Monday, April 25, 2016

MADAKTARI BINGWA WA MAGONJWA SUGU NA MAGONJWA MBALIMBALI WANATARAJIA KUTUA MKOANI IRINGA

 
Dokta Abdull Maulid Abdull akimpima Miwani ya kuonea Mwananchi Chale Muumin Fumu mkaazi wa Kijiji cha Matemwe Tunda ngaa katika matibabu yalio fanyika skuli ya matemwe mkoa wa Kaskazini unguja.Dokta Rajab Mohd(picha kutoka maktaba)

NA RAYMOND MINJA IRINGA

MADAKTARI Bingwa wa Magonjwa sugu na magonjwa mbalimbali wanatarajia kutua mkoani Iringa kwa ajili ya kutoa huduma  kwa  wagonjwa ambao walishindwa kusafiri kutoka mikoani  kufata huduma hizo katika hospitali kubwa .

Kuja kwa madaktari hao bigwa kunaelezwa kuwa  kutawarahisishia wananchi  kupata huduma kwa garama ndogo tofauti na wagonjwa hao wangesafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo .

Hayo yamesemwa Meneja wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Iringa Dk. Mohamed Kilolile wakati akizungumza  na Mtanzania ofisini kwake juzi kuhusu ujio wa madaktari bingwa ikiwa ni lengo la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwapeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni mwa nchi kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa kina  na kutibu wanachama wa Bima ya Afya pamoja na wagonjwa wengine wa kawaida.

Dk Kilolile alisema kuwa lengo la madaktari hao kutoa huduma hiyo mkoani Iringa na mikoa ya jirani ni kuweza kuwarahisishia wananchi wa kuweza kupima na kujua afya zao na kupunguza gharama kwa wale ambao hawana kadi za bima ya afya ambapo zoezi hilo litafanyika pia mkoa wa Njombe.

Alisema kuwa huduma ya madaktari bingwa zitafanyika  katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kuanzia April 25 hadi 30 na kuwataka wananchi mbalimbali kujitokeza kuweza kupata huduma ya matibabu kwa wale wenye kadi za bima ya afya na wasio na kadi watatibiwa kwa gharama  zinazotozwa hospitali hapo .

“ Mfuko wa bima ya afya  kwa wajali watumishi na wateja wa bima ya afya huwa unaandaa mipango ya kuboresha huduma zake hivyo mwaka huu madaktari bingwa watakuwepo mkoani Iringa kwa lengo kila mtu aweze kujielewa afya yake kwani endapo utapojua afya yako baada ya kufanya vipimo itakuwa rahisi kupata matibabu ambayo tayari ushaletewa hapohapo karibu bila kuifuata sehemu za mbali “Alisema

Alisema kuwa madaktari hao ni mabingwa katika wa maradhi mbali mbali yakiwemo magonjwa ya nje na ndani ,kisukari, usingizi, kinywa na meno magonjwa ya Moyo, huduma za  mama na mtoto na magojwa  mengineyo.

Hata hivyo Kiholile aliwataka  wazazina walezi kuwaingiza watoto wao katika  mpango mpya wa huduma za matibabu kwa watoto chini ya umri wa miaka (18) unajulikana kwa jina la  “Toto Afya Kadi” kwa lengo la kuwawezesha watoto kuwa na uhakika wakupata matibabu wakati wote.

 Kilolile alisema kuwa katika jitihada za kufikia lengo la afya bora kwa watu wote ,Mfuko wa bima ya afya (NHIF)umetanua wigo wake na sasa unasajili watoto katika huduma zake ili nao wapate huduma zao
pindi wanapokubwa na matatizo ya ugonjwa.

Alisema kuwa mara nyingi wazazi wamekuwa wakitumia garama kubwa katika kuwahudumia watoto wao katika swala la afya na wakati mwingine kukosa fedha kwa ajili ya kuwatibu watoto  wao jambo linoloweza wakati mwingine  kusababisha kupoteza maisha  lakini kwa kupitia huduma ya
toto afya kadi mtoto atatibiwa kwa mwaka mzima kwa shilingi 50,400/= sehemu yoyote atakayopenda mwanachama

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More