Sunday, November 12, 2017

MH FREEMAN MBOWE KUMNADI MGOMBEA KATA YA KITWIRU TAREHE 16 MWEZI HUU

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) taifa freeman Mbowe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa kata ya Kitwiru utakao fanyika tarehe 26 mwezi huu na ataambatana na wakurugenzi wa uchaguzi kutoka makao makuu ya chama hicho.

Akuzungumza na blog hii Mratibu wa Kampeni Kata ya Kitwiru ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Iringa Mjini (Bavicha), Leonce Marto alisema kuwa mwenyekiti Mbowe atakuja Iringa kwa lengo la kuhakikisha chama cha CHADEMA kinashinda katika chaguzi zote zinazoendelea hapa nchi.
"Huyo ndio viongozi wetu mkubwa hivyo lazima afanye kampeni nchi nzima kuhakikisha wagombea wake wote wanashinda katika chaguzi hizi ndogo zote nchi nzima"alisema Marto
Marto alisema mbali na mwenyewekiti wa chama hicho taifa pia mbunge wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa atakuwepo katika mkutano huo.

Marto aliongeza kuwa mkutano huo utafanyika katika uwanja wa mpira Nyamhanga C walipofanyika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hich.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More