Friday, November 27, 2015

MEYA WA MANISPAA YA IRINGA KUJULIKANA DISEMBER 2



Chama Cha Demokrasia na maendeleo Chadema jimbo la Iringa mjini kimedai kimekamilisha mchakato wa umchagua diwani atakayegombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Iringa na Naibu wake na sasa wahusika hao wanasubiri  Baraka kutoka kamati kuu ya Chadema Taifa baada ya kuwasilisha majina yao.

 Katika uchaguzi huo madiwani watatu walijitokeza kuwania nafasi ya Meya wa Manispaa na wengine watatu walijitokeza kuwania nafasi ya Naibu Meya wa Manispaa hiyo ambayohaijawahi niuongozw ana Chama cha Upinzani tangu ulipoasisiwa mwaka 1992.

 Waliojitokeza kuwania nafasi ya Meya ni Diwani wa kata  ya Isakalilo Alex Kimbe ambeya aliongoza kwenye kura za maoni, wengine ni Baraka Kimata kutoka kata ya  Kitwiru na Franki Nyalusi kutoka kata ya Mivinjeni.

 Madiwani waliojitokeza kuwania nafasi ya Naibu Meya ni Joseph Ryata kutoka kata ya Kwakilosa  ambaye  diyealiyeongoza kwenye kura za maoni akifuatiwa na  EvaritoMtuti na Dadi Igogo.

Akizungumzia mchakato huo mbele ya  waandishi wa habari mjini hapa jana Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema TaifaMchungaji Peter Msigwa alisema kazi ya chama Jimbo ilikuwa kupendekeza jina lamgombea na kuliwasilisha kwenye kamati kuu ambayoi ndiye yenye

 “Sisi kazi yetu ilikuwa  kupendekeza majina ya wagombea wa  nafasi ya Meya na Naibuwake,madiwani  kazi hiyo tumeikamilisha na majina tumeshayatuma makao makuu  ingawa wapo tuliowapa asilimia kubwa bado kazi ya kuchagua mgombea inafanywa na kamati kuu”alisema Msigwa.

Huku akisita kutaja kiasi cha asimilia walizotoa kwa wagombea hao,Msigwa alimtaja diwani wa kata ya Isakalilo Kimbe kuwa ndiye mgombea aliyepata asilimia nyingi kuliko wagombea wakingine na hivyo katika nafasi mkubw aya  kuteuliwa na chama kuwa mgombea wa nafasi ya Meya.

 Kimbe alifuatiwa na  Kimata ni diwani kata ya Kitwiru ba katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa wa Iringa na na Nyalusi ambaye ni diwani kata ya Mivinjeni na mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Iringa mjini.

Katika nafasi ya Naibu Meya Ryata aliongoza kwenye kurea za maoni na ksha kufuatiwa na Mtitu pamoja na Dadi Igogo.

 Kwenye mkutano huo ambao viongozi wa Madiwani wa Chadema pia walitambulishwa mbele ya waandishi wa habari,viongozi hao waliambatana na madiwani wote 21 kutoka katika chama chao ambao madiwani 14 ni wa
kuchaguliwa sita kati yao wakuteuliwa na wawili ni wabunge.

Msigwa alitumia mkutano huo kuwaomba wakazi wa Manispaa ya Iringa kujitokez kwa wingi Desemba 2 mwaka huu siku watakayoapishwa madiwani hao na kuongez akuwa hiyo itakuwa ni siku ya kihstoria kwa madiwani kuchagua Meya wa kuongoza Halmashaurin ya Iringa wakitokjea upinzani.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Jimbo la Iringa mjini Frank Nyalusi alikiri kuwa mchakato ndani ya chama hicho uliambatana na mgogoro lkakini akasisitiz akuwa suala hilo limekwisha.

 “Unapofanyika uchaguzio unaohusisha watu Zaidi ya watatu lazima kila mtu anakuw ana kundei lake,kwa sasa makundi hayo yamemalizika na madiwani wote tumebaki wamoja tunajipanga kumteua Meya kutoka katika chama chetu”alisema Nyalusi.

Awali katibu wa Chama hicho Jimbo la Iringa Suzan Mgonokulima alisema chama hicho kimefuata taratibu na miongozi ya chama kuwapata wagombea na kwamba kazi iliyobaki ni kusubiri uamuzi wa kamati kuu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More