Monday, December 11, 2017

MBARONI KWAKUMKATA MWENZIE KOROMEO

Serengeti. Mtuhumiwa anayedaiwa kuingia kininja ndani ya gesti bubu na kumkata koromeo mwanaume aliyekuwa na mke wake kisha kutoroka katika kijiji cha Tamukeri wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amenaswa.
Mtuhumiwa Simioni Mturi(50) alitenda unyama huo oktoba 3 mwaka huu majira ya usiku baada ya kuingia gesti bubu kwa kupitia darini na kumkata kichwani Paul Chacha (24)Mkazi wa kijiji cha Nyansurura wilaya hapa na baada ya kuanguka akamchinga mithiri ya mbuzi, kisha akamkata kifundo cha mguu mkewe Bhoke Simion(36)na kutoroka.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Mang’era Magesa amesema mtuhumiwa amekamatwa desemba 10 majira ya sita mchana mwaka huo muda mfupi baada ya kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
“Baada ya kutenda tukio hilo alitoroka na amekuwa anaishi kwa kujifichaficha, tuliweka mtego baada ya kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha, amekabidhiwa Polisi kwa ajili ya hatua za kisheria,” amesema.
Polisi wilayani hapa wamekiri kumshikilia mtuhumiwa na kuwa taratibu za kiuchunguzi zikikamilika atafikishwa mbele ya Sheria.
Kwa mjibu wa majeruhi Paul na Bhoke walikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na siku ya tukio walikuwa ndani ya gest bubu hapo kijijni na kushambuliwa.
“Tukiwa ndani mlango wa chumba tulichokuwa uligongwa na hatukufungua,ghafla mtuhumiwa akaingia chumbani kupitia darini akiwa na panga na kuanza kumkata mke wake kifundo cha mguu kisha akanishambulia,nilizinduka baada ya siku mbili nikiwa hospitali Teule ya Nyerere wilaya ya Serengeti,” alisema Paul.
Hata hivyo Bhoke ambaye ni mke wa mtuhumiwa alisema, siku ya tukio Mme wake aliaga anaenda msibani kijiji tofauti na hakujua nani alitoa siri hiyo na kuwavamia na baada ya kuwa kata akiamini Paul amekufa alichukua sh 80,000 alizokuwa nazo huyo mwanamke na kutoroka.
Majeruhi baada ya kutoka hospitali hawajaonekana Polisi kutoa maelezo kwa kile kinachodaiwa hofu ya kuhojiwa kwa kukamatwa ugoni.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More