Wednesday, November 15, 2017

CHADEMA YAPATA PIGO TENA KATIBU MKUU WA NYASA FRANK MWAISUMBE AHAMIA CCM

Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa kanda ya juu kusini (NYASA) bwana Frank Mwaisumbe  akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchukua uamuzi wa kuhama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha demokrasia na maendeleo chadema nyanda za juu kusini kimepata pigo baada ya aliyewahi kuwa katibu mkuu wa kanda bwana Frank Mwaisumbe  kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM) kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano DR John Pombe Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwaisumbe alisema kuwa Rais wa awamu hii amerudisha hali ya utendaji wa kazi na wananchi wameacha tabia ya kuishi kimazoea

“Hata mkiangalia nyinyi waandishi wa habari mtagundua kuwa saizi wananchi wanafanya kazi kutokana msimamo wa rais wetu kuhimiza kufanya kazi kwa lengo la kukuza kipata cha nchi na mtu mmoja mmoja hata nchi zilizoendelea wananchi wake wanafanya kazi muda wote” alisema Mwaisumbe

Mwaisumbe alisema kuwa maono ya Rais Maguli haikuwa kuwa Rais bali ilikuwa kuhakikisha anafanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kuwaleta maendeleona kuwaondoa katika mfumo tengemezi na kuwapeleka katika mfumo wa kujitegemea.

“Tanzania yetu wananchi wengi tumeishi kwa kuwa wategemezi na swala hilo halina ubishi lakini toka tumempata Rais huyu mambo mengi sana yamebadirika na kuwafanya hata wananchi kuanza kuishi kwa kufanya kazi na kujua nini maana ya kujitegemea” alisema Mwaisumbe

Aidha Mwaisumbe alisema kuwa ameingia CCM kuafanya kazi kama alivyokuwa anafanya kazi wakati akiwa CHADEMA na kufanikiwa kukijenga chama hadi hapa mnapokiona chama hicho nyanda za juu kusini kilikuwa kutokana na mchango wake.

“Nilikabidhiwa chama tukiwa kwenye kikao na chama kilikuwa hakina ofisi hata moja lakini nyie waandishi mashaidi saizi CHADEMA imekuwa huku kusini kutokana na mchango wangu wa hali na mali hivyo naondoka naelekea CCM kufanya kazi nanitafanya kazi kweli” alisema Mwaisumbe

MWAISUMBE alisema kuwa ataendelea kukitumikia chama cha mapinduzi na kukieneza kwa kuwa tayari ameshakuwa mwanachama wa chama hicho na moja ya jukumu la mwanachama ni kuhakikisha unakieneza vilivyo chama ulichopo.

Lakini Mwaisumbe alisema kuwa alichokuwa akikidai hapo awali kwa uongozi wa chama cha mapinduzi kulinda rasilimali za nchi ndio anachokifanya Rais wa awamu ya tano hivyo hawezi kubakia CHADEMA kwa kuwa kinakinzana na ukweli wa mambo anayoyafanya Rais. 

“Zamani nilipiga kelele sana juu ya kulinda raislima za nchi lakini serikali ilikuwa haichulii maanani hivyo nimeona awamu hii serikali ya chama cha mapinduzi imekuwa makini mno na inafanya kazi kwa kujituma kwa kulinda rasilimali za nchi ndio maana nilijiunga na CCM” alisema Mwaisumbe

Mwaisumbe aliwata wapinzani kuacha kuuposha umma kwa kudai kuwa Rais Magufuli ni dikteta hivyo nawaomba waonyeshe kuwa udikteta wa upo katika Nyanja gani.

Hivi tuongee ukweli udikteta upo wapi maana siasa ameruhusu zinafaika kwenye majimbo ya wabunge husika ,sheria ya mitandao ya kijamii ilitungwa kabla yake kuingia madarakani hivyo naomba wapinzani watafute mambo mengi ya kusema Rais lakini sio kumuita Rais Magufuli dikteta” alisema Mwaisumbe

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More