Friday, November 10, 2017

IIED NA HAKI MADINI YAWAJENGEA UWEZO WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI MKOANI GEITA.

Baadhi ya wadau wa sekta ya madini Nchini na wachimbaji wadogo wakiwa kwenye mjadala ambao umeandaliwa na Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na  maendeleo(IIED )wakishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali  hakimadini,Kampuni ya ushauri(MTL) na kituo cha kimataifa cha utafiti wa mistu(CIFOR) na kufanyika kwenye ukumbi wa hotel ya alphendo Mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha mgeni Rasmi kwaajili ya kuzungumza na wadau wa sekta ya madini wakati wa Mkutano wa majadiliano juu ya swala la uchimbaji  madini kwa wachimbaji wadogo.

Kamishina msaidizi wa madini anayeshughulikia wachimbaji wadogo ambaye pia ni mgeni rasimi , Mhandisi David Mulabwa akifungua majadiliano hayo mapema hii leo kwenye ukumbi wa mikutano wa alphendo hotel.

Bw,Fitsum Weldegiorgis ambaye anatoka Taasisi ya kimataifa ya Mazingirana na  maendeleo(IIED ) akielezea namna ambavyo taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli pamoja na sekta ya madini Nchini.

Rebecca Burton ambaye anatoka taasisi ya Tiffany akizungumza namba ambavyo taasisi yao inafanya kazi wakati wa Mkutano wa majadiliano.

Mtafiti  wa kampuni ya ushauri  Dkt,Willson Mtagwaba,akibainisha changamoto ambazo wamekutana nazo wakati wakifanya tafiti kwa wachimbaji wadogo.<!--[if gte mso 9]>

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More