Friday, April 8, 2016

Jeshi La Polisi Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam Limefanikiwa Kuwakamata Watu 63 Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi

Jeshi  la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63 wanaodhaniwa kuwa  majambazi wa kutumia silaha katika operesheni endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.

Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita  kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.

Katika tukio jingine  kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kukamata silaha sita  aina ya SMG  moja ,Short gun pump action tatu na Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Amesema silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.

“Tunaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo. Hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea kufanyika, jeshi lipo imara na tutapambana nao,”alisema Sirro.

Ameongeza kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimefichwa na kufunikwa kwa taulo zikiwa na maandishi ya Collessium Fitness Club  moja ikiwa na namba A 6777013 iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L 691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa kwenye magazine.

Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.
 
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa  na uchunguzi unaendelea kufanyika

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More