Friday, November 27, 2015

VIBAKA WAONGEZEKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKU MKOANI IRINGA

Jeshi la polisi mkoani iringa limewatahadharisha wananchi kuwa makini ili kuepukana na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
 




Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa iringa RPC RAMADHANI ATHUMANI MUNGI alipokuwa akizingumza na nuru fm juu ya kuzuia unyang’anyi wa kutumia silaha kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.


Aidha kamanda MUNGI ameyataja na kuyatahadharisha baadhi ya maeneo kuwa makini na vitendo vya unyang’anyi wa kutumia silaha ni pamoja na kwenye mabenki, na maduka ya kubadilisha fedha.

Akizungumzia namna ya kuepukana na matukio hayo kamanda mungi amesema kuwa ni pamoja na wafanyabiashara kupeleke benki na kuacha kukaa nazo majumbani mwao.
 
hapohapo imeelezwa kuwa uelewa mdogo wa sheria katika jamii umetajwa kuwa sababu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa RPC RAMADHANI ATHUMANI MUNGI alipokuwa akizungumza na nuru fm mara baada ya kutokea kwa tukio la wananchi kumuu mtu kwa kosa la kuiba spika ya redio.

Aidha ameitaja sababu nyingine ya wananchi kujichukulia sheria mkononi ni pamoja na wananchi kutokuwa uhakika wa kujua mtu wanaempiga ndiye muhusika.

Katika hatua nyingine kamanda mungi amewataka wananchi kutoa taarifa katika jeshi la polisi na vyombo vya usalama wanapoona matukio kama hayo ili kuendana na sheria ya nchi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More