Tuesday, December 12, 2017

CAMFED: HALMASHAURI KILOLO NA IRINGA ENDELEZENI MIRADI YA KILIMO

 Baadhi ya viongozi waliohudhuria katika kikao cha mrejesho mradi wa kilimo endelevu yahoo ambao ni Marcus Nyagawa mratibu camfed Iringa,Donard Mshani mkrugenzi wilaya ya iringa,Neema Msemwa mratibu camfed Kilolo,Asnath Ujengo mratibu camfed Mufindi.
Baadhi ya washiriki walioshiki katika kiakao cha mrejesho wa mradi wa kilimo endelevu

Na Adelphina Kutika

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kilolo na Iringa zimetakiwa kuendeleza mradi wa kilimo endelevu uliokuwa ukifadhiliwa na shirika la Campein Female Education (CAMFED) chini ya dona yahoo katika wilaya hizo ili kufikia malengo yaliyotarajiwa.
 
Wito huo umetolewa na kaimu mkurugenzi wilaya ya Iringa Donard Mshani katika kikao cha tathimini ya mradi wa kilimo endelevu baada ya mradi huo kufikia kikomo mwezi huu ambao ulikuwa na lengo la kuhakikisha upatikanaji wa chakula mashuleni ili kuongeza ufaulu katika shule.

“Iringa na killolo zimeteuliwa katika mradi huu kilimo endelevu na mradi wenyewe utatekelezwa na wasichana waliomaliza kidato cha nne (agricultural champion) ambao tunaamini kuwa watautekeleza ipasavyo” alisema Mshani

Mshani alisema kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa kasi kubwa ili kuwa na chakula cha ziada ambacho kitatumika kwenye shule ambazo zinauhitaji mkubwa wa chakula na kulipongeza shirika kwa kuchagua fungu jema ambalo litakuwa na faida kwa taifa.

“Naomba kutoa angalizo kwa wasichana waliopata elimu hii wanapaswa kuitumia vizuri ili ianze kuwasaidia wenyewe na jamii kwa ujumla hapo ndipo tutakapo ona faida ya elimu waliyoipata kutoka katika shirka hili” alisema Mshani

Aidha Mshani amelipongeza   shirika la Camfed   kwakutoa elimu ya kilimo kwa vikundi 206 vya wazazi vilivyopo katika wilaya ya iringa na kilolo jambo ambalo limesaidia kuongeza ajira kwa vijana waliokuwa wanawezesha katika vikundi 

Kwa upande wake mratibu wa shirika la Camfed wilaya ya Iringa Marcus Nyagawa alisema kuwa ukomo wa mradi huo sio chanzo cha vikundi hivyo kufa kwani ipo mikakati ambayo wameiweka kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kwa kuzidi kutoa elimu na wasimamizi kuongeza juhudi za kutembelea vikundi hivyo.

“Serikali imetuahidi kuwa mara baada ya mradi huu kuisha watakuwa wanaufatilia vikundi kama vinafanya kazi ipasavyo hivyo imani yangu kuwa vikundi hivi haviwezi kufa kwa kuwa serikali inamikakati madhubuti ya kuviendeleza” alisema Nyagawa

Naye afisa maendeleo kata ya kising’a Anna Baraka ameomba mashirika mengine kuiga mfano wa shirika la camfed kwa kuwasaidia watoto wanaoishi mazingira magumu.

“Nashukuru hata serikali ya wilaya imetambua kazi iliyofanywa na shirika hili hivyo kwangu naona kama ni shirika namba moja ambalo linafanya vizuri zaidi katika wilaya hii” alisema Baraka

Baraka alisema kuwa kazi iliyofanywa na shirika la CAMFED ilitakiwa kufanywa na serikali lakini waisaidia serikali kutokanana ufinyu wa bajeti isinge weza kufanya hivyo naomba mashirika mengine kuiga mfano kutoka shirika hili.
 

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More