Monday, November 20, 2017

BARAKA KIMATA MIMI KIGEUGEU WA MANDELEO NA SIO MNAFIKI KAMA WALE

 Mgombea udiwani wa kata ya Kitwiru kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Baraka Kimata akizungumza na wananchi wa kata ya kitwiru ili apate ridhaa ya kuwa diwani.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa chama hicho ulifanyika katika mtaa wa kitwiru Stand 

Na fredy Mgunda,Iringa.

MGOMBEA udiwani wa kata ya Kitwiru kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Baraka Kimata amekubali tuhuma za wapinzani kuwa kigeugeu ila ni kigeugeu wa maendeleo kwa wananchi wa kata ya Kitwiru na sio kigeugeu kwa kuwageuka wananchi.

Akizungumza kwenye mikutano ya hivi karibuni Kimata alisema kuwa tuhuma anazopwa na wapinzani kuwa nikigeugeu zimekuwa na ukweli kwa sababu aligeuka kutoka chama cha demokrasia na maendeleo na kuahamia CCM kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Kitwiru.

“Siwezi nikakaa mahali ambapo huwezi kutimiza matakwa ya wananchi kwa kuwaletea maendeleo ndio maana niliamua kugeuka na kuhamia upande mwingine ambako naona naweza kupata fursa ya kuwatumikia wananchi wa kata yangu hivyo kweli mimi nikigeugeu ili kigeugeu wa kutafuta maendeleo” alisema Kimata

Kimata aliongeza kuwa chama cha demokraisa na maendeleo kimepoteza mvuto kwa wananchi na kuishiwa hoja za kumnadi mgombea wake ndio maana wamebaki kuniandama kwa kutumia lugha matusi majukwaani.

“CHADEMA saizi hawana jipya kutoka na kuwa wanakataliwa na wananchi kuwa uongo wao hivyo wameanza kutafuta nani mchawi wameshindwa sasa wameanza kunichafua kwa kuniita kigeugeu kitu kinachopelekea wananchi kuendelea kuamini sera zangu chini ya chama cha mapinduzi” alisema Kimata

Kimata alisema kuwa waliwahidio wananchi wa kata ya Kitwiru kuwaletea maendeleo mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2015  lakini hali ilikuwa tofauti ndio maana nikaamua kugeuka kwa kuwa ni haki yake ya msingi kuhakikisha  maendeleo yanapatika katika kata hiyo.

“Nigeukageuka kutokana na kuona chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kinawapeleka wananchi wa kata ya kitwiru shimoni ndio nikaamua kugeuka ili niweze kuwaokoa wananchi wa kata hii kwa kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo” alisema Kimata

Aidha Kimata alisema kuwa hata chama cha mapinduzi kimegeuka kutoka kule kilikokuwa kinaeleka na sasa kimeanza kutengeneza CCM mpya hivyo hata huko nako ni kugeuka geuka hivyo hoja za wapinzani hazina mashiko mzikatae na kumkata hata mgombea wake.

“Jamani wote hapa mashaidi kuwa chama cha mapinduzi kimeanza kugeuka geuka kutokana na kuanza kutengeneza CCM hivyo inatengeneza CCMya kuleta maendeleo kwa wananchi hivyo maendeleo yapo njiani” alisema Kimata

Kimata aliwataka wapinzani wake kutafuta hoja nyingine kwa kuwa hoja ya kigeugeu haina mashiko tena kwa kuwa ameshaijibu na ataendelea kuijibu hadi wakose kitu cha kujibu maana hawana hoja mpya.

“Wameishiwa hoja hawanajipya  na wamezidiwa sana na wanajua kuwa hawawezi kushinda kata hii ya Kitwiru ndio maana wamebaki kininanga mimi badala ya kuongelea hoja zao za kuwashawishi wananchi wawachague” alisema Kimata

Kimata alimalizia kwa kuwaomba wananchi kumpigia kuwa katika uchaguzi wa tarehe 26 ili ashinde kwa kishindo na kuwaacha mbali wapinzani wake ambao wameishiwa hoja .

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More