Thursday, November 16, 2017

MBOWE AICHARUKIA SERIKALI YA CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mheshimiwa Freeman Mbowe amesema hawatakubali kuona Rais Magufuli akizuia uhuru wa demokrasia kwa kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa kwa sababu hana mamlaka hayo kikatiba.

Mbowe amesema Chadema imejengwa kwa maumivu makubwa sana na wanawake na wanaume kujitoa mhanga zaidi ya miaka 25 sasa na Chama hicho kimeonyesha kuwa na sura ya kitaifa kwani mpaka sasa Chadema ina wabunge toka mikoa yote Tanzania.

Mbowe ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa Kampeni za udiwani katika kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa jioni ya leo

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More