Friday, November 10, 2017

CHADEMA : KITWIRU MKATAENI KIGEUGEU BARAKA KIMATA

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kampeni za chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mtaa wa Uyole B manispa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa

WANANCHI wa kata ya Kitwiru manispaa ya Iringa wametakakiwa kutomchakugua mgombe wa chama cha mapinduzi CCM bwana Baraka Kimata kwa kuwa ni kigeugeu kwa kuwa hana hoja za kueta maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.
Kimata hafai kuwa kiongozi katika kata hii kwa ajili amekuwa akiwageuka wananchi kwa ajili ya faida yake na sio kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata ya Kitwiru hivyo hapaswi kabisa kuchaguliwa.

“CHADEMA imewataka wananchi wakumbuke kuwa mtu anayekubali kununuliwa ipo siku atakuja kuwauza wananchi wa kata ya Kitwiru hivyo mnatakiwa kuwa makini siku ya uchaguzi  tarehe 26 msimpe kura hata moja.”

Hayo yasemwa wakati wa kuomba kura kwa wananchi wa mtaa wa Uyole B katika kata ya Kitwiru wakati CHADEMA kimemnadi mgombea wake udiwani kata ya Kitwiru Iringa Mjini kikisema hana njaa, anawania nafasi hiyo kwa lengo moja tu la kuwatumikia wananchi wa kata hiyo.

Chademaimemsimamisha Bahati Chengula katika uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 26, mwaka huu na kuongeza kuwa mgombea wetu hana njaa ya kununulika hivyo huyu ndio mtu sahihi kuwa diwani katika kata hii.

“Huyu ni mgombea mwenye dhamira ya dhati ya kuwapigania wananchi wa kata hii, hajaja kutafuta fedha,” alisema Kamanda Mbuma wakati akimpigia debe katika mtaa wa Uyole B.

Aidha chama hicho kimesema hakisombi watu kwa ajili ya kwenda kwenye mikutano yake inayoendelea katika mitaa mbalimbali ya kata hiyo kwakuwa kinataka ujumbe wake ufike kwa wapiga kura halisi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More