Monday, December 18, 2017

Mahakama Kuu yamuachia huru Sheikh Issa Ponda

Mahakama Kuu ya Tanzania imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchihi, Sheikh Issa Ponda katika rufaa iliyokatwa na Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama ya Morogoro iliyokuwa imemuachia huru.

Mahakama chini ya Jaji, Johnson Mkasimongwa ambaye ameeleza kuwa anakubaliana na uamuzi wa Mahakama ya Morogoro ya kumuachia huru Sheikh Ponda katika kesi ya kutoa lugha ya uchochezi.

Jaji Mkasimongwa amesema Mahakama ya Morogoro haikukosea kumuachia huru Sheikh Ponda na yeye anakubaliana na uamuzi huo, hivyo amechukua uamuzi wa kumuachia huru.

Akitolea maelezo juu ya maamuzi hayo, Jaji Mkasimongwa amefafanua  kwa kusema kuwa upande Jamhuri haikupaswa kumshtaki Sheikh Ponda kwa kosa lile la kuvunja amri ya Mahakama ya Kisutu bali ilitakiwa wamrudishe katika Mahakama hiyo ili imchukulie hatua zaidi.

Sheikh Ponda alishtakiwa kwa tuhuma za uchochezi ambapo mnamo August 10, 2013, August 10, 2013, alidaiwa kutoa kauli za kichochezi kwa waumini wa kiislam ambapo moja ya kauli zake alisema kwamba (Waislam) wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA, ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More