Wednesday, November 29, 2017

KASESELA AMEIPONGEZA SHULE YA SEKONDARI YA BREAD OF LIFE KWA KUTOA ELIMU BORA

 MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ameipongeza shule ya sekondari ya Bread of Life kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo akiwa sambamba na maaskofu wanne ambao nao walifanikiwa kufika katika mahali ya kwanza ya shule hiyo toka kuanzishwa kwake
 MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika maabara ya shule ya sekondari ya Bread of Life akionea ubora wa vifaa vilivyopo katika maabara hiyo
 MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kaseselaakipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bread of Life alipotembelea maabara ya shule hiyo
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kaseselaakipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bread of Life alipotembelea maabara ya shule hiyo

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ameipongeza shule ya sekondari ya Bread of Life kwa kutoa elimu bora kwa wananfunzi wanaosoma katika shule hiyo na kuzitaka shule nyingine kuiga mfano wa uongozi wa shule hiyo wakati wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi. 
 
Akizungumza wakati wa mahali ya kwanza ya shule mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza tangu kuanzwa kwa shule hayo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa amefanikiwa kutembelea shule nyingi lakini amegundua kuwa shule hiyo inakitu cha ziada kinasaidia wanafunzi kufanya vizuri.

“Naomba nichukue furasa hii kuwapongeza walimu na viongozi wa shule hii kwa kutoa elimu bora na pia kuwa na vifaa vya kuwawezesha wanafunzi kusoma masomo yao kwa bila kuwa na bughuza” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa shule hiyo inamaabara bora ambavyo imekamilika vifaa vyote pamoja na kuwa na walimu ambao wanaweledi wa kufundisha wanafunzi wakafundishika.

“Ukishakuwa na walimu wazuri wanafundisha vizuri ni lazima kuzalisha kizazi cha kazi kwa kuwa watakuwa wamepata elimu ya bora kutoka shule bora ya sekondari ya Bread of Life” alisema Kasesela


Aidha Kasesela alisema kuwa kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na ujuzi wowote ule ili kufanikiwa katika maisha yao.

Kasesela alimalizia kwa kuwapa wosia wahitimu kupitia mstari wa biblia wa matayo 4:13, ‘Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako

Kwa upende wa uongozi wa shule ya sekondari ya Bread of Life umeupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuijali vilivyo sekta ya elimu kwa kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanapata elimu bora na kuwa na taifa ambalo linakuwa na wasomi wengi.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha nne shule hiyo mkuu wa shule, Pawde Mwasanje kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi wa shule, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gaville alisema kuwa bila ushirikiano na serikali ya Wilaya ya Iringa, basi shule ya sekondari ya bread of life isingekuwa na mafanikio waliyofikia.

Mkuu wa shule huyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake hivyo anawakaribisha wanafunzi wengine kujiunga na shule hiyo.

Mwasanje alisema kuwa katika mtihani wa kujipima a kidato cha pili, shule hiyo ilishika nafasi ya sita kati ya shule 31 za Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa kwa ufaulu wa asilimia 100.

Mwasanje alisema wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ya kidato chapili walikuwa 19 ambapo wasichana 11 na wavulana 8.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More