Friday, December 4, 2015

GARI YA MAGAZETI YA MWANANCHI IMEUWA WAWILI NA KUJERUHI SITA

Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine sita kujeruhiwa, mmoja vibaya baada ya gari lililokuwa likisafirisha magazeti ya mwananchi kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa  na Mbeya  kupata ajali eneo la mlima kitonga barabara kuu ya Dar-es-Salaam-Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 11 alfajiri wakati garia hili lilipogonga gari aina ya roli iliyokuwsa imefunga tela kwa nyuma.

“Leo imetoka ajali mbaya sana hapa Iringa,ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Haice iliyokuwa imebeba magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communication LTD,gari hilo lilipata ajali baada ya kuganga lori lenye tela kwa nyuma’alisema Mungi na kuongeza:

“Dereva wa gari  hilo lililopata ajali alitaka kulipita loli ambalo nalo lilikuwa linaelekea Mbeya,mara baada ya kutaka kulipita aliona gari jingine likija mbele yake na ndipo alipoamua kurudi upande wake na kugonga loli hilo kwa nyuma”alisema.

Kamanda Mungi akiwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Eliud Ogwasa (40) na Godfrey Owino (34) wote wakazi wa mkazi  Dar es Salaam.
Mungi aliwataka walijeruhiwa kuwa ni Baraka Shitindi (32) ambaye hali yake ni mbaya na Kevin Shitindi (30) wakazi wa Mbozi Mkoani Mbeya na Herold Shitindi (25) mkazi wa Morogoro.

Wengine ni  Zabroin Izote (29) mkazi wa mbeya Joseph Kayani (37) mkazi wa Mafinga mkoani Iringa. 

“Kamanda Mungi aliwasa madereva kuwa makini na kuendesha gari kwa kuzingatian sheria za barabarani na pia kuepuka mwendo kasi ili kuepuka ajali zinazoweza kuwapoteea maisha wao pamoja  na abria wao

Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Alfred Mwakalebela alisema wamepokea maiti mbili ambazo zimehifadhi kwenye chumba cha kuhifadhia miti hospitalini hapo.

Dkt. Mwakalebela alisema pia wamepokea majeruhi wanne ambao wameumia maeneo mbalimbali mwilini ikiwemo kuvunjika mguu na mmoja ana hali mbaya zaidi ambaye haweza kuzungumza.

.
Majeruhi Kevin Shitindi  ambaye ameumia mkono na kifuani alisema walitoka Dar es Salaam saa sita usiku wakiwa 10 kwenye gari hiyo na walipofika Morogoro saa nane watu wawili walishuka.

Baraka Shitindi amevunjika taya la chini na eneo la kichwani na hali yake ni mbaya wakati Izote amevunjika mguu wa kushoto na Kayani alipata mshtuko.

Majeruhi Kayani na Lisote walisema hiace hiyo ilikuwa inakwenda kasi na wakati ajali inatokea wao walikuwa wamelala walichosikia ni kishindo na baadaye kuona madereva wamekufa papo hapo.

Mwakilishi wa Mwananchi anayeshughulikia usambazaji Iringa, Alex Kadeha alisema ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa gari hiyo kukwepa kugongana uso kwa uso na gari nyingine iliyokuwa inakuja mbele yao wakati wakilipita lori.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More