Wednesday, December 23, 2015

UWT MKOA WA IRINGA WAMTAKA RAIS DK. JOHN MAGUFULI- KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA MAFISADI



 
 Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa Tanzania (UWT), Mkoa wa Iringa, Zainab Mwamwindi
UMOJA wa Wanawake wa chama cha mapinduzi UWT mkoa wa Iringa, umeuomba  uongozi wa rais wa awamu ya tano dk. John Magufuli- kuendeleza mapambano, kwa kuibua yale yote yaliyofichika,  zoezi linalofahamika kama ‘Utumbuaji wa majipu” kwa madai kuwa nao UWT wanaziunga mkono jitihada hizo zinazoendele.


 Hayo yamezungumzwa na Zainabu Mwamwindi mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT  Mkoa wa Iringa, wakati akinamama wa umoja huo – wakikabidhi misaada mbalimbali ya kijamii kwa wagonjwa wa Kituo cha afya cha Idodi.

 Bi - Mwamwindi amesema mpango wa “Utumbuaji majipu” licha kuwa na tija kwa wananchi, pia unakinaimarika chama cha mapinduzi -tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya uongozi wa Dr.John Magufuli.

Rose Tweve  mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa, anasema Mpango wa utumbuaji Majipu umelenga kuinua hali ya uchumi na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu na afya, huku  Mwajemi Balagama katibu wa UWT mkoa wa Iringa akisema  jambo hilo la Utumbuaji Majipu ni jema na linapaswa kuungwa mkono na kila mwenye utashi- huku akiwasisitiza wananchi juu ya suala la uimarishaji wa afya.

 Akinamama hao wa UWT mkoa wa Iringa wametoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika kituo cha afya cha Idodi -zikiwemo Sabuni, Mafuta, Miswaki, dawa za kusuguklia meno nk, misaada iliyoambatana na shughuli ya usafi, kwa kufagia mazingira ya kituo hicho cha afya cha Idodi –zoezi lililoambatana na upandaji wa miti katika shamba la UWT lililopo Tungamalenga.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More