Wednesday, November 29, 2017

KENANI KIHONGOSI MWENYEKITI MPYA WA UVCCM MKOANI IRINGA

Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi akitangazwa na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo uliofanyika katika manispaa ya Iringa.
 katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marco Mbaga akimpongeza Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi kwa ushindi mkubwa aliupata na kuwa kiongozi wa jumuiya hiyo.
 Viongozi mbalimbali walimpongeza mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi kwa kupata kura za kishindo na kuonyesha kuwa anakubalika na vijana wa chama hicho.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Hatimaye umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umempata mwenyekiti mpya bwana Kenani Kihongosi alichaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kurudisha matumaini mapya ya kuanza safari ya kuijenga CCM mpya kwa vijana wa mkoa huu wa Iringa.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye msingi katika uchaguzi huo Kihongosi alisema kuwa atahakikisha jumuiya zote za umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi zinarudi na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha wanapata wanachama wapya ambao itakuja kuwa nguzo ya chama hicho hapo baadae.

“Sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyokusubiwa na kuhakikisha chama kinapata matokeo chanya kutoka kwetu vijana hivyo naomba mniunge mkono kuhikikisha tunakuwa wamoja” alisema Kihongosi

Kihongosi aliwataka vijana kufanya kazi na kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga CCM na Tanzania mpya.

“Sisi ndio vijana ambao tunatakiwa kuonyesha mfano kwa kufanya kazi na kuonyesha wapinzani wa mkoa wa Iringa kuwa sasa kuna UVCCM ambavyo inania ya kuhaikisha inaumaliza upinzani uliopo hapa mkoana na CCM ikachukua jimbo la Iringa Mjini” alisema Kihongosi

Aidha Kihongosi aliwashukuru wanachama wote wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoani Iringa kwa kumpigia kura za kuwa na imani naye na kuhakikisha anakuwa mwenyekiti wa umoja huo.

“Bila kura zenu mimi nisingekuwa mwenyekiti hivyo naona nitoe shukrani zangu za dhati kwenu wote kwa kunipa ushindi huu niweze kuwaongoza hivyo naomba mnipe ushirikiano wa kutosha ili tujenge UVCCM mpya hapa mkoani Iringa” alisema Kihongosi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More