Sunday, November 22, 2015

MGOMBEA UBUNGE LUDEWA DEO NGALAWA AIFUNIKA LUDEWA.

Deo Ngalawa akimkabidhi fomu za ubunge msimamizi wa jimbo la uchaguzi la Ludewa Bw.Wiliam Waziri pembeni ni Mwanasheria wa wilaya ya Ludewa Bw.Chalamila

maandamano ya bodaboda yakiendelea kumuunga mkono Bw.Ngalawa




huu ndio usafiri alioutumia Deo Ngalawa wakati akirudisha fomu ya ubunge






Deo Ngalawa akiwasalimia wananchi kwa kupunga mkono wakati akirudisha fomu ya ubunge
Cledo Filikunjombe ambaye ni mdogo wa hayati Deo Filikunjombe akiwa na gari yake akimuunga mkono Deo Ngalawa katika kuirudisha fomu ya ubunge wa jimbo la Ludewa.







Mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa kupitia chama cha mapinduzi Bw.Deo Ngalawa jana alifunika wilaya ya Ludewa kwa kufanyiwa maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea wakati akirudisha fomu ya ubunge katika ofisi ya tume ya Taifa ya uchaguzi wilayani hapa.


Akiongea na wananchi mara baada ya kuikabidhi fomu hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa Bw.Ngalawa aliwaeleza wananchi kuwa hata waangusha katika uongozi wake kwani atafuata nyayo za aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo hayati Deo Filikunjombe.


Bw.Ngalawa alisema kuwa katika uongozi wake atafanya kazi zaidi katika sekta ya elimu,Afya,Miundombinu na kukuza uchumi kwani bado wananchi wa wilaya ya Ludewa wanahali ngumu kiuchumi hivyo imepelekea vijana wengi kukimbilia miji mingine na kuhaimia huko.


“Sita waangusha katika suala zima la maendeleo ni ukweli usiopingika  kuwa hayati Filikunjombe aliyapeleka maendeleo kwa kasi kubwa hivyo hata mimi nitafanya hivyo na nitajitahidi kufanya kazi mara mbili yake ili wilaya ya Ludewa na wananchi wake wafurahie matunda ya uhuru wa taifa letu”,alisema Ngalawa.


Alisema kuwa maendeleo hayaletwi na mtu mmoja hivyo wananchi wanapaswa kushiriki ipasavyo katika kuleta maendeleo na kujiletea maendele pia aliwataka vijana,akina mama na wazee kuanzisha vikundi mbalimbali ambavyo vitaweza kukopesheka na kujiinua kiuchumi.


Aidha katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano Mbosa alisema kuwa katika kata 26  jimbo la Ludewa CCM imeshinda kata 25 na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimeshinda kata moja ya Madope hivyo huo ni ushindi mkubwa kwa ccm ambao utaleta matokeo mazuri yasiyo na shaka katika ubunge.


Bw.Mbosa alisema mgombea wa ubunge kwa jimbo la Ludewa anauzika hivyo aliwataka wagombea wengine ambao kura hazikutosha katika mchakato wa kura za maoni kumuunga mkono Bw.Ngalawa katika kampeni zake ambazo zinatarajia kuanza hivi karibuni.


Akikabidhiwa fomu za ubunge na mgombea wa ccm msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ludewa  ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hii Bw.William Waziri aliwataka wagombea kufanya kampeni za kistaarabu ambazo zitajenga heshima kwa wananchi wa jimbo hili.


Bw.Waziri alisema kuwa jimbo la uchaguzi la Ludewa lina wagombea wawili wa nafasi ya ubunge ambao ni Deo Ngalawa kutoka chama cha mapinduzi na Bathromeo Mkinga(Msambichaka) kutoka chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) hivyo kila mgombea anapaswa  kuwaeleza wafuasi wake kanuni za uchaguzi ili amani iweze kutawala.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More