Monday, December 11, 2017

CHADEMA YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kutekeleza ahadi za mgombea wake Urais  Ndg. Edward Lowassa kwa kuwapa msamaha wasanii Nguza Viking na mwanae Johnson Nguza (Papii Kocha), waliofungwa kifungo cha maisha.
Msamaha huo wa Rais Magufuli kwa wafungwa hao na wengine zaidi ya 60 umetolewa leo kwenye sherehe za Uhuru zilizoadhimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma.
Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari inaeleza kuwa, Chadema inampongeza Rais Magufuli kwa ujasiri wa kuendelea kutekeleza baadhi ya ahadi zilizotolewa na Chama hicho kupitia Mgombea wa Urais wake Mhe. Edward Lowassa, wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
Aidha, imeeleza kuwa, pongeza hizo wamezitoa baada ya Rais Magufuli kuhutubia sherehe za siku ya Uhuru wa Tanganyika ambapo ametoa msamaha kwa wafungwa wa kifungo cha maisha Ndg. Nguza Vicking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha).
Ilieleza kuwa, kutokanana kitendo alichokifanya leo Rais Magufuli kwa kutumia ibara ya 45 ya Katiba ya nchi kama ambavyo mgombea wa urais aliahidi iwapo CHADEMA ingeshinda uchaguzi , kushika dola na kuongoza Serikali, chama kingetoa wito kwa serikali kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa sheria za nchi, hususan kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya (DPP) kwa utaratibu wa *Nolle Prosqui*, iondoe nia ya kuendelea kuwashtaki, Masheikh wa Zanzibar wanaoshtakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Tanzania Bara pamoja na Mahabusu na watuhumiwa wa makosa ya mitandao.
Pia watuhumiwa na mahabusu wa makosa ya kisiasa, ikiwemo kesi za uchochezi zinazohusisha kumkosoa Rais Magufuli, kuikosoa serikali yake na chama chake au tuhuma zinazotokana na kutekelezwa shughuli halali za kisiasa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchini, ikiwemo maandamano, mikutano ya hadhara na vikao vya ndani.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More