiuchumi.
Bw. Danford Sango akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema kwamba mdahalo huo ni muhimu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa tishio kwa ustawi wa wanadamu.
Aidha aliwakaribisha wataalamu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kushiriki katika mdahalo huo wenye tija kwa mataifa ya Kusini mwa Afrika.

MWENYEKITI CCM IRINGA KUNYANG’ANYA KADI WANACHAMA WANAOVUNJA KANUNI,SHERIA NA KATIBA YA CHAMA

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Mufindi wakimusikiliza kwa umakini mkubwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila wakati wa ziara yake ya kwanza ya kikazi 
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Iringa wakiwa kazini kupata habari kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akipokelewa na green gard wa wilaya ya Mufindi na kupewa heshima anayostahili
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akivishwa skafu nagreen gard wa wilaya ya Mufindi 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya wilaya hiyo mjini Mafinga,Chalamila alisema kuwa amesikia kuwa kuna wanachama wameanza kupita pita kuanza kufanya kampeni za chini chini na kusababisha wapunge wa majimbo hayo kutofanya kazi zao kwa ufanisi. 

Chalamila aliyataja Majimbo ambayo wananchama hao hao wameanza kupita ni jimbo Mafinga Mji linaloongozwa na Mbunge Cosato Chumi, jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamudu Mgimwa na Mufindi Kusini Meldrad Kigolla.

Alisema kuwa anafanyakazi kwa ukaribu na vyombo ya usalama wa taifa ili kupata taarifa ambazo ni sahihi na kuwabaini baadhi ya wana CCM walioanza kujitengenezea mazingira kwa ajili ya kupata uteuzi katika uchaguzi mkuu ujao kinyume na kanuni hizo za chama.
  
Chalamila aliwataka viongozi waliochaguliwa na wananchi kufanya kazi kwa kujituma na kukitendea haki chama cha mapinduzi (CCM) ili kiendelee kuaminiwa na wananchi 

Aidha Chalamila alisema katika mazingira ya kusikitisha alisema wana CCM wengine wanaoshiriki kuhatarisha amani ndani ya chama hicho ni wale waliopewa dhamana ya kuwa wajumbe wa vikao vikubwa vya chama na katika onyo lake kwao aliwatahadharisha dhidi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kwao.

“Waacheni wabunge na madiwani waliopo wafanye kazi, wamalize miaka yao mitano kwa uhuru. Mliwachagua wenyewe, wapeni nafasi na kama mnataka kuamua vinginevyo subirini hadi pazia la uchaguzi litakapofunguliwa lakini sio sasa,” alisema Chalamila.

Mwenyekiti  huyo aliwataka wajumbe  hao,kuhakikisha wanaweka mikakati  ya ushindi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa kuhakikisha wanazirudisha ndani ya ccm  kata  2 zilizochukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 wilayani humo.

Chalamila alizungumzia visasi na mioyo ya kinyongo miongoni mwa wana CCM wakati na baada ya chaguzi za chama na jumuiya zake, na za serikali akisema; mambo hayo yamekuwa yakisabisha mpasuko wa muda mrefu ndani ya chama hivyo ni lazima yaachwe.

“Visasi na vinyongo vimevuka mipaka. Wapo pia wana CCM ambao kila kukicha kazi yao ni kuwazushia na kuwachafua wenzao kwamba ni wafuasi wa vyama vingine vya siasa kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba wana mienendo mibaya ndani ya chama mambo ambayo si ya kweli. Wana CCM tupendane na tutendeane mema,”alisema Chalamila.

Aliwataka wenye taarifa za wanachama wenye mienendo mibaya na inayotishia uhai wa chama waziwasilishe kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba ya chama ili ziweze kufanyiwa kazi.

Mwenyekiti Chalamila alimalizia kwa kusema kuwa watawanyang’anya kadi wanachama wote ambao watakuwa wanaendelea kuvunja kanuni,sheria na katiba ya chama cha mapinduzi

“Kwakweli nitakuwa mkali sana na nitasimamia vilivyo kwa wale ambao watakuwa wanavunja kanuni,sheria na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuwa madaraka hayo ninayo kwa mujibu wa kanuni na sheria za chama chetu” alisema Chalamila

Baada ya kukutana na halmashauri kuu ya CCM ya wilaya ya Mufindi, Chalamila anatarajiwa pia kukutana na na wajumbe wa vikao hivyo wa wilaya ya Kilolo, Iringa Vijijini na Manispaa ya Iringa katika ziara yake anayofanya akiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Viti 15 Bara), Theresia Mtewele

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More