Thursday, November 23, 2017

KATIBU MARCO MBAGA : MBUNGE PETER MSIGWA NI MNAFIKI WANANCHI MKATAENI NA MGOMBEA WAKE

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marco Mbaga akiwahutubia wananchi kwenye moja ya mikutano yake wakati wa kuomba kura kwa mgombea wa chama hicho kata ya Kitwiru Baraka Kimata.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Marco Mbaga amemtaka mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa kurudia mungu kwa kile anachokifanya ni tofauti na kujiita mchungaji kwa kuwa amekuwa akiwadanganya wananchi mambo mengi tofauti na alivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mbaga alisema mchungaji Msigwa amekuwa akiwadanya wananchi kwa mgongo wa kujiita mchungaji hivyo anatakiwa kuwataka radhi wananchi kuwa kusema uongo hadharani kuwa mabalozi wa serikali ya mitaa wa kata ya Kitwiru kuwa wamelipwa shilingi laki tatu.

“Msigwa amewadanganya hadharani wananchi kuwa wamepewa laki tatu kutoka chama cha mapinduzi kitu ambacho sio cha kweli hata hao mabalozi wanalijua kuwa sio kweli hivyo wananchi wa kata ya Kitwiru wanatakiwa kukikataa chama hicho na kumyima kuwa mgombea wao” alisema Mbaga

Mbaga aliwataka wananchi wa kata ya Kitwiru kumjua kuwa walimchagua mtu wa aina gani kwa kuwa amekuwa mpotoshaji wa maswala ya wananchi na kuwachonganisha na baina ya wananchi na wananchi hivyo katika kampeni hizi najua wananchi mmejifunza kuwa msigwa ni mtu wa aina gani

“Huwezi kuwa kiongozi wa kuwachonganisha wananchi badala ya kuwatafutia maendeleo wananchi hivyo mnapaswa kumkata huyu mchungaji feki pamoja na wafuasi wake wote na mnatakiwa kuwanyima kabisa kura mwezi ili iwe fundisho kwake na kwa chama chake kuwa iringa hawanajipya tena” alisema Mbaga

Mawakala wa chama cha mapinduzi wanajua utalatibu wetu hivyo Msigwa ameshindwa kutatua matatizo yaliyopo ndani ya chama chake hivyo anaamua kujificha kwa kukichafua chama cha mapinduzi hivyo anapaswa kujua kuwa amechokwa ndani ya chama chake na nje chama chake kutokana na udikteta anaoufanya kwa viongozi wake pamoja wananchi anaowaongoza” alisema

Aidha Mbaga alisema kuwa chama hicho hakina haja ya kununua wanachama wapya kwa kuwa wanachama wengi kuliko chama chochote hapa nchini.

“Nimesema kuwa chama cha mapinduzi kinawananchama wengi kuliko chama chochote hapa nchini hivyo hatuna haja ya kununua mwananchama yoyote Yule huko ni kutapatapa kwa msigwa tu na ajiandae kushindwa Kitwiru” alisema Mbaga


 Mbaga alisema kuwa kiongozi yoyote Yule wa chama cha mapinduzi akikutwa anafanya kazi ya kununua wanachama wapya atakuwa amejiondoa kwenye chama kwa mjibu wa katiba ya chama cha mapinduzi.

Lakini Mbaga amewataka viongozi wa CHADEMA manispaa ya Iringa waache propaganda ambazo wanaendelea kuzieneza dhidi ya mgombea wa chama cha CCM Baraka Kimata kuna anataka kurudi CHADEMA tena.


“Usiku wa kuamkia juzi wameanza kutengeneza meseji za kumchafua mgombea wetu Baraka Kimata kwa kujifanya kuwa mgombea wetu amerudi CCM jambo ambalo sio la kweli hizo ndio dalili za watu hawa kushindwa katika uchaguzi huu” alisema Mbaga
Hata hivyo makada wa chama cha mapinduzi wameendelea kumuombea kura mgombea wao Baraka Kimata ili awe diwani wa kata ya Kitwiru katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo.

Luciana Mbosa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amekifananisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kilabu kilichoishiwa pombe akisema wateja wake wazuri wameendelea kukikimbia.

Ametoa kauli hiyo baada ya vigogo wake wawili, Lawrance Masha na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha) Patrobas Katambi hii leo kuomba mbele ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kujiunga na CCM sambamba na makada wengine kutoa chama cha ACT wazalendo.

“Kama ilivyokuwa kwa  NCCR Mageuzi, TLP, UDP na vyama vingine vya upinzani kupoteza umaarufu kwa umma na kisha kupotea, anguko hilo sasa linainyemelea Chadema,” alisema katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Kitwiru kupitia CCM, Baraka Kimata.

Naye Kimata aliwaambia wapiga kura wa mtaa wa Uyole mwisho kwamba akiwa Chadema amejifunza mengi yanayokinzana na demokrasia inayohubiriwa majukwaani hatua iliyomfanya ashuke katika basi lao na kupanda basi lenye injini bora.

“CCM ni chama chenye mfumo mzuri, chenye demokrasia ya kweli na ndio maana kimeweza kuongoza nchi kwa miaka yote tangu Uhuru,” alisema.

Kimata alitaja changamoto kubwa mbili zinazoukabili mtaa wa Uyole, maji na umbali wa shule ya msingi akisema atatumia uwezo wake wote kuzishughulikia mara atakapochaguliwa tena kuwa diwani wa kata hiyo.


“Serikali ya CCM ina mipango mizuri ya kutatua kero ya maji, nina hakika suala hilo litafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo lakini pia vijana wetu wanasoma mbali na maeneo haya wanayoishi, kwahiyo nitaanzisha harakati za ujenzi wa shule mpya ili wawe jirani na shule yao,” alisema


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More