
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru
fedha zilizopaswa kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru
ambazo zingefanyika tarehe 09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa
barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa
kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.
Tayari
fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa
barabara hapa nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo,
linalopaswa kuanza mara moja
Akizungumza
na Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar
es Salaam, Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka
ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara...