Monday, December 21, 2015

HAKUNA TENA MNADA ENEO LA MASHINE TATU MANISPAA YA IRINGA

 
alex kimbe meya na naibu  meya joseph lyata
  
zile ndoto za wafanyabiasha wadogowadogo kufanya mnada katika eneo la mashine tatu bado halina ufumbuzi kutoka na eneo hilo kugeuzwa kuwa eneo la kushushia na kupakia abiria wa daldala za kutoka kihesa kuelekea zizi la ng’ombe na isakalilo.
 Hivyo tunaweza kusema kuwa eneo hilo sasa haliwezi kutumika tena kwa kuweka mnada kwa kuwa muda mwingi patakuwa panatumika kwa shuguli za daladala.
Wakizungumza na blog hii baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo wamesema kuwa wamewachagua madiwani wengi wa chadema pamoja  mbunge na kuwapa halmashauri lakini hawaoni dalili zozote zile za kuwasaidia wananchi kupewa kibali maalumu cha kufanya mnada katika eneo hilo la mashine tatu angalau mara moja kwa wiki.

“Angalia mwandishi wahabari wameingia tu madarakani  wametusahau tuliowaweka hapo maana hatuoni juhudi wala hawatupi majibu yoyote yale juu ya lini tunaanza kufanya mnada katika eneo” walisema wananchi 

Aidha wananchi hao wamesema kuwa eneo hilo limegeuzwa kuwa vituo vya daladala hivyo nafasi ya kufanya mnada katika eneo hilo ni gumu mno kutokana na wingi wa daladala ambazo zimehamishiwa katika eneo hilo.

Kwa upande wake naibu meya JOSEPH LYATA amesema kuwa wapo kwenye mchakato wa kulitafutia ufumbuzi kwa kuangalia mpangilio wa mji kwa ofisi ya mipango miji ili kujua eneo hilo linatumika kwa nini.

“Ziwezi kuamka asubuhi  nikawaruhusu wafanyabiasha waanze kufanyabiasha katika eneo hilo mimi sio mungu kila kitu kinapangwa na mipango miji kwa hiyo tunaanda mpango sahihi wa maalumu kwa kuwanufaisha wananchi katika eneo hilo” alisema LYATA

Lakini LYATA amesema kwa sasa wapo kwenye vikao vya kulitafutia ufumbuzi wa eneo hilo na mambo mengine.

“Tunaomba wananchi wawe na subira wakati tunatafuta njia mbadala ya lini wanaanza kufanya biashara na akinani wanatakiwa kufanya biashara sio kila mfanyabiashara atauruhusiwa kufanya biashara katia eneo hilo”alisema LYATA.

kwa sasa eneo hilo linatumika kushushia abiria na kupakia abiria wa  daladala zitokazo kihesa kuelekea isakalilo na zizi la ng'ombe,hapo sasa wananchi na wafanyabiashara ilatakiwa kutafuta njia nyingine ya kufanya biashara kwa sasa

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More