Thursday, November 5, 2015

Vijana wa (UVCCM ) mkoa wa Iringa limepanga kuandaa la kuwakutanisha makada mbalimbali wa chama cha mapinduzi (CCM)

JUMUIYA ya Vijana wa (UVCCM ) mkoa wa Iringa  limepanga kuandaa la  kuwakutanisha makada mbalimbali wa chama cha mapinduzi (CCM) ambao hawakuhudhuria sherehe za kuapisha kwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Magufuli zinazotarajia kufanyika leo jijini Dar es Salaam.

C hama hicho  mkoani hapa   kimeandaa kongomano litakalofanyika kama sehemu ya kushiriki maadhimisho ya kuapishwa kwa Rais mteuli wa awamu ya tano Dk John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa Kaimu katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Elisha Mwampashi amesema tukio la ushindi wa CCM kwa ngazi ya urais na sherehe za kuapishwa kwake ni jambo la furaha na la kihistoria kwa utawala wa Tanzania wa kupokezana vijiti kwa amani.

 Mwampashi amesema baadhi ya viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa na wilaya walisafiri kwenda Jijini Dar es Salaam kuhudhuria sherehe hizo za kuapishwa kwa rais wakiwawakilisha wananchi wa Iringa na kuongeza wale waliobaki ndio watajumuika pamoja kwenye kongamano hilo.

Akuzungumzia tukio la kusitishwa kwa uchaguzi wa Zanziba Mwampashi amewataka wananchi wa visiwa hivyo kuwa watulivu na wenye subira katika kipindi hiki cha mpito wakati taratibu zikifanyika za kutatua tatizo lilipo kwa sasa.

Alisema Zanziba inasheria na katiba yake hivyo ni muhimu mambo yote yanayohusu visiwa hivyo yakafanyika kwa kufuata misingi ya sheria na katiba ya Zanziba huku akisisitiza kuwa suala la muhimu ni kwa wananchi hao kudumisha amani na utulivu iliyodumu tangu uhuru ,muungano na hadi sasa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More