Tuesday, October 31, 2017

MWENYEKITI (CWT) MUFINDI OBI KIMBALE SERIKALI LIPENI MADENI YA WALIMU KWANZA

 Mwenyekiti chama cha walimu wa Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi Obi Kimbale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Baadhi ya walimu waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda,Mufindi

Chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimeitaka serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kutatua changamoto za walimu ili kukuza na kuboresha sekta ya elimu ambayo ndio kiungo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho mwenyekiti wilaya ya Mufindi Obi Kimbale aliitaka serkali kulipa madeni wanayoidaiwa na walimu ili kuboresha maisha ya walimu ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.

“Walimu tunadai madeni ya malimbikikizi ya mishahara,madaraja tatizo kubwa na walimu wanadai madeni ya likizo hivyo walimu wanakuwa hawana morali ya kufndisha kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa wakati” alisema Kimbale

Kimbale alisema kuwa kutoka mwaka 2016 hadi hii leo walimu wa wilaya ya Mufindi hawajalipwa stahiki zao hivyo kupunguza kasi ya walimu kuwa na wabunifu wakati kuandaa maandalio ya kwenda kuwafundisha wanafunzi ili  wapate elimu bora.

“Serikali ililipa madeni kidogo sana miaka ya nyuma hivyo bado serikali tunaidai pesa nyingi za walimu wa wilaya ya mufindi hivyo naitaka serikali kulipa madeni yote wanayodaiwa na walimu ili kuwaacha walimu wafundishe wakiwa huru kwa kupata stahiki zao zote” alisema Kimbale

Aidha Kimbale aliwaomba walimu kuendelea kuwafundisha wanafunzi kwa moyo wao wote wakati viongozi wao wanavyoshugulikia swala la madeni wanayoidai serikali.

Akijibu hoja hizo mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William alikiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu katika wilaya hiyo na kuahidi kuanza kuzitafutia ufumbuzi.

“Kweli kuna changamoto za miundombinu,stahikiza walimu na tatizo la upungufu wa walimu serikali inayafanyia kazi hayo yote ili kumfanya mwalimu afanye kazi yake kwa weledi unaotakiwa” alisema William

William aliwataka walimu kudhibiti nidhamu ya walimu na wanafunzi ili kumaliza tatizo utoro mashuleni ambao umekuwa ukisababisha wanafunzi wengi kushindwa kufaulu masoma yao na wengine kupata mimba wakiwa na umri mdogo.

“Mufindi kumekuwa na tatizo la wanafunzi wengi kupata mimba wakiwa na umri mdogo kutokana na utoro hivyo nawataka walimu kudhibiti nidhamu mashuleni na kupunguza hizi mimba za utotoni” alisema William
Aidha William aliwataka walimu kuacha kufanya siasa mashuleni ili kuboresha elimu kwa kizazi wanachokifundisha na kupata matunda mema hapo baadae.

MBUNGE KABATI ACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE YA MSINGI IGELEKE

IMG-20171028-WA0045
MBUNGE wa viti maalum, Ritta Kabati akizungumza na kamati ya shule na wazazi ambao hawapo pichani juu ya ukarabati wa shule ya Msingi Igeleke ambayo inakabiliwa na uchakavu wa majengo na miundo mbinu mibovu hali inayohatarisha afya na usalama wa wanafunzi na walimu.
Picha na Denis Mlowe
………………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
 
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa,Iringa kwa tiketi ya CCM Ritta Kabati amechangia kiasi cha mifuko ya saruji 100 na siling’ibodi 100 kwa shule ya msingi Igeleke iliyoko katika manispaa ya Iringa kutokana na  uchakavu wa majengo ya shule hiyo.
 
Akizungumza na kamati ya shule na wazazi wa shule hiyo mara baada ya kufanya ukaguzi wa miundo mbinu ya shule hiyo mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo kuwa miundo mbinu mibovu ambayo inawafanya wanafunzi kukaa kwa wasi wasi.
 
 
Alisema kuwa shule hiyo licha ya kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani majengo yake hayaendani kabisa na hali halisi ya ufaulu wa wanafunzi hivyo kwa kushirikiana na wazazi ambao wamechangia vitu mbalimbali ukarabati wa shule hiyo utaanza jumamosi wiki hii.
 
