Tuesday, December 5, 2017

BREAKING NEWS!!!!!! ALBERT CHALAMILA NDIO MWENYEKITI CCM MKOA WA IRINGA

 Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila akitoa hotuba yake ya kwanza kuwashukuru wapiga kura mara baada ya kushinda uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa leo akiwashinda wapinzani wake wawili Bw. Evance Balama na Salim Abri ambaye amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC mkoa wa Iringa.
 Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila akitoa hotuba yake ya kwanza kuwashukuru wapiga kura na kuelezea Dira na Mwelekeo wa Uongozi wake mara baada ya kushinda uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa,  katikati ni  Salim Abri ambaye amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa na kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi huo Mh. Januari Makamba.
 Bw. Salim Abri  Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa  katika uchaguzi huo akiwashukuru wapiga kura mara baada ya kutangazwa mshindi  kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi huo Mh. Januari Makamba na kulia ni Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila
 Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila kulia  na Bw. Salim Abri  Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa wakiwashukuru wana CCM mkoa wa Iringa kwa kuwaamini na kuwapa ridhaa ya kukiongoza chama hicho.
 Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila kuli  na Bw. Salim Abri  Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa washindi katika uchaguzi huo.
 Mwenyekiti mpya wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Albert Chalamila na Bw. Salim Abri  Mjumbe mpya wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC mkoa wa Iringa wakiwa wakii.furahi paoja na wapiga kura mara baada ya kutangazwa washind
Salim Abri Asas Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM( NEC) akipongezwa na wanachama mbalimbali wa CCM mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Hatimaye chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa umempata mwenyekiti mpya ndugu Albert Chalamila alichaguliwa kwa kura nyingi za kishindo na kurudisha matumaini mapya ya kuanza safari ya kuijenga CCM mpya kwa vijana wa mkoa huu wa Iringa.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye mshindi katika uchaguzi huo Chalamila alisema kuwa atahakikisha jumuiya zote za chama cha mapinduzi zinarudi na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha wanapata wanachama wapya ambao itakuja kuwa nguzo ya chama hicho hapo baadae.

“Sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa pamoja na kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyokusubiwa na kuhakikisha chama kinapata matokeo chanya kutoka kwetu vijana hivyo naomba mniunge mkono kuhikikisha tunakuwa wamoja” alisema Chalamila

Chalamila aliwataka vijana kufanya kazi na kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuijenga CCM na Tanzania mpya.

“Sisi ndio vijana ambao tunatakiwa kuonyesha mfano kwa kufanya kazi na kuonyesha wapinzani wa mkoa wa Iringa kuwa sasa kuna CCM ambavyo inania ya kuhaikisha inaumaliza upinzani uliopo hapa mkoani na CCM ikachukua jimbo la Iringa Mjini” alisema Chalamila

Aidha Kihongosi aliwashukuru wanachama wote wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoani Iringa kwa kumpigia kura za kuwa na imani naye na kuhakikisha anakuwa mwenyekiti wa umoja huo.

“Bila kura zenu mimi nisingekuwa mwenyekiti hivyo naona nitoe shukrani zangu za dhati kwenu wote kwa kunipa ushindi huu niweze kuwaongoza hivyo naomba mnipe ushirikiano wa kutosha ili tujenge UVCCM mpya hapa mkoani Iringa” alisema Kihongosi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More