Friday, November 20, 2015

Bomoabomoa Dar Yakumba makanisa, Waumini Waangua Kilio Hadharani

Bomoabomoa ya nyumba na makazi zilizojengwa kinyume cha sheria iliendelea jana katika Wilaya ya Kinondoni, ambapo Kanisa la Anglikana pamoja na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mivumoni zimekumbwa na bomoabomoa hiyo.

Shughuli hiyo ya ubomoaji ilianza jana saa 12 asubuhi katika eneo la Mbezi Jogoo, ambapo nyumba 25, makanisa mawili, fremu mbili za biashara na sehemu ya kuoshea magari zilibomolewa.

Mbali na kanisa la Aglikana,  kanisa jingine ni la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Bunju B, nyumba ya mwanajeshi ambaye amerejea kutoka  kulinda amani Darfur Sudan nayo imebomolewa na kusababisha mke wa mwanajeshi huyo kuzirai.

Mbezi Jogoo
Bomoabomoa ilifanyika karibu na kiwanda cha Interchick ambapo nyumba moja na eneo la kuoshea magari vilibomolewa.
 
Aidha bomoabomoa iliendelea eneo la Basihaya Bunju ambapo  nyumba 19 zilibomolewa pamoja na fremu mbili za biashara ya mbao inayomilikiwa na Ally Khamis.
 
Mwenyekiti wa Mtaa wa Basihaya, Kata ya Bunju, Malinus Ndule alisema nyumba hizo tayari wananchi wake walilipwa fidia ikiwemo viwanja katika eneo la Mabwepande.

Waumini waangua vilio
Waumini wa Kanisa la Tanzania Assemmbles of God (TAG) walifika eneo la tukio wakiwa na Biblia wakiomba na kuangua kilio huku wakisema Mungu ana mpango nao.

Akizungumzia tathimini ya ubomoaji huo, Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya alisema shughuli hiyo inaendelea vyema na ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua vigogo waliojenga kinyume na sheria.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More