Thursday, December 10, 2015

Wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) mtawi ya chuo kikuku cha mkwawa wamejitokeza kufanya usafi katika hospital ya rufaa ya iringa


 Wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) mtawi ya chuo kikuku cha mkwawa wakiwa eneo la mochwari katika hospitari ya rufaa ya iringa.



Wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) mtawi ya chuo kikuku cha mkwawa wamejitokeza kufanya usafi katika hospital ya rufaa ya iringa kwa lengo la kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dr john pombe magufuli. 

Wakizungumza wakati wakiwa wanafanya usafi katika eneo hilo wamesemakuwa wameamua kufanya usafi katika hospital hiyo kwa kuwa ndio hospital inayohudumia wananchi wengi kuliko hospitali nyingine zilizopo mkoani hapa.
 
KHALID ISSA ABUDALA katibu kata wa kata ya mkwawa wa chama cha mapinduzi (CCM) amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa lengo la kuwaonyesha wananchi na wafanyakazi wa hospital hiyo kuwa iringa kuwa safi inawezekana kutokana na kauli moja tu aliyoitoa rais imekuwa gumzo kila kona hivyo wananchi wanatakiwa kufanya usafi kila mara na usafi uwe jadi yao.

“Angalia hapa leo hospitali kama hii ya rufaa uchafu wote huu unatoka hapa kama wanagekuwa wanafanya usafi kila siku na kuona usafi ni sehemu ya maisha yao tusingeona hali hii na pia tusinge pata wagonjwa wa magonjwa ya milipuko naomba wananchi wezangu zoezi hili liwe endelevu”alisema khalid abudala 

wamesema ni aibu wananchi kukumbushwa kufanya usafi na rais wakati huo ni wajibu wa kila mwananchi na kuongeza kuwa wanampongeza rais wa awamu ya tano  kwa kasi yake anayoendana nayo sasa kwa inawafanya watanzania waanze kuiamini serikali yao tofauti na ilivyo kuwa hapo awali.
 
SAIDI RAMADHANI KAZANDA amewataka wananchi kuendeleza juhudi za rais kwa kuwa wasafi kila siku na kuafanya usafi kila mara ili nchi hii isikumbwe na magonjwa ya milipuko na kuongeza kuwa serikali ya manispaa ya iringa inatakiwa kutunga sheria ndogondogo za usafi.

“Hapa iringa hatuna kabisa sheria za usafi kwa utaona wananchi wanatupa takataka hovyo huku viongozi wa mji huu wakiwa kimya kwa namna hiyo hatuwezi kuwa na mji msafi hata siku moj,ukienda pale stand watu wanakojoa na kujisaidia hovyo lakini hawachukuliwi hatua yoyote ile “alisema saidi kazanda

ZINDUNA KASUMU amewaomba wananchi kuendeleza kufanya usafi kwa kuwa ndio jadi ya mtazania hata ukikumbuka hapo zamani wakati mwalimu nyerere akiwa hai alikuwa akisisitiza usafi hivyo ujio wa rais huyu wa awamu ya tano john magufuli naanza kufananisha na marehem waziri mkuu Edward molinge sokoine kwa uchapaji kazi wake.
 
“Leo nimemuana rais huyu akizama kwenye matope kufanya usafi huku akiwa na sura ya furaha kujumuika na wananchi wakati wa kufanya kazi hiyo ni ishara tosha kumlinganisha na marehemu mwalimu nyerere kwani alikuwa anafanya kazi pamoja na wananchi wake”. alisema zinduna kasumu

Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wamewapongeza wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM)  kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa wamejituma kufanya usafi kwenye mahodi na nje ya hodi hasa wanaume walikuwa wanadeki huku kwenye mahodi hicho ni kitendo cha kujivunia kutoka kwako.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More