Tuesday, December 8, 2015

TAMASHA LA MPIRA WA MIGUU LA KIMATAIFA LA AMANI LAZINDULIWA IRINGA


ZAIDI ya vijana 150 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati wanatarajia kushiriki katika tamasha la mpira wa miguu la kimataifa lijulikanalo kama ‘SOCCER FOR PEACE’ kwa lengo la kuhamasisha vijana katika kushiriki mchakato wa kuhamasisha amani na maendeleo kwa watu wote.

Tamasha hilo la wiki moja linalojumuisha vijana wa kike na kiume kuanzia umri wamiaka 14 hadi 17kutoka mashirika 16  kwa uratibu wa wa mtandao (SREET FOTBALL WORLD) linalojumisha mashirika ziidi ya 100
yenye lengo lengo la kutumia michezo kuhubiri Amani limezinduliwa mkoani mkoani Iringa na  uhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo

Akizungumza na wandishi wa habari katika uwanja wa kimataifa wa FIFA mjini hapa mwenyekiti  wa kongamano hilo kutoka nchini Kenya Gishuku Fransisi alisema kuwa lengo la kuwakutanisha vijana hao ni kataka kuwajengea utamaduni wa kuhubiri Amani tangu wakiwa watoto

Fransisi alisema kuwa kwa kutumia michezo ni rahisi kuwafundisha watoto wadogo kudumisha Amani kwani kama watoto hao wangefundishwa kupendana tangua wakiwa awali hakuna nchi ingekuwa na vita kwani
wengekuwaa wameshaandaliwa toka mapema kuwa binadamu wote ni sawa

 “Ukitazama nchi  za wenzetu kule kwao kila siku ni vita na wanawatumia watoto  kwenda kupambana na kama hakuna Amani basi hakuna
maendeleo ,kwa mfano mzuri tu ni kama nchi ya  Rwanda na Burundi walitakiwa kushiriki lakini wameshidwa kufika kutokana na vita iliyoko huko hivyo ni vema tukaanza kuwafundisha watoto kulinda na kudumisha
Amani kupitia michezo


Kwa upande wake mkurungenzi wa shirika lisilo la kiserekali la IDYDC Dk  John Mkoma ambao ndio wenyeji wa shindano hayo lisema lengo la kuleta mashindano hayo hapa nchni ni moja ya kuenzi utamaduni wa watu wa Tanzania na kuuonyesha ulimwengu jinsi nchi ya Tanzania walivyoweza kulinda  na kudumisha Amani yao

Nkoma alisema kuwa kwa kupitia kuongamano hilo watoto hao watajifunza mambo mbalimbali ikiwemo kujisimamia wenyewe katika kutunga sheria zao katika soka kwani katika michezo hiyo  itakayokuwa ikujumuisha wavulana watatu na wasichana watatu kutoka kwa kila timu kutakuwa hakuna muamuzi bali watakuwa wakijiamulia mwenyewe kwa kutumia busara na weledi wao wenyewe ili kujenga usawa na bila kubaguana

Nasma  Masudi ni mmoja kati ya washiriki kutoka ipogoro mjini Iringa waliohudhria kongamano hilo yeye anasema kuwa “ michezo ni ajira michezo inamjenga mtu kimwili ka kumuepusha na mambo mbalimbali kama madawa ya kulevya na ngono zembe mategemeo yangu nikitoka katika kungamano hili nitakuwa ni mtu mwingine kabisa katika tasnia hii ya michezo.

Masudi aliwashauri wazazi kujenga utamaduni wa kuwaruhusi watoto wao kishiriki katika michezo mbalimbali kwani wazazi wengine wanadhani kuwa mwanafunzi kushiriki michezo kutamsababishia kufanya vibaya katika msoma yake jambo ambalo siyo la kweli Katika kongamano hilo la aina yake  dk Nkoma alisema kuwa mshindi wa kwanza katika kongamano hilo atapatiwa kikombe ,mshindi wa pili akipatiwa medali na mshindi wa jumla atapatiwa kikombe pamoja na medali.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More