Friday, November 20, 2015

MKOANI IRINGA UNAKABILIWA NA TATIZO KUBWA LA UPUNGUFU WA MAAFISA UGANI

NA RAYMOND MINJA IRINGA
Upungufu wa maafisa ugani imekuwa ni tatizo kubwa mkoani Iringa hali hali inayopelekea afisa ugani mmoja kuhudumia wakulima zaidi 2,500 Manispaa ya Iringa tofauti na uwiano wa kitaifa ambapo afisa mmoja anatakiwa kuhudumia wakulia 800.
Akizungumza na wakulima wa mahindi, wasindikaji wa unga na wauzaji wa pembejeo kwenye ukumbi wa Kanisa la Anglikana Manispaa ya Iringa Afisa Masoko wa Shirika la BRAC Stephano Mahenge alisema jambo hilo lina athari katika uzalishaji wa mahindi Iringa.
Mahenge alisema tathimini waliyofanya kati ya Mei na Julai mwaka huu ambayo ilijumuisha masoko Manispaa ya Iringa walibaini kuwa kuna maafisa ugani 16 katika kata 18 zilizopo na kupelekea mzigo mkubwa kwa watumishi waliopo.
Msindikaji wa unga Changae Juma alisema kiwango cha mahindi kinachozalishwa mkoani Iringa hakiwatoshelezi wasindikaji wa unga wa Manispaa ya Iringa hivyo hulazimika kwenda kufuata malighafi hiyo mikoa ya jirani ya Njombe, Ruvuma na Mbeya.
Afisa kilimo wa Manispaa ya Iringa Richard Nyegela alisema hali ilivyo kwa sasa kwa Halmashauri hiyo ni nafuu kwa kuwa kila kata ina mtaalamu wa kilimo isipokuwa kwa kata zilizopo kati kati ya mji.
Mwenyekiti wa shamba darasa la Ipogolo, Nazareti Sanga alisema kuna upungufu wa maafisa shamba na wachache waliopo wamekuwa wakikimbilia kufanya kazi za mifugo kuliko zile za shamba.
Alisema maafisa shamba wamekuwa wakikimbilia kwenye kazi za mifugo kutokana na kupatiwa zawadi na wafungaji na kuwaacha nyuma wakulima.
Mahenge alisema tatizo hilo limekuwepo hata miongoni mwa wakulima wenyewe kwa kutoa kipaumbele kwenye mifugo kuliko kilimo kwa kuwa ni rahisi mfugaji kupiga simu kuwa ng’ombe wake anaumwa kuliko mkulima kupiga simu juu ya matatizo ya mazao yake.
Alisema Brac imelenga kuboresha kipato cha kaya maskini zinazoishi vijijini ambazo ni za wakulima wadogowadogo kupitia mpango wa LEAD unaotekelezwa kwenye mikoa 15 na wilaya 64 ukihusisha mikopo, masoko, uwekezaji na usimamizi wa kilimo cha mahindi na ufugaji wa kuku.
Alisema kati ya watakaonufaika asilimia 65% ni wanawake hasa wa kutoka kaatika maeneo ya vijiji ikiwa ni mkakati kabambe wa kuwakomboa kuondokana na umaskini uliokithiri kwa sasa kwa wananchi.
Alisema mikopo itatolewa kwa wakulima wadogodogo ambayo ni kati ya sh50,000 na 350,000 wakati kwa wakulima wakubwa ni kati ya sh8m na 50m ambayo itakuwa na ruzuku ya 40% kwa wakulima wakubwa.
Alisema LEAD itasaidia kuboresha uzalishaji wa kuku wa kienyeji, uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na mahindi pia kuboresha uzalishaji wa mbegu bora na kilimo cha kisasa na mawasiliano baina ya maafisa ugani na wakulima wadogo wadogo ili kuongeza uzalishaji kwa kutumia kilimo.
 Kwa upande wake mkulima kutoka tarafa ya pawaga John Mkude alisemaa wamekuwa wakipata adha kubwa katika maeneo yao hali inayopelekea kupata mazao madogo kutokana na kukosa watu wa kuwapa ushauri kwa ajili ya kuendesha kilomo cha faida
Mkude alisema kuwa itakuwa jambo la busara serekali kuongeza maafisa ugani katika tarafa zao na kuwataka maafisa ugani kuiga mfano Afisa kilomo na mifigo Faustina Muhagama wa tarafa ya Kalenga kwaa kufanya kazi kwa bidi nakuishi eneo la kazi ili kuwahudumia wakulima na wafugaji tofauti na wengine wanaofanya kazi kalenga lakini wanaishi mijini

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More