Alisema kuwa majengo ya shule hiyo yamechakaa hali ambayo inahatarisha afya na uhai wa wananfunzi kwa kuwa vumbi kwa chini hivyo kutokana na hilo atakahakikisha shule zote chakavu zinafanyiwa ukarabati uendane na ubora unaotakiwa.
 
“ Nimetembelea shule nyingi mkoani kwetu hasa za msingi kuweza kuangalia miundo mbinu na majengo yake kwa kweli hali inatisha na majengo mengi yamekuwa chakavu hivyo nitajitahidi kwa kushirikiana na wadau wa elimu kuweza kukarabati yaendane na hali ya sasa ya kuwa bora zaidi” alisema
 
Kabati aliongeza kuwa shule ya Igeleke ni moja ya shule zinazofanya vizuri katika mitihani yake lakini imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wanafunzi wanasoma katika mazingira magumu na kudumisha elimu ya wanafunzi hao waendelee kuongoza mkoani hapa.
 
Hadi sasa Kabati amekwisha fanya ukarabati kwa shule za msingi za Azimio, Kihesa,Mtwivira na shule ya Kibwabwa ambazo alizitembelea na kubaini uchakavu mkubwa wa majengo na miundo mbinu mibaya na shule nyingine alizoahidi kuzifanyia ukarabati ni shule ya msingi Gangilonga.

KIKOSI KAZI SEKTA YA ARDHI CHAKUTANA KUREJEA MWONGOZO NA KUKAMILISHA MKAKATI,MOROGORO

Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta kuu za matumizi ya Ardhi na Asasi za Kiraia wamekutana kwa ajili kuendelea kurejea Mwongozo wa ushirikishaji katika kupanga mipango ya matumizi ya Ardhi pamoja na kukamilisha kazi ya rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo kuutafsiri kwa lugha ya kiswahili.
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi, pamoja na kupongeza kazi nzuri ambayo inafanywa na kikosi kazi, lakini pia lizungumzia swala la mipango miji,upangaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi utakaozingatia mtazamo wa kuipeleka nchi katika Dira ya viwanda na pamoja na swala la mabadiliko ya Tabianchi, ili wananchi wawe tayari kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi kunatakiwa kuwe na mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, Sera na Mawasiliano wa TumeBi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi kazi ya kikosi kazi ya kukamilisha andiko la Mkakati wa changamoto za mato za matumizi ya Ardhi ikiwa ni pamoja na kuandaa mwongozo na kubadili andiko kwa lugha ya kingeleza ili lipate kusomwa na wafadhiri pia wadau wengine.
Afisa Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald Mwakipesile (wa kwanza kulia) akiwapitisha kikozi kazi katika maeneo mbalimbali ya kukamilisha mkakati wa kutatua changamoto za matumizi ya Ardhi nchini.
Afisa Tawala wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bi. Nakivona Rajabu akitoa mrejesho wa kikao kilichofanyika na Mh. William Lukuvi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa anakabidhiwa Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi cha tarehe 14.08.2017 mjini Morogoro.
Wanakikosi kazi wakiwa wanafuatilia mrejesho huo
Wanakikosi kazi wakiwa katika makundi kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja kulibadili andiko la mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi kwa lugha ya kingeleza ili uweze kuja kusomwa na wafadhiri pamoja na wadau wengine mbalimbali.

Bw. Paulo Tarimo  kutoka Wizara ya Kilimo akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Bw. Emmanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo.
Bwana Daniel Ouma(kushoto) Afisa Miradi kutoka TNRF akichangia jambo wakati kikosi kazi kikiendelea na kazi.
Bw. Mbaraka Stambuli kiongozi wa Kipengele cha maendeleo ya kisera na kitaasisi katika programu ya kuwezesha umilikishwaji wa Ardhi, akichangia jambo la maboresho wakati wa kubadilisha andiko katika lugha ya kingeleza.
Bwana Herman Nyanda Afisa wanyama pori (TAWA) mwandamizi katika dawati la ushirikishwaji jamii katika uhifadhi wa wanyama pori akichangia hoja wakati shughuli ya kubadilisha andiko katika lugha ya kingeleza inaendela
Kikosi kazi wakiendelea na kazi

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More