Tuesday, November 7, 2017

RITTA KABATI AFANYA UKARABATI WA SHULE YA MSINGI IGEREKE MANISPAA YA IRINGA

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa amebeba ndoo ilikuwa na mchanga akiupeleka kwa mafundi walikuwa wanaendelea na ujenzi wa kukarabati chumba cha wanafunzi wa shule ya Msingi Igereke
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa amejitwisha ndoo ilikuwa na mchanga akiupeleka kwa mafundi walikuwa wanaendelea na ujenzi wa kukarabati chumba cha wanafunzi wa shule ya Msingi Igereke
 Hili ndio moja ya madarasa yalikuwa yanakarabatiwa katika shule ya msingi Igereke kwa kutumia nguvu za mbunge Ritta Kabati pamoja na ushirikiano na wananchi wanaoizunguka shule hiyo


Na Fredy Mgunda,Iringa.
 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ameendelea kutimiza ahadi ya kukarabati miundombinu ya shule za msingi manispaa ya Iringa kwa lengo la kuboresha elimu kwa wanafunzi ili kuja kuleta maendeleo ya nchi hapo baadae.
 
Akizungumza na blog hii wakati wa ukarabati wa baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Igereke Kabati alisema kuwa ameamua kufanya maendeleo kwa kufanya ukarabati wa shule ili kuhakikisha kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa manispaa ya Iringa kinapanda na kuleta manufaa kwa mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.

“Mimi ni muumini wa kuhakikisha kuwa wanatoto wetu wanasoma katika mazingira rafiki ili waweze kupata elimu iliyobora kwa faida ya maisha yao ya hapo baadae kwa kuwa bila elimu hakuna maendeleo ya uhakika” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa amuamua kufanya shughuli za kijamii ili kuifanya jamii ya watu wa Iringa kuwa na Elimu iliyobora na kuweza kuwa na kizazi ambacho kitakuwa cha kimaendeleo.

"Mimi sipendi kuona watoto wa Iringa wanakuwa wafanyakazi wa kazi za ndani kwa watu kwenye Pesa au wafanyakazi wengi najiuliza tu kwanini ile Iringa ndio chimbuko la wafanyakazi wa kazi za ndani,nitapambana kuhakikisha Iringa inakuwa na wasomi wengi ili kupunguza utegemezi"alisema kabati

Aidha Kabati aliwaomba wananchi na viongozi wa kufanya kazi kwa kujituma ili kwenda sambamba na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Magufuli na kuomba jamii kufanya kazi za kujitolea zaidi kuliko kusubili serikali kuleta maendeleo.

“Mkiwa mnajitolea kama hii leo naamini tukiwa na wananchi na viongozi wengi basi nchi hii itapata maendeleo ya haraka na kwa kasi kutokana na wananchi kufanya kazi kwa nguvu na moyo wa kuinua uchumi” alisema  Kabati

Kabati aliongeza kuwa shule nyingi za hapa nchi zilijengwa miaka mingi iliyopita hivyo nyingi zimechakaa kutokana na kutokarabatiwa kwa wakati hivyo nawaomba viongozi wengi kuwa wabunifu wakati wa kutafuta pesa nyingi za kusaidia kukarabati miundombinu ya shule na maeneo mbalimbali ilimradi kukuza uchumi na kutoa elimu bora.

“Hichi nilichokitoa hii leo ni kidogo sana ila nimefurahishwa na kujituma kwenu katika swala nzima la kusaidia ukarabati wa shule hii ya kigonzile ambayo ilikuwa katika mazingira ya kufungwa kutokana na uchakavu wake” alisema Kabati

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli  ametutuma kufanya kazi kwa wananchi wakawaida kwa kuwa wao ndio wanamahitaji mengi kuliko watu wa kipato cha kati na cha juu hivyo hata mimi nimeamua kufanya kazi za kwasaidia kuleta maendeleo wananchi wengi wa chini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo ndio inafanyiwa ukarabati kwa jitihada za mbunge kabati.

“Mwandishi ukiangalia majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo katika halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi hawaingalii kwa jicho la tatu kitu kinachotupa shida sisi viongozi wa eneo hili lakini tunamshukuru huyu mbunge Kabati” alisema Madembo

Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta viongozi waliotayari kule maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa viongozi.

“Leo hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo
 
Naye mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
 
Nao baadhi ya wananchi wa Kata ya Mkimbizi waliwashuku viongozi wa serikali pamoja na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati kwa Juhudi kubwa za kukarabati shule hiyo ya Igereke kwa kuwa ilikuwa katika wakati mgumu sana.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More