Monday, November 2, 2015

MBWANA SAMATA SASA AELEKEZA NGUVU ZAKE KUISAIDA TAIFA STARS KUING'OA ALGERIA

MSHAMBULIAJI mahiri wa Tanzania anayekipiga katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mbwana Samata, ameahidi kuiua Algeria itakapokwaana na Taifa Stars. Mbwana na pacha wake kiuchezaji, Thomas Ulimwengu wamewasihi Watanzania kuwaunga mkono kwa dua na kujitokeza kwa wingi uwanjani. 

“Mimi nawaomba Watanzania watuunge mkono, waiamini timu yao, tunaweza kuifunga Algeria na hata timu nyingine kubwa za Afrika, cha msingi tuwe na mshikamano,” alisema Samata  Alisema uwezekano wa kuifunga Algeria upo kwa kuwa katika soka kinachotakiwa ni mandalizi na mshikamano, ambapo alitolea mfano timu bora kama Uholanzi kuachwa katika mbio za kufuzu Euro 2016. 

Stars itaikaribisha Algeria ambao ni vinara wa ubora wa soka barani Afrika, Novemba 14, mwaka huu na zitarudiana Novemba 17 nchini Algeria ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya makundi kusaka tiketi ya Kombe la Dunia 2018 litakalopigwa nchini Russia

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More