Wednesday, December 13, 2017

WADAU ICHANGIENI TIMU YA MUFINDI UNITED ILI IWEZE KUPANDA LIGI KUU

 Kocha mkuu wa timu ya Mufindi United akiwa makini wakati wa kuiongoza timu ya Mufindi United kwenye mechi dhidi ya Mbeya Kwanza iliyochezwa katika uwanja wa Wambi katika mji mdogo wa Mafinga
Hii ilikuwa mechi ya ligi daraja la kwanza iliyochezwa siku za nyuma baina ya Mufindi United dhidi ya Mbeya Kwanza, na Mufindi United waliovaa jezi rangi ya machungwa

Na Fredy Mgunda, Iringa

TIMU ya Mpira ya Mufindi united zamani kurugezi Fc wameomba wadau na wapenda mpira Mkoani Iringa kuichangia timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza mwaka wa 2017/2018 ili iweze kufanikiwa kuingia ligi kuu msimu ujao.
Akizungumza na blog hii wadau wa timu hiyo walisema kuwa lengo la timu nikuhakikisha msimu huu timu inapanda kutoka daraja la kwanza hadi ligi kuu ndio maana timu tumeirudisha kwa wananchi.
"Tukuwa ligi daraja la kwanza kwa takribani miaka mitano sasa hatujawahi kupanda ndio maana mwaka huu tumeamua kubadilisha jina timu na kuirudisha kwa wananchi ili kuwa karibu na kuweza kuisaidia katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ya timu hivyo naomba wananchi waipokee hii timu kama ya kwao" alisema walisema wadau
Aidha wadu waliongeza kuwa timu ya Mufindi united inatakuwa inachezea mechi zake katika uwanja wa wambi uliopo Mafinga Mjini  hivyo wanaomba wadau wa soka mkoa wote wa Iringa kuanza kuiunga mkono timu ili kupata timu mbili zitakazo kuwa ligi kuu.
Tunavimba vyombo vya habari kuwasaidia kufikisha kikamilifu habari za timu hiyo kwa kuwa sasa ipo mikononi kwa wananchi wa Mufindi na mkoa mzima wa Iringa.
"Nyie waandishi wa habari unaushawishi mkubwa sana kwa wananchi na wadau wa Mpira wa miguu hivyo tunaomba msaada wenu kufikisha kilio chetu kwa wananchi na wadau wa Mpira wa Mkoa wa Iringa waliopo ndani na nje ya Mkoa

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More