Monday, November 20, 2017

MSIGWA : BAHATI CHENGULA ANATOSHA KUWA DIWANI WA KATA YA KITWIRU

 Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msingwa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwaomba wananchi kumpigia kura diwani wa chadema Bahati Chegula 
 Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msingwa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akifurahia jambo na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za kuwania nafasi ya kumpata diwani mpya wa kata hiyo

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msingwa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) amewaomba wananchi wa kata ya Kitwiru kumchagua mgombea wa chama hicho Bahati Chengula kuwa diwani wa kata hiyo kwa kuwa anafaa kuwa kiongozi wa kata hiyo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara wa kumnadi Chengula uliofanyika katika mtaa wa Kitwiru Stand,Msigwa alisema kuwa mgombea wa chama hicho anaweza kuwaletea maendeleo kuliko mgombea mwingine ambaye ni kigeugeu.

“Kwasasa kata ya Kitwiru inahitaji kiongozi makini ambaye atakuwa sambamba na wananchi wake,na ukiangalia kwa umakini mkubwa utandua kuwa mgombea wa chama chetu anasifa zote za kuwa diwani wa kata hii hivyo naomba wananchi msipoteze wakati bali mnatakiwa kuhakikisha Chengula anakuwa Diwani” alisema Msigwa

Msigwa alisema kuwa mgombea wao Chegula anania thabiti ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo tofauti  na Baraka Kimata ambaye anataka madaraka ya juu na sio kuwatumikia wananchi wa kata yake hivyo wananchi mnapaswa kuwa makini.

“Kwa bahati mbaya sana watu wakipewa uongozi wanaona waondio wanaakili sana kuliko watu wengi hivyo naombeni mmpigie kula nyingi mgombea wetu Bahati Chegula kwa anaweza kufanikiwa kutatua changamoto za wanakitwiru” alisema Msigwa

Aidha Msigwa alisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kilimuibua Baraka Kimata kutoka kuwa kushona nguo na kuwa wanasiasa hivi leo anakizalilisha chama kwa uroho wa madaraka hivyo wananchi naombeni kura zote ziende kwa Chengula.

“Tulimuokota Ipogolo akiwa  anashona nguo na alikuwa hajui chochote kuhusu siasa na tulimpandisha jukwaani hadi leo kawa mwanasiasa na anaanza kukidhalili chama cha CHADEMA kwa ajili ya mambo yake” alisema Msigwa

Msigwa aliongeza kwa kusema kuwa wananchi wa Kitwiru wanapaswa kumpigania mgombea wa chama chao kwa kuwa yupo katika mikono salama na yenye nia ya kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa kata ya Kitwiru.

Akijinadi wakati wa kampeni Mgombea udiwani wa CHADEMA Bahati Chengula amewaomba wananchi wa Kitwiru kumpigia kura siku ya tarehe 26 mwezi huu kwa kuwa anastahili kuwa diwani wa kata hiyo.

“Nawaombeni kaeni kwenye foleni na minipigie kuwa kwa kuweka alama ya tiki kwenye box la kura ili niweze kuwatumikia na kuwaleta maendeleo ambayo mlikuwa mnayasubili kwa muda mrefu na muwaambie na wengine kuwa Chengula ndio diwani wa kata ya kitwiru” alisema Chengula

Chengula aliwataka wananchi kufanya siasa za kistaarabu maana kumekuwa na taarifa kuwa CHADEMA tunafanya siasa chafu hivyo naomba mzipuuze taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuhakikisha mnanichagua siku ya tarehe 26.

“Jamani naombeni tuendelee kuomba kama tulivyoanza mwanzo hadi mwisho kwa kuwa tukitumia hekima ya mwenyezi mungu tutashinda kwa kishindo na tusifanye vurugu zozte zile” alisema Chengula

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More