Monday, December 21, 2015

Madiwani wa CUF Kufikishwa Mahakamani Kwa Kufanya Vurugu

Madiwani kumi wa Chama Cha wananchi (CUF) waliodaiwa kufanya vurugu katika uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya jiji la Tanga wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi wa Tanga, Zubery Mwombeji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la vurugu zilizotokana na madiwani wa CUF kupinga matokeo ya uchauguzi huo.

Kamanda Mwombeji alisema kuwa madiwani hao walikamatwa na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Chumbageni na baadaye waliachiwa kwa dhamana majira ya saa sita usiku.

Alisema kuwa madiwani hao walikamatwa kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuchoma pazia na kujaribu kuvunja mlango wa ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.

Madiwani wa CUF wanadaiwa kufanya vurugu katika ukumbi wa halmashauri ya jiji hilo uliotumika kupigia kura baada ya Mkurugenzi wa jiji hilo kumtangaza diwani wa CCM, Mohamed Mustafa kuwa mshindi kwa kupata kura 19 dhidi ya mgombea wa CUF aliyepata kura 18.

CUF walipinga matokeo hayo na kudai kuwa walihujumiwa na kuporwa ushindi hususan kwa kuwa wana idadi ya madiwani 20 dhidi ya madiwani 17 wa CCM.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More