Tuesday, December 12, 2017

VIWANDA VIDOGO VIDOGO VITATUOKOA “RITHA KABATI”

Mbunge viti maalumu ccm mkoa wa Iringa Mh Ritha Kabati amewapongeza wananchi  wa iringa waishio dar  kwa kuanzisha kikundi cha maendeleo  kitakacho endana na kasi ya serikali  awamu ya 5 ya Tanzania ya viwanda
Mbunge viti maalumu iringa Mh. Ritha Kabati akiwahutubia wana kikundi cha Mkon’gano
Amewapongeza wakati wa uzinduzi kikundi cha Mkon’gano  uliofanyika Majumba sita wilaya ya Ilala jijini dar es salaam na kuwapongeza kwa hatua hiyo waliyoifikia ikiwa ni pamoja na risara iliyoandaliwa na kikundi hicho kwa jiri ya siku ya hiyo maalumu.
“kiukweli nimefurahishwa sana na umoja huu kwani tunaamini umoja ni nguvu yenye mawazo ya pamoja kuweza kupata maendeleo yetu binafsi na taifa letu kwa ujumla” amesema Kabati
Mbunge viti maalumu iringa Mh. Ritha Kabati katika picha ya pamoja na wanakundi wa Mkon’gano
Pia amesema upo uwezekano wa kuaanzisha kiwanda cha usindikaji wa ulanzi kutokana na malengo ya kikundi hichoo ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo huku akisisitiza juu ya wamiliki wa vikundi kuvisajiri ili kupata mikopo na uwezeshwaji unaotolewa na serikari kwa vikundi vilivosajiriwa kisheria
“kutokana na marengo yenu ya kuanzisha viwanda mimi nashauri tuanzishe kiwanda chetu cha usindikaji wa ulanzi pale iringa kwani ni kinywaji kinachopendwa na watu wengi na pia tutatekereza sera ya Tanzani ya viwanda  na vilevile serikari itatuwezesha kupata nguvu itakayo tusaidia kupata soko ndani na je ya nchi yetu.
Mbunge viti maalumu Iringa  Mh. Ritha Kabati

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More