Wednesday, November 29, 2017

RITTA KABATI AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI YA IRINGA GIRLS

 MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi  CCM Ritta Kabati akikabidhi mifuko ya sumenti kwa mwalimu wa shule ya Iringa Girls akiwa sambamba na diwani wa Kata ya Nduli Bashir Mtove
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi  CCM Ritta Kabati akikabidhi mifuko ya sumenti kwa wanafunzi wa shule ya Iringa Girls akiwa sambamba na diwani wa Kata ya Nduli Bashir Mtove

Na Fredy Mgunda,Iringa. 

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati amechangia kiasi cha mifuko ya saruji 50 kwa shule ya sekondari ya Iringa Girls iliyoko katika manispaa ya Iringa kutokana na uhaba wa baadhi ya majengo ya shule hiyo.

Akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iringa Girls Kabati alisema kuwa ameamua kujitolea kutoka kwenye posho yake kuhakikisha elimu kwa wanafunzi wa shule zilizopo mkoani Iringa wanasoma na wanapa elimu iliyo bora kutokana na ubora wa miundombinu iliyopo.

“ Nimetembelea shule nyingi mkoani kwetu hasa za msingi kuweza kuangalia miundo mbinu na majengo yake kwa kweli hali inatisha na majengo mengi yamekuwa chakavu hivyo nitajitahidi kwa kushirikiana na wadau wa elimu kuweza kukarabati yaendane na hali ya sasa ya kuwa bora zaidi” alisema Kabati

Hadi sasa Kabati amekwisha fanya ukarabati kwa shule za msingi za Azimio, Kihesa,Mtwivira na shule ya Kibwabwa ambazo alizitembelea na kubaini uchakavu mkubwa wa majengo na miundo mbinu mibaya na shule nyingine alizoahidi kuzifanyia ukarabati ni shule ya msingi Gangilonga.

Kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo Bazila Kondo alimushukuru mbunge huyo kwa msaada wake alioutoa kwa kuwa utawasidia kujenga majengo ya mabweni ya wanafunzi hapa ambayo imekuwa ikiwasumbua na kuongeza mlundikano kwa wanafunzi mabwenini.

“Tulikuwa tunasherekea jubilee ya shule hivyo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Joyce Ndalichako  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe  Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamhuri David na Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela,Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa hivyo mbunge kabati ametimiza ahadi yake”alisema Kondo

Kondo alisema lengo la shule ni kuhakikisha wanajenga jingo la bweni jipya la wanafunzi pamoja na kujenga vyoo viwili vya wanafunzi wenye mahitaji maalum

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More