Wednesday, April 13, 2016

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA WANAWAKE KATIKA UONGOZI UKUMBI WA MIKUTANO WA MWALIMU JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu akihutubia wakati akifungua kongamano la wanawake katika uongozi lililofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Uongozi.
 Taswira ya meza kuu katika kongamano hilo.
  Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu (kushoto) na Spika wa Bunge mstaafu wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Mwanasheria Vicky Mandali akichangia jambo kwenye kongamano hilo.

 Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Lusindi akitoa mchango wake katika kongamano hilo.
 Balozi Mwanaidi Maajar, akichangia jambo kwenye kongamano la wanawake katika uongozi lililofunguliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Uongozi.
 Wadau  wakiwa kwenye kongamano hilo lililowajumuisha wanawake wenye taaluma mbalimbali na viongozi.
 Kongamano likiendelea.
 Taswira kwenye kongamano hilo.
Usikivu wa mada kwenye kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI mbalimbali nchini wametakiwa kutumia uwezo na nyazifa zao ili kuwahamasisha na kuwawezesha wanawake wapate maendeleo.

Mwito huo umetolewa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu wakati akifungua kongamano la wanawake katika uongozi lilifanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi ambalo liliandaliwa na Taasisi ya Uongozi.

"Kila mtu na hasa sisi viongozi katika uwezo wetu na nyadhifa zetu tuzingatie kutumia kila nafasi kwenye ofisi zetu kuwahamasisha na kuwawezesha wanawake" alisema Suluhu.

Suluhu alisema wanawake wanapaswa kupewa sauti katika maamuzi mbalimbali na kama tunavyosema ukimuelimisha mwanamke unakuwa umeelimisha taifa zima.

Alisema usemi huo wa wahenga ukaonekane katika ushiriki wao na aina ya maamuzi watakayoyafanya na kuyasimamia ili yalete tija kwao na taifa kwa ujumla.

Samia alisema kwamba kongamano hilo lenye maudhui ya wanawake katika uongozi lina lengo la kuwapatia nafasi wanawake ambao wako kwenye uongozi na wale wanaokusudia kuwa viongozi katika maeneo mbalimbali ikiwemo serikali, kwenye vyama vya soasa, sekta binafsi, vyama visivyo vya kiserikali, kushirikiana katika kutambua mazingira wezeshi katika kumpatia mwanamke fursa ya kufikia nafasi ya uongozi.

Alisema Tanzania uwakilishi wa wanawake ndani ya chombo cha uwakilishi na maamuzi ambacho ni Bunge ni asilimia 30 lakini wamejiwekea lengo la kufikisha asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More