Tuesday, December 26, 2017

WAFUGAJI WAMUANGUKIA NAIBU WAZIRI ABDALLAH ULEGA WAOMBA SHERIA IREKEBISHWE KWANI INAWAACHA MASIKINI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akizungumza na wafugaji wa Ng'ombe kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe wakati alipofika kuwasikiliza kilio chao.

Naibu Waziri akifatilia kero mbalimbali ambazo zimetolewa na Wafugaji ikiwemo kukamatwa kwa Ng'ombe zao lakini hawapewi taarifa ya aina yoyote hata wakipelelkwa mahakamani na matokeo yake Ng'ombe zao zinapotea katika mazingira ambayo yanadaiwa ni ya uonevu.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto Biteko akizungumza na kuelekezea matatizo ambayo yameendelea kuwakumba wafugaji ambao wapo kwenye jimbo analoliongoza ndani ya wilaya ya Bukombe.

Baadhi ya Ng;ombe ambao wamepigwa mnada.

Na,Joel Maduka,Geita

Wafugaji Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita,wamemuomba Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega kuingilia kati manyanyaso ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka kwa  watu wa maliasili ambao wamekuwa wakichukua mifugo yao na mwisho wa siku kupigwa  mnada bila ya kufikisha mahakamani hali ambayo imekuwa ikiwasababishia umasikini.

Imeelezwa kuwa baadhi ya Minada ya Ng’ombe wanaokamatwa katika Mapori ya Hifadhi imekua ikifanyika kinyume na kwa udanganyifu hasa ambapo katika mnada uliofanyika hivi karibuni Wilayani Bukombe imegundulika katika Ng’ombe waliopigwa mnada 1600 kati yao 500 haijulikani ilipo huku kukiwa na malalamiko mengi kutoka kwa Wafugaji.

Akizungumza kwa niaba ya wafugaji Bw,kwa niaba ya wafugaji Bw,Emmanuel Maricholi wanzake amemweleza naibu waziri kuwa wamekuwa wakikutana na shida kubwa pindi mifugo yao inapokamatwa na kwasasa wafugaji wengi wamefilisika kutokana na hali ya mifugo yao kukamatwa na kupigwa mnada bila ya kuwepo kwa maelewano baina yao na watu wa maliasili na kwamba ni vyema wakaitazama kwa makini sheria ambayo inafanyiwa kazi kwa sasa kwani imewafanya kuwa masikini zaidi.
   
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Doto  Biteko alisema ana taarifa ya  baadhi ya Watu wanafaidika na Mnada huo kwa manufaa yao wenyewe lakini pia amewataka Wafugaji kuvuta subiri juu ya mabadiliko ya sheria ambayo yanaendelea kwani ukiangali sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2009 ilikua inatoa adhabu ya vitu vitakavyokamatwa katika Mapori ni kutaifishwa na Marekebisho yameplekwa bungeni na ishasomwa mara moja yenyewe inaondoa adhabu ya kutaifisha na badala yake kuna faini.

Aidha,Mh Doto Biteko ameongeza kuwa anatambua  serikali imeendelea kujishughulisha na watu masikini na kwamba ni lazima wafugaji wakaelimishwa hili wajue sheria na wajue kuyatunza mazingira kabla ya kuendelea kuwahukumu kuwa wanaharibu mazingira na kwamba kuna watu ndani ya idara wamekuwa na tabia ya kukamata mifugo kwaajili ya kujipatia fedha hata kabla ya mnada.

Hata hivyo kwa upande wake Naibu waziri wa mifugo na uvuvi,Abdallah Ulega,amewataka wafugaji kutokukataa tamaa na kusubili hadi pale watakapo kuwa wameweka sheria mpya  huku  akivitaka Vyombo vya Dola kuchunguza tuhuma za uendeshaji wa minada ya Ng'ombe na hatua za haraka zichukuliwe kwa wote ambao wamefanya minada hii kujinufaisha na kuwanyanyasa .

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More