Wednesday, December 2, 2015

MATUKIO YA UALIFU YAENDELEA KUTOKEA IRINGA KWA KASI

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Jophrey Mhongole (37) amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika kisha mwili wake kuwekwa chini nyuma ya gari lake lenye namba za usajili T850ACC aina ya Toyota mark II.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema mauaji hayo yalitokea Novemba 28, mwaka huu saa (kumi na moja)11.00 alfajiri eneo la TRM-minyarani kihesa, manispaa ya Iringa.
Kamanda Mungi alisema kuwa baada ya polisi kupata taarifa walikwenda eneo lilipotokea mauaji hayo ambapo walipofanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa Jophrey Mhongole aliauawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiofahamika na kumweka chini nyuma ya gari lake baada ya kumkuta na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za mwili wake.
Alisema haikuweza kufahamika mauaji hayo yalilenga nini kwani Mhongole alipopekuliwa na polisi alikutwa na fedha kiasi kikubwa(hakutaja kiwango alichokutwa nacho), simu yake ya mkononi pamoja na gari lake.
Alisema kuwa polisi inaendelea kuwatafuata waliofanya mauaji hayo, kufanya uchunguzi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kufahamu chanzo mauaji hayo na kuwa wakikamatwa watafikishwa mahakamani.
Katika tukio lingine mtembea kwa miguu amefariki dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya Rufaaya Iringa baada ya kugongwa na pikipiki isiyofahamika namba wala mtu katika eneo la mnazi mmoja,Kitwiru manispaa ya Iringa barabara ya Iringa/Mbeya.
Kamanda Mungi alisema mtembea kwa miguu aitwae Ektori Kipalile (55) mkazi wa Igangidungu, Iringa Vijijini aligogwa na pikipiki isiyofahamika namba wala mtu Nov.29 saa 3.00 usiku na kufariki wakati akipata matibabu.
Kamanda Mungi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mwendesha pikipiki huyo ambaye hakujali matumizi ya barabara kwa watembea kwa miguu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More