Thursday, November 5, 2015

Jimbo la marehemu Filikunjombe limepata mgombea….

Tanzania bado iko kwenye majonzi  baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo Haule Filikunjombe pamoja na Rubani Captain William Silaa na watu wengine wawili Egid Nkwera pamoja na Cassablanca Haule waliofariki kwenye ajali ya Helikopta kwenye mbuga ya Selous.

Najua kuna watu walikuwa na maswali juu ya atakayewaongoza wakazi wa Ludewa, sasa leo Novemba 5, 2015 mke wa marehemu Deo Filikunjombe ‘ Saraha’ ameyaandika maneno haya kupitia akaunti yake ya instagram kuhusiana aliyeteuliwa kugombea jimbo la Ludewa.

Nawaombeni wana ludewa wote kwa heshima nawaomba niwaambie ukweli kuwa huyu ndie anayeweza kuvaa viatu vya mume wangu mpendwa kwani mara nyingi amewahi kumchangia kaka yake ada za watoto tuliokuwa tunawasomesha huko ludewa naombeni msidanyike na maneno ya hao wagombea wengine mbona leo ndo wamekuja ludewa walikuwa wapi kujakuleta maendeleo mpaka iwe baada ya deo kufariki kati ya wagombea wote hakuna rafiki wa mume wangu’ – Saraha

‘hata mmoja tena kwa macho yangu nimewaona wakipewa misaada walete Ludewa na hawakufikisha na mara nyingi amelalamika na kuwaomba jamani tupeleke maendeleo nyumbani hakuna aliesikia hata mmoja ndo maana hawana nyumba ya kufikia matokeo yake wanawaomba kura ilingali hata hawana pakufikia wamefikia nyumba ya kulala wageni mkitaka kumwona mbunge mta mkuta wapi tuwemakini Deo amefanya mengi mpeni mdogo wake amalizie aliyoahidi asanteni sana wanaludewa niwaganili sana mdalikhe sana ccm hoyeeeeeee👍👍👍👍chagua ccm chagua Philipo filikunjombe hapa kazi tu’ – Saraha

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